Nishaurini kati ya Dstv na Azamtv ninunue kisimbuzi gani?

Nishaurini kati ya Dstv na Azamtv ninunue kisimbuzi gani?

Napenda mipira yote ya bongo na ulaya, king'amuzi gani kinafaa hapo kwa huu uchumi wa kati? Naombeni ushauri
Mkuu nakushauri nunuwa dstv,
Nilikuwa na azam TV,,tena fully package cha 35000.

Lakini hakina maajabu yeyote.
Nimerudi kwenye dstv..

Good quality ,
Good programs,

With dstv there will be no regrets.
 
Kama unataka kusikia kelele za vijana wasiojua kuchambua au kutangaza mpira tumia azam. Kama unataka quality mbovu ya sautu tumia azam.

Ila kama unataka burudani nyumbani kwako tumia dstv jaza ile yenye espn ili tutazame basketball, hokey, American football zote za wamerikani.
 
Kama unapenda maudhui ya mashariki ya kati nunua Azam
 
Kwa king'amuzi cha Azam utaidi yafuatayo:

1. Ligi kuu bongo
2. Azam federation cup
3. Caf champions lg na shirikisho - group stage
4. Carabao cup England ( all matches)
5. FA cup England (all matches)
6. Ligue 1 - France
7. Bundesliga - Germany
8. Ligi kuu uholanzi ( Eredivisie)
DSTV haya yote yapo + EPL.
......then Azam kila jmosi huwa wanaonyesha game moja ya England
 
Uzuri dstv vifurushi vikubwa vikubwai huwa naweka nyakati za likizo kwa watoto na nyakati za sikukuu kama vile Kristmas na Mwaka mpya, pasaka hivyo, hizo zingine za kawaida naweka nyakati za kawaida mambo ya mipira nacheki bar maisha yanasogea
 
Ili uwe huru uache kigombania remote na madogo au wife, inabidi uwe na zote mbili DStv & Azam
 
Jamani ebu nipeni uzoefu kuhusu dstv maana nilikuwa najaza kifurushi changu cha 29900 napata channel kibao kama magic bongo , national geography na vinginevyo vizuri tu ... Lakini sasa nimeweka Kama wiki hivi imepita kifurushi cha 29900 zaidi naona wasafi tu ,,, kama kuna mtu anafahamu channel nyingne za maana anielekeze aisee
 
Back
Top Bottom