Nitafurahi Kilimanjaro Stars wakipandishwa kwenye lori kurudi nyumbani baada ya mechi ya mwisho, wametuaibisha mno!

wasubiri wakishapanda mashua/boti lao litungue ili watumbukie baharini.....tumewachoka. Yaani hawa kuwapandisha lori ni kama vile kuwapendelea tu, wanahitaji boti lililo oza kabisa si vinginevyo.
Kweli mkuu hawa watu wametuaibisha..
 
Tanzania kama nchi imewahi kufanikiwa katika lipi kiasi tuwabebeshe lawama vijana wasio na elimu hali ya kwamba hata tuliowagharamia elimu wanaboronga?

Tuanze na maprofesa wetu kwanza, maana kwa wenzetu Vyuo Vikuu ni sehemu za mavumbuzi, kwetu ni ofisi za kuchukulia mshahara.
 
wale nyumbu wanaotokaga kenya wanapita masai-mara wanatokea serengeti watapita mwezi wa ngapi wawasubiri tu wachezaji wetu wavuke nao?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hapa ni soka hayo ya siasa tulishachoka nayo.
 
Wachapwe bakora hadharan..mbele ya umati wa watu sokon
 
Sijakuelewa mkuu..
Kwenye heading umeandika Taiga stars halafu humo ndani umeiongelea Kilimanjaro stars

Au hakuna tofauti mkuu??(nadhani utanielewa sasa)
Zingatia: Taifa Stars=Kilimanjaro Stars +Zbar Heroes
 
Yaani nina hasira na kile kikocha chao kinajifanya kuishi kwake ulaya tuonekane mazuzu anakera na mipango yake ya ajabu.

Kwanza naomba hata wapotee huko Machakos tutafute timu mpya ya taifa yenye vijana wenye uchu sio hawa wazee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…