Nissan Dualis Imetembea Non Stop Dar to Musoma

Mkuu sio kweli huwezi kutembea umbali huo non-stop au hamuelewe maana ya non-stop?

Non-stop maana yake hakuna kusimama sasa wewe kweli ulitembea bila kusimama?
 
Mi mwenyewe nawashaa hao washauri najiuliza hivi hawa ni drivers kweli au washindia vijiweni?
Pale kwenye dashboard kama hapajaku-alert cho chote utaipumzisha kisa nini na ni ngumu Dar - Musoma non stop!
 
Asante kaka kwa maelezo yako.
Hii Gari ni taam sana kwenye mkeka.
Imetulia vibaya mnoo.Na Dereva yuko so comfortable.
 
Manure ya hiyo gari inasomaje? Ikiruhusu hamna shida, unao wahoji na wanao toa ushauri sio ma-expert wa hiyo gari! Gari sio kama pikipiki trailer 90, eti saa 4 halafu uzime, hata 48hr haina shida iwapo tu ulitia oil bora!
 
Manure= mbolea ya wanyama/samadi.
Nadhani ulimaanisha MANUAL....(kitabu cha maelekezo..)
 
Wakuu zangu nimetembea na Nissan Dualis Mpaka Musoma pasipo kupumzika na kuizima.

Je, vipi kuhusu Gearbox yake kwa Skendo za kufa? Kweli imenifurahisha na imetembea sana.
Kawaida tu. Ata Passo, Vitz, zote zinafika vizuri tu. Bila shida. Magari ya sikuhizi engine imeboreshwa sio maajabu hayo. Ila DUALIS sio gari bado kwa Tanzania. Ipo siku utajua.
 
Wakuu nimerudi salama kutoka Musoma.Gari imetulia na haina shida.Weekend hii nategemea kupeleka Service na kuendelea na maisha mengine.
 
Mimi pia sishauri gari yenye engine ndogo kutembea umbali mkubwa bila kuipumzisha,ingawa kitaalamu sio mjuzi sana...
 
Hii gari inasemwa vby Sana[emoji848]
Kuna uzi nilileta humu kuomba ushauri kuhusu hiyo gari.

Kuna watu walitoa shuhuda zao... na kuna ambao walisagia vibaya mno! [emoji23]

Mwisho wa siku nikavuta chuma.

Nilichogundua, comments nyingi kuhusu magari hapa JF ni maneno ya vijiweni na ushabiki tu!

Nissan Dualis ni gari nzuri sana!
 
Binafs Sijawahi hata kuzijaribu,
naziona tu barabarani zinatembea
 
Umetoa ushauri mzuri sana.

Lakini Kinachounguza hizo gari hakihusiani kabisa na wiring!
 
Mi mwenyewe nawashaa hao washauri najiuliza hivi hawa ni drivers kweli au washindia vijiweni?
Pale kwenye dashboard kama hapajaku-alert cho chote utaipumzisha kisa nini na ni ngumu Dar - Musoma non stop!
Tena kwa Dualis, Temperature iko pale ina display kidigitaly kabisa!
 
Kawaida tu. Ata Passo, Vitz, zote zinafika vizuri tu. Bila shida. Magari ya sikuhizi engine imeboreshwa sio maajabu hayo. Ila DUALIS sio gari bado kwa Tanzania. Ipo siku utajua.
Acha hizo...
Niko nayo huku mkoani, rough road 30km then lami 52km (kwenda na kurudi ni 60km rough na 102km lami) three times a week, na inakaribia mwaka sasa haisumbui chochote!

Hiyo gari ni ngumu tofauti hata na muonekano wake!
 
Nakubaliana na wewe mpaka asaivi na dunda nayo mtaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…