Nissan xtrail 2500cc inakula sana mafuta

Nissan xtrail 2500cc inakula sana mafuta

Hivi mpaka leo bado kuna watu wananunua third hand cars!! Mara nyingi ukiona m bongo anauza gari ujue either ana shida kubwa ya ghafla au ina tatizo na hatokuambia. Ni vyema ukaenda na fundi wa kuikagua vyema gari na ukapiga round kadhaa kabla hujalipia.
Back to the question, huo ulaji wa mafuta nadhani ni city drive. Jaribu kupiga nayo ruti ndefu uone. Gari zenye cc kubwa ukiendesha sehemu zenye msongamano hutumia mafuta mengi sana. Lakini kwa kwa ulaji huo uliosema, nadhani gari yako itakuwa na tatizo la oxygen sensor.
Ni kweli, nina OBD2, nimescan bila kupata fault code za oxygen sensor. ikibidi nitabadilisha oxygen sensor.
 
Nimebadilisha catalytic converter, nimebadilisha spark plugs, nimebadilisha air cleaner, nimemwaga oil na nimebadilisha air filter na pia najitahidi kujaza upepo kwenye matairi kila unapopungua.
Kuna kitu kimoja umesahau kubadilisha. Badilisha engine. Weka ya 2000cc. 2500cc is already such a hughe engine...
Nenda Kkoo wakuuzie skeleton. Ile block ikiwa complete. Ng'oa vifaa vingine kwenye engine ya sasa ufunge mle. It will cost less.
 
hii gari ni QR25 four cylinder. Sio six cylinder. Manufacturer catalogue inasema gari inakunywa 11.9km/L ila hii sababu imeshatumika sanaa ilibidi iwe angalau 9km/L.
Heeeeeeeee.

Hapo pa 4 cylinder nina mashaka.
 
Ni gari nzuri sana, hazina shida kabisa
Bujibuji hebu funguka in detail hapa utusaidie wengi binafsi nataka nikanunue ka xtrail ila baada ya kuulizia kwa watu naambiwa eti ina engine ambazo ni sensitive sana kwa mazingira ya joto hivyo kibongobongo x trail huwa zinatabia ya kuchemsha😳
 
Mkiambiwa xtrail ni cancer mnabishanaga, hizo gari zina mechanical issues sana na ni expensive kuzi maintain.You must be very lucky kupata ambayo haisumbui
 
Usipokuwa na hela daily kila kitu utakilalamikia, iwe Luku, gari , Bill za maji, Misosi n.k kila kitu utaona kama haiko fair kwako... kama upo smart na hela zipo gari yoyote unamiliki na fresh tu. Tatizo hapa ni hela ya mafuta amini nakuambia
 
Habari wadau,

Nimenunua nissan xtrail cc 2500 kwa mtu, ni modeli ya uingereza imetembea kilometa 136,000

Nilivonunua tu nilijaza full tank, cha ajabu nimetembea kilometer 200 taa ya mafuta ikawaka. Nikaenda kujaza tena full tank, ilichukua lita 51 kujaza full tank kwa mara ya pili.

Hivo km 200/51 ni sawa na kilometa 4 kwa lita moja.

Hii gari inatembea Kilometer 4 kwa lita moja.

Nimebadilisha catalytic converter, nimebadilisha spark plugs, nimebadilisha air cleaner, nimemwaga oil na nimebadilisha air filter na pia najitahidi kujaza upepo kwenye matairi kila unapopungua.

Lakini bado tu fuel consumption iko vile vile. Kwa wenye utaalamu hebu nipeni ushauri niangalie kitu gani tena ? au kama kuna fundi mzuri unamjua hebu nipe mawasiliano yake.
Check timing
 
Back
Top Bottom