Nissan Dualis inagonga ukikata kona

Nissan 5w30
Hiyo ndiyo oil recommended na manufacturer?Nina wasiwasi mkubwa kuwa hutumii oil ambayo ni recommended na manufacturer,nimefuatilia oil ambayo ni recommended kwa Nissan dualis lakini sijaona yenye viscosity hiyo.Nakushauri rudia kuangalia manufacturer anarecommend oil ipi kwa Nissani dualis!
 
Na me nakazia hapo kwenye CVT joint.
 
Anasema inagonga akiwa anakata kona sio kwamba inatoa huo mlio wa kha kha kha
Mmh may be...[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]

Ila changamoto ya watu wengi wanashindwa kutoa maelezo ya matatizo yanayowakumba na ndiyo maana sometimes unakuta mtu ananunulishwa spea ambayo haijafa.

Fundi mzoefu kama kachoka ukimuambia tu gari langu linagonga nikikata kona, atakujibu kwa urahisi... stabilizer link imekufa, ball joint imekufa au kitu kingine kinachohusiana na mfumo wa Suspension..

Kugonga (knocking sound) inatokea kwenye ball joint mbovu, Shock up mbovu, stabilizer link mbovu, wish bon bush mbovu, steering rack mbovu n.k...

Kuna milio ambayo kama kitu kinavunjika au kusuguana.(clicking au clanking noise) Hii hutokea kwenye cv joint...

Hivyo huenda mleta mada kusikia clanking noise akachnaganya na knocking sound...

Endapo mmiliki wa gari hajaelewa mlio upi ni upi, mwishoe kama fundi ni mvivu wa kukagua, utanunua spea ambayo siyo...kama huko juu kuna watu wamesema ni wheel bearing ndiyo mbovu...Wheel bearing haigongi ikifa..balli inatoa Whine sound na kusababisha wobbling endapo itakuwa imechoka sana.
 
Mchawi wa cv joint ni
Boot rubber kupasuka na kumwaga grease, kisha vumbi liingingie na maji...maji yanaingia kwa urahisi kwa sababu tunaosha magari na kupita kwenye madimbwi.

Fundi alipoweka rubber mpya, aliweka na grease mpya pia...hiyo grease ndiyo ilisaidia isilie kwa siku hizo mbili kisha mlio ukarudi pale pale kwa sababu tayari gololi za cv joint zilishasaga zile njia zake.

Nadhani tatizo bado ni hiyo cv joint kwa 90%...

Eneo la kwanza kucheck liwe hapo, fundi akijiridhisha kuwa haijafa, basi kagua suspension parts...
 
Nakazia hapo kwenye cv joint
 
Nakazia hapo kwenye cv joint
Mimi nina gari ya Nissan station wagon ya miaka hiyo ya zamani ambayo ilitengenezwa kwa ajili ya matumizi ya Ulaya, ukikata kona kuzidi angle fulani inatoa mlio bila kuwa na ubovu wa kitu cho chote.
 
Mimi nina gari ya Nissan station wagon ya miaka hiyo ya zamani ambayo ilitengenezwa kwa ajili ya matumizi ya Ulaya, ukikata kona kuzidi angle fulani inatoa mlio bila kuwa na ubovu wa kitu cho chote.
Nakubaliana na wewe hata kwenye nissan navara na hardbord hua zinatoa mlio huo ukikata kona kuzidi angle hata hivyo arudi tu kwa fundi amchekia hiyo CV joint maana kwa hizo gari za nissan mara nyingi rubber boot ikipasuka huwa CV joint zake zinaharibika mpaka uweke nyingine mpya hata fundi akisafisha na kuwekea greese haichukui muda imenitokea sana kwa nissan navara
 

Stablizer link za Rav4 Miss TZ zinaweza kuwa bei gani? maana umetaja dalili hapa naona kabisa sina links
 
Stablizer link za Rav4 Miss TZ zinaweza kuwa bei gani? maana umetaja dalili hapa naona kabisa sina links
Genuine sijui itakuwa bei gani ila hizi za kawaida wanaazia 30k na kuendelea kulingana na aina na ukunwa gari..
 
Umeongea sahihi kabisa.
 
MREJESHO

Nilifanikiwa kwenda kucheki na tatizo lilikuwa ni CV joint, baada ya kubadilisha tatizo likaisha.

Nawashukuru sana wote kwa mawazo yenu, yamesaidia sana.
Tunashukuru na kukupongeza kwa mrejesho...
Hiki ndicho kitu kinachotakiwa na kitasaidia wengi.

Kuna watu wakishapewa ushauri, wakifanikiwa au wasipofanikiwa, hawaleti mrehesho..

Hawajui kuwa haya mawazo na mrejesho ni reference kwa watu wengine watakaokutana na changamoto kama hizo..
 
Kabisa mwenyekiti wetu wa Nissan ngazi ya taifa.
 
[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
Kuna bwana anaitwa Extrovert yule anatakiwa awe mwenyekiti wa Toyota ngazi ya taifa..
@Extrovert nimeshazungumza nae. Tatizo anaogopa sana gharama sasa nimeshamwambia kuwa sisi huku team Nissan, VW, Audi, BMW na Mercedes Benz huwa tuna connections nyingi sana. Hatuwezi kumtazama member mwenzetu anakosa pesa ya services tutamtupia muamala bila shida.

Ni swala la muda tu atahama atakuja tulipo.
 
Kuna siku atakaribia tu kwenye brands nyingine..[emoji16][emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…