Nitafutieni waziri yeyote kwenye serikali ya Marekani ambaye jina linaanza na Profesa

😂😂
 
Prof. Makame
Prof. Tibaijuka
Prof. Kabudi
Prof. Ndalichako
Prof. Muhongo
Et al
Prof. Jay Wa Mitulinga
Prof. Majimarefu (RIP)
Prof. Baba Levo
Prof. Mwijaku
Dr. Masanja Mkandamizaji
Dr. Cheni
Dr. Mkoloni, etal...
 
Hata ukifundisha community college utaitwa professor.

Watanzania bado wana ulimbukeni sana na hizi titles.

Wengine wanasema eti Obama Juris Doctor lakini hajiiti Dr.

Hawajui kuwa hiyo Juris Doctor haina hadhi sawa na PhD, kwa Marekani.
Yule bidada wa Spelman naye alikuwa anafundisha chuo, Professor.

Nilikuwa namtuliza Professor.

Siku moja akanialika niende chuoni kwake anapofundisha nikaangalie anavyofundisha, nikaenda. Nikakaa darasani namuangalia anavyofundisha.

Halafu tunarudi nyumbani na mimi namfundisha 😂😂😂
 
Kibongo bongo hiyo title ina maana sana Prof. Stroke.
 
Nyerere alikuwa degrees nyingi za heshima kuliko Samia. Pia elimu yake aliisomea vizuri sio ya kuungaunga pale Makerere, Edinburgh. Samia ukimuuliza amesoma wapi ni kasheshe kupata jibu la kueleweka.Leo tumepata malimbukeni kila mmoja anajiita Dr, Pro, Wakili msomi.

Nyerere hakuwahi kujiita professor, alitaka aliitwe mwalimu tu.
 
CPA ni title za kipuuzi sana Wala hazipo duniani ni utaahira wa tz TU! Rubbish sana!
Hivi vitu vimeanzishwa na malimbukeni miaka ya 2010 huko kujiita hata haya majina. Wakina mengi walikuwa maccountants wa kimataifa, Lamwai, Mkono mawakili wa kimataifa, hawakujiita wakili msomi. Hivi ni mbwembwe tu za wahuni.
 
Ukiachilia mbali hilo la watawala, kuna upuuzi mwingine wa hawa graduates masomo ya sayansi hadi wa DIT nao hupenda kujiita Engineer.
Yanni tumekuwa nchi ya hovyo sana kwa kuabudu vitu visivyo na tija halafu vyenye tija tunavipuuzia.
 
Hawa wakwetu wanajivika hayo majina ili kutetea maamuzi yao ya kipumbavu, kumbuka
  1. Prof wa Vinyesi Mara
  2. Prof wa Singeri kutoka Jalalani
  3. Kuna mwingine alitajwa na Mwendazake kuwa ni wa hovyo
 
Kwahiyo kwa Marekani Dr ni title kubwa kuliko professor. Hapa kwetu sasa majina makuubwa but when it comes into result orientation bure kabisa😀😀
Imejazana tu serikalini hakuna lolote lenye tija katika kuboresha jamii za watanzania😪
 
Kwa Marekani Dr. inajulikana kuwa angalau una Ph.D, wakati Professor ni mtu anayefundisha chuo kikuu tu.

Marekani unaweza kuwa una Masters tu huna PhD, wewe ni Professor kwa sababu unafundisha Chuo Kikuu, hata Community College kama alivyosema Nyani Ngabu.

Na pia, watu hawashobokei kuitwa Dr. au Professor nje ya mazingira ya academia. Ni ulimbukeni tu.

Robert Gates, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Director wa CIA, alikuwa anaitwa tu Secretary Gates, au Mr. Gates, ukiangalia press coverage hukuti akiitwa Dr. Gates.

Lakini ana Ph.D.
 
Itakuwa alijikita sana kwenye utafiti
 
Wenzetu wanachukulia, elimu uliyofikia haina umuhimu kwa jamii, bali ni ya kwako katika nyanja ya elimu.
Ila katika kujitambulisha ngazi ya elimu uliyofikia, ndio unaweza kujitambulisha niko ngazi ya u-dokta, u-profesa, u-digrii, u-masta n.k
Na si kulazimisha watu wakuite jina ambalo kwao halina msaada na halibadilishi chochote kwao.​
 
hamia marekekani gentleman, unababaika sana na wakati jambo rahisi tu 🐒
 
Duniani kote hakuna ila hapa Afrika tu - ULIMBUKENI TU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…