Nyami2010
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 227
- 50
WanaJamvi
Ninatangaza nia ya kugombea Ubunge kupitia CHADEMA 2015 katika Jimbo la Kyerwa-Kagera. Uwezo wa kuwa mbunge ninao na nia ninayo. Mbunge wetu wa sasa Mhe. Yustace Katagira, amekuwa mbunge tokea 1995 kwa tiketi ya CCM, japo 2000-2005 alipumzishwa na TLP, na akarejea tena 2005-2010 na 2010-2015. CCM kwetu haitusaidii hata kamwe. Mbunge wetu wetu ni mzee (70+), ni mfanya biashara wa kahawa(zao kuu la biashara jimboni kwake-imagine), na huwa haendi Bungeni(mtoro namba moja). Kyerwa nzima yenye wakazi takribani 400,000 haina shule hata moja ya A-level, haina hata Mita moja ya rami, maji ndo usiseme, haina hospitali, haina chuo chochote, hakuna hata nyumba moja yenye umeme, barabara ni tabu kuliko maelezo...ni shida tu. Ni Mzee ambae amekaa kimaslahi zaidi kuliko kuwatumikia wananchi.
Hivyo, wapendwa wanaJamvi nimeamua kwa dhati nijitose kupambana na Mzee huyu kigogo wa CCM ili CHADEMA ipeperushe bendera yake Kyerwa. Naombeni sala na dua zenu juu ya nia yangu ya kuwakomboa wananchi wetu.
Ninahitimisha:israel: