Nisome kozi gani ambayo inaajira kwa baadae?

Nisome kozi gani ambayo inaajira kwa baadae?

Dogo kacheki kama unaweza ku qualify ukasomee certificate of East African Custom clearing and forwarding chuo cha Tax utatoka tuu achana na kupoteza muda na computer
 
huyu akasomee ufundi cherehani utamfaa
 
Sio ajira tu! !
Chagua kozi yenye muendelezo huko mbele ili mambo yakikaa vizuri uongeze elimu pia.
 
Jaman magreat thinkers ninaombeni msaada wenu. Nimemaliza kidato cha nne mwaka jana na kwa bahati mbaya nimepata 4 ya 32 na inanipasa kwenda chuo sio form 5. Je ni kozi gani itakayo kua na ajira hapo badae?
Nenda Veta ukasomee Welding and Metal fabrication. Utafika tu mdogo wangu
hawa wanaokushauri vibaya wasikukatishe tamaa.
 
Huo uandishi wako tu ndio maana ulifeli.Inawezekana hata kwenye mtihani uliandika "Xo" badala ya "So".Uandishi huo wa kisharobaro unaboa sana eti "xaikolojia".P****fu sana!

wanaboa sana utafiki keyboard haina S bhana
 
Mbona mnamdis wakati kafaulu vizuri tu, na uhakika una C mbili au tatu na D za kutosha, omba eduation au nursing kama ulisoma masomo ya science utapata
 
Dogo usiende kusomea ajira. Wengine tuna degree zaid ya moja lakini ajira hamna. Somea ujasiriamali mdogo wangu.
 
ajira haina formula mdogo wangu, unaweza kuona kozi ina soko kwa sasa lakini ukianza kuisoma leo mpaka uje kumaliza unakuta haina wadau tena. kila kozi inalipa(ukipata kazi), ndio maana zikawekwa na watu wanazisoma kila mwaka. siwezi kukushauri usomee kozi fulani halafu ukiisoma na baadaye ukikosa ajira, utaishia kunilaumu tu. kitu kingine ni kwamba, siku hizi kupata ajira bila kuwa na 'refa' utapata tabu na kama huna akili ya kujiajiri ndo utaimba haleluya.
 
Dogo unapenda computer kusoma na unataka upate ajira haraka sasa mimi kwa ushaur wangu tu fikiria juu ya fani hizi kwa sasa Elimu,Afya na Kilimo na mifugo ukitaka makuu utaishia kuingiza nyimbo kwenye simu na kuchoma CD

mkuu umenifurahsha!
 
vyovyote utakavoamua soma,ila panga kujiajiri pia
 
Jaman magreat thinkers ninaombeni msaada wenu. Nimemaliza kidato cha nne mwaka jana na kwa bahati mbaya nimepata 4 ya 32 na inanipasa kwenda chuo sio form 5. Je ni kozi gani itakayo kua na ajira hapo badae?

kasome nursing ndio itakufaa. Au nenda chuo cha serikali za mitaa za Hombolo Dodoma.pia unaweza kupata ajira ukihitimu japo kuna gharama kubwa.
 
Dogo unapenda computer kusoma na unataka upate ajira haraka sasa mimi kwa ushaur wangu tu fikiria juu ya fani hizi kwa sasa Elimu,Afya na Kilimo na mifugo ukitaka makuu utaishia kuingiza nyimbo kwenye simu na kuchoma CD

Makuu ni yapi hayo chief?

Ledson,
Ningependekeza mtu awe na malengo ya kujifunza zaidi ya fani moja. Ujuzi wa fani mojawapo mhusika aweze kuutumia kwenye fani ya pili, mfano ukasoma Ualimu na baadae IT. Au Uhasibu + IT. Wadau hapa watatoa mifano mingine.

Pia, kutambua kwamba kuajiriwa sio hatua ya mwisho. Unaweza kuajiriwa na ukafanya shughuli binafsi on the side. Baada ya hapo unaweza kurudi shule kujiendeleza. Pengine ukatoka hapo ukaacha kazi ya kuajiriwa ukaunganisha nguvu na mtu mwingine mkafungua shughuli yenu binafsi. Baada ya muda mkaanza kuajiri wengine.

Wameshauri hapa kwamba ni muhimu ukarudia upate credits walau 3 sasa (na sio baadae). Nami naafiki.
 
Back
Top Bottom