Nissan Dualis: Msaada mwenye uzoefu na hili gari naomba ufafanuzi

Nissan Dualis: Msaada mwenye uzoefu na hili gari naomba ufafanuzi

Mkata-tamaa

Senior Member
Joined
Nov 21, 2018
Posts
180
Reaction score
312
1596259818394.png

Picha: Nissan Dualis

Wakuu nianze kwa kuwasalimu na kuendelea kukumbushana pia kuhusu namna ya kujikinga na hili gonjwa la sasa.. Corona

Naomba nije kwenye topic kuu sasa.

Nimekuwa nikitamani sana kumiliki gari lililo juu juu (wenyewe wanaita SUV), kutokana na mazingira niliyopo, gari la chini linaumia sana.

Nimejipanga nimepata 15Mil, kuna mdau akanishauri kwa bajeti yangu gari la juu juu ninaloweza kupata ni ilo gari tajwa Nissan dualis

Sasa nimekuja kwenu wataalam kuomba ushauri pia kabla sijafanya maamuzi ya kununua ilo gari

  • Ni kweli naweza kupata nissan dualis kwa bajeti ya 15Mil?
  • Vipi kuhusu vipuri vyake?
  • Uimara wake upoje?
  • Shida na matatizo ya hili gari ni yapi?
  • 15km kwa lita moja, fuel consumption ni kweli?
  • Kuna SUV yoyote ninayoweza kupata kwa bajeti ya 15Mil?
  • Kuna model ngapi za hili gari?

Nakadhalika nakadhalika, naamini kupitia JF, nitapata mawazo na ushauri mzuri kabla ya kufanya maamuzi

Nilichokifanya mpaka sasa nimegoogle tu nikaliona muonekano wake na likanivutia pia kimuonekano

Natanguliza shukrani zangu kwenu wakuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio mtaalamu wa magari niseme nitayajibu maswali yako mkuu. Nichokoze mada.

Kwa muonekano ni kagari kazuri na portable saana. Niseme napenda muonekano wake.

Parts...nina wasiwasi maana bongo sijayaona mengi.

Ulaji wa mafuta....kuna ndugu yake wametoka kabila moja hilo hilo la Nissan anaitwa Primera...tank halijai na ni kama umemwagia maji kwenye mchanga. Hili lilinifanya niogope jina Nissan.

Kwa muonekano nje na ndani nalipa 98%. Sema naona wapenda Nissan wanakimbilia saana Qashkai (sijui nimepatia jina) kuliko Dualis
 
Sio mtaalamu wa magari niseme nitayajibu maswali yako mkuu. Nichokoze mada.

Kwa muonekano ni kagari kazuri na portable saana. Niseme napenda muonekano wake...

Mkuu asant kwa ushauri wako, ngoja nione wadau wengine watanishauri vipi
 
Nitajibu kama ifuatavyo:

Uimara
Magari yote yaliyotengenezwa miaka ya 2004 na kuendelea yanafanana kwa asilimia kubwa uimara wake bila kujalisha make...yaani ni magari ambayo uimara wake unategemea na unavyolitunza......Usitegemee dunia ya leo kupata SUV ngumu kama Jeep zilizotumika kwenye Vita vya Vietnam..

Upatikanaji wa vipuri
Vipuri vya sehemu nyeti kama engine, miguu vinapatikana kwa sababu kwa asilimia kubwa vinavaliana na X-trail ambazo ni nyingi sana....Ila bei ipo juu kidogo..body parts ndiyo changamoto mfano taa,vitasa n.k.

Ulaji wa mafuta
haijaachana na wakina xtrail, rav 4 na SUV nyinginezo za saizi hizo..

Model zake
Hii ndiyo generation ya kwanza kwa bongo bado hatujapata generation ya pili...Ulaya na America inauza kama Nissan Quashqui..

Ground clearance
Ipo poa sana hivyo inamudu barabara mbovu...

Ubaya wake
Ukitaka kuliuza mteja hapatikani haraka, na bei ya kuuzia si nzuri kwa sababu Tanzania Toyota ndiyo zinapendwa zaidi ikiaminika kuwa hata masikini anaweza kumiliki toyota.

General conclusion
Nissan dualis ni gari nzuri kama wewe ni mpenzi wa Nissan...au kama umechoshwa na Rav 4, Clugger, basi Dualis ni mbadala mzuri..
Karibu NISSAN..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,

Kwa hiyo pesa dualis unapata. Ila kwa nijuavyo mimi utapata model ya kwanza yaani gari za 2007 ukizidi sana utapata za 2008. Kuanzia model ya 2009 inaweza kuwa ngumu kdg.

Kama wewe ni mpenzi wa Nissan, lets enjoy the ride.
 
Boeing 747,
Mkuu asante sana kwa maelezo yako,yamenipa mwanga mzui sana

Kiukweli apo kwenye kuliuza hata mimi nilifaham ilo,maana watz ni vigumu kuwaconvince kingine tofauti na Toyota

Ningetamani sana nichukue mbadala wake (Rav4,Clugger etc) sema kwa bajeti niliyonayoya 15mil sidhani kama nitaweza kununua magari ayo niliyoyataja.
 
Mkuu,

Kwa hiyo pesa dualis unapata. Ila kwa nijuavyo mimi utapata model ya kwanza yaani gari za 2007 ukizidi sana utapata za 2008. Kuanzia model ya 2009 inaweza kuwa ngumu kdg.

Kama wewe ni mpenzi wa Nissan, lets enjoy the ride.


Mkuu toleo la kwanza la 2007 lina utofauti upi na matoleo yake ya mbele?

Ningefurah sana kufahamu jambo hili pia
 
Watu wanaogopa hio CVT ndio maana demand yake imeshuka.
Ukifuatilia Japanese cars, utagundua Nissan waliwahi kutumia technology mpya ya CVT kabla ya Toyota....sasa cvt za nissan zilipoingia mtaani,mafundi wa mwembeni wakaziponda na kuwaanisha watu ni mbovu, kumbe wao ndiyo wabovu...walizoea kuchokonoa Ordinary Automatic Transmission za Kwenye Corolla na Carina..

Nadhani wanaogopa CVT kwa sababu mbili kubwa...
1. Wabongo tunapenda vitu vya bei rahisi...mtu anataka kumwaga oil ya gear box asitumie zaidi ya 80k...
Kwa upande wa CVT lazima ujipange, oil peke yake maeneo mengi ya TZ haipungui 130k kwa gharama za chini, hapo bado hujamlipa fundi..

2. Elimu...Nimegundua wamiliki wengi wa magari hawana elimu ya kutosha juu ya magari wanayoyamiliki...mtu haelewi gari lake lina gear box ya mfumo gani, yeye anachojua ni kushift kutoka P na kwenda R au D...Mafundi nao hawana elimu ya kutosha....
Umeshawahi kujiuliza kwa nini watu wengi siku hizi wanaomiliki Toyota latest hawakawii kuua gear box...?

Unakuta Toyota imekuja na VCT gear box, siku ya service wanaweka cheap ATF kutoka PUMA Patrol station....Walishakariri Carina zinatumia ATF za pale Puma, basi wanaweka hizo hizo kwenye Passo, IST na nyinginezo....hawana taarifa kuwa hata hizi passo na ist zipo za CVT..

Conclusion
CVT ni transmission nzuri sana ukiweza kuitunza na kuipa fluid yake iliyopendekezwa kwa sababu inakupa smooth driving bila kusikia mshtuko wa kubadilika kwa gear.

Hivyo nimawaasa watu wawe waangalifu, CVT kwenye Nissan zimeshakuwa common, kwa sasa zinakuja kwa kasi kwenye baadhi ya Toyota, Mitsubish na Suzuki. Wale wamiliki wa Toyota wanaopenda cheap services kutoka Puma petrol station, mtaua gear box zenu kila siku.

Soma kwenye kweny deep stick ya oil ya gearbox uone umeambiwa uweke fluid ya aina gani, ufanye hivyo na si vinginevyo.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukifuatilia Japanese cars, utagundua Nissan waliwahi kutumia technology mpya ya CVT kabla ya Toyota....sasa cvt za nissan zilipoingia mtaani,mafundi wa mwembeni wakaziponda na kuwaanisha watu ni mbovu, kumbe wao ndiyo wabovu...walizoea kuchokonoa Ordinary Automatic Transmission za Kwenye Corolla na Carina....

Nadhani wanaogopa CVT kwa sababu mbili kubwa...

Nimependa ufafanuzi wako ila kwa kuongezea tu hata Subaru wanatumia sana hii technology ambayo kwa dereva wa kawaida utagundua pale unaporndeaha hutasikia gear zikishift


Sent using Jamii Forums mobile app
 
CVT kwa maana ya continously variable transmission au nini? Maana hii haijawahi kuwa tatizo kwa gari nyingine


Sent using Jamii Forums mobile app
Yes kwa maana hio hio,Nissan ni pioneer wa hio CVT, so watu wengi wa mwanzo hawakuelewa utofauti wa CVT na hizo AT tulizozoea wakawa wanaweka nornal ATF wakawa wanaziua sana lkn pia Nissan Murano 1st gen zilikua baadhi zima matatizo toka kiwandani na zilikua recalled
 
Ukifuatilia Japanese cars, utagundua Nissan waliwahi kutumia technology mpya ya CVT kabla ya Toyota....sasa cvt za nissan zilipoingia mtaani,mafundi wa mwembeni wakaziponda na kuwaanisha watu ni mbovu, kumbe wao ndiyo wabovu...walizoea kuchokonoa Ordinary Automatic Transmission za Kwenye Corolla na Carina...
Naunga mkono hoja zako kwa 100%
Nissan ni pioneer wa hio CVT, so watu wengi wa mwanzo hawakuelewa utofauti wa CVT na hizo AT tulizozoea wakawa wanaweka nornal ATF wakawa wanaziua sana lkn pia Nissan Murano 1st gen zilikua baadhi zima matatizo toka kiwandani na zilikua recalled
 
Mkuu jaribu pia kufikiria gari inaitwa Toyota RUSH. Ni ya juu kiasi na ulaji wake wa mafuta ni mzuri cz injini yake ni 1490cc.

Kwa upande wa bei kwenye hiyo 15M yako nadhani utaongeza kidogo endapo utaagiza mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app

Weeeee hata hasijaribu hii gari inapata moto sana . Mimi sio mtaalamu ila na jamaa zangu 3 wote wanajuta kununua hii gari. Inatumia mafuta kidogo sana ila inachemka . Watalaamu wanajua sana kesi ya Rush asee.
.....
Kuhusu hii Nissan Dulas me nakushuri ichukue . Kwa sababu za wadau hapo juu sijaona sababu ya maana sana ya kutoichukua.
1. Kuhusu kuuza gari yeyote unauza muda wowote ili mradi uwe mtulivu na pia sio gari ya zamani sana bado ni new model kwa TZ.

2. Spare parts siku hizi sio tatizo kabisa Tanzania . Spare zipo sana na Dunia imekuwa kijiji unaagiza hata wiki haiishi umepokea mzigo wako, hapo kenya pia zipo spare nyingi.

Mwisho niliiona hii gari mara kadhaa niliielewa sana nikakutana na mwanangu mmoja Triple B goba akanipa full details haina tataizo wala usumbufu kabisa japo mimi sio mpenzi wa Nissan.
 
Back
Top Bottom