Nishawai toka Kyela hadi Mbeya na Manzi na sikumsemesha neno lolote. Alinikuta nimekaa hakusalimia nikasema wacha niupokee huu mpira kama ulivyokuja

Unajua umri nao unakuwaga tatizo sana nakumbuka nilikuwa kama na miaka 20 hivi,naye alikuwa sister du fulani wa miaka hiyo
Nina visa vingi,hii ilikula kwangu,Nilikuwa nimetoka Maputo napitia Lilogwe to Dar,sasa nilipofika lilogwe kulikuwa na Mabasi ya kampuni ya Taqwa yanayokwenda Dar,na hapo lilongwe palikuwa na wabongo wengi sana wake kwa waume,yaani ukifika kwenye mtaa mmoja unaitwa devil street ni kiswahili tu,
Basi nikapata basi mapema tu,ilikuwa kama saa moja usiku na basi linaondoka saa mbili,baada ya mda akaja dada mmoja wa kitanzania akaniambia umekaa kwenye siti yangu,nilikuwa nimekaa dirishani,nikamwambia siti yangu,akataja namba yake ya siti na mimi nikaitaji hiyoyo kwa kumzingua,ikabidi akamuite konda,alipokuja konda nikampisha,lakini nikamwambia huko ndiko mabasi yanakopigwagwa pasi,
Safari ikaanza kila mtu kamchunia mwenzake,dada mzuri,si unajua wafanya biashara,basi baada ya kama masaa matatu nakaanza kujisikia homa natetemeka mpaka yule dada ananisikia,akaniuliza vipi unaumwa,nikamwambia ndiyo,una dawa hapana,akatoa dawa akanipa,nikawa nimezishika tu,niakulizwa tena unamaji sina,akanipa niakanywa hapo hali ikatulia nikapata usingizi,bado tuko kimya na usiku kama saa tano hivi,
Niasema basi ikifika mji mmoja unaitwa Mzuzu nitaenda kumnunulia maji yake nimrudishie,kweli niakanunua maji kumpa akakataa,niliona aibu sana hapo milango kama ya saa nane,tukafika borde ya Malawi Songwe alfajiri saa 12 ikabidi tuanze storie sasa na kupiga supu wote,kugonga paspoti hapo tukaanza safari ya Kasumulu tu.Dar kalibu masaa 15 tulipiga storie sana mpaka safari ilikuwa fupi kulaliana ruksa,dada akaishia kunipa namba yake ya simu,kipindi hicho simu za mkononi,call box, alikuwa anakaa sinza mimi nafikia Guest,kutokana na protocol ya biashara yangu sikumtafuta tukaishiana hivyo ilikuwa mwaka 1998 kama sikosei
 
Mtoa mada mbona unazingatia vitu vidogo vidogo hvy
 
imekaa poa sana ila huyo mwanamke ni mtu mwenye exposure sio hawa mapasua
 
Uungwana huo tunaita.
Umefika pahala umekuta mtu,ukisalimu hufi,ni jeuri na uhuni tuu tusidanganyane.

Sasa kama uliona salamu ni kazi jiulize wewe mwenye huduma unazotaka.Ya nini kunisumbua?Upuuzi huo mkubwa sana.

Salimia jirani yako vyema kama mko kwa safari au pahala.
 
Unapokuja kwangu inamaanisha wewe unanihusu lazima nikusikilize, tunapokutana kwenye bus wewe hunihusu wala mimi sikuhusu, sihusiki wala uhusiki na chochote kwetu
Duuh kweli tuko tofauti daktari wangu....

Ujirani unaweza kuwa kazini...
Ujirani unaweza kuwa wa viti kanisani...
Ujirani unaweza kuwa wa zuliani msikitini....

Unaposema ujirani wa safarini haukuhusu basi tambua linaweza kutokea jambo la dharura humo safarini na huo UJIRANI usioutaka ukawa na manufaa....iwe ajali ,iwe usafiri kuharibika njiani,meli kupata dharura majini....
Mnaweza kushirikiana kwa kupeana moyo ama hata kuomba maombi/dua kwa pamoja ha ha ha ha katika nyumba za ibada inapoombwa dua mnaitikia AAAMIN kwa huo ukaribu wa ujirani hapo.....

Naheshimu mawazo yako daktari wangu !
 
Daktari wa nini
 
sijaelewa, boda ya songwe, mara kasumulu (which is in kyela), fafanua hapo. hayo maeneo tunayajua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…