bado hujatueleza unasukumwa na nini kugombea ubunge ukijibu swali hili tutakuunga mkonop
Mliberali,
Asante sana kwa swali lako zuri. Ninasukumwa na haya yafuatayo:
1. Tulipata Uhuru katika kipindi kimoja na nchi za kusini mwa Asia ya mbali zikiwemo Malasia, Singapore, n.k, iweje leo leo nchi hizo ni middle income earners wakati sisi ni miongoni mwa nchi masikini sana duniani?
2. Huduma za jamii kama umeme, maji, afya, elimu bora, bima, n.k ni haba sana miongoni mwetu. Iweje ziwe ni kwa baadhi ya watanzania wachache tena viongozi na wafanyakazi wa serikali ngazi za juu na familia zao? Asilimia kubwa ya wananchi tulio wengi hatupati huduma hizi
3. Tazama CCM na mfumo wake, hivi kweli katika hali hii tutafika? Eti Bunge lisionyeshwe live kulikoni? Hivi unadhani Mhe. Makinda na Job Ndugai wanalitendea haki taifa hili?
4. Tunahitaji team ya vijana pale mjengoni Dodoma, hata ikibidi zipigwe kwa kutetea hoja zenye maslahi ya taifa....
5. Hivi Tanzania tuna mfumo wa Elimu kweli? Au ni uozo tu na uhuni na ujanja wawachache bora liende kwa CCM ilopo madarakani?
6. Ni mabilioni mangapi yako mikononi mwa wevi wachache huko Uswiss, n.k? Tunafanyaje hayo Mabilioni yarudi ili yawekezwe kwenye elimu, afya, maji n.k hapa nchini?
Mkuu ninayo mengi na wewe ninajua unayo mengi ila tukiunganisha nguvu bila unafiki TUNAWEZA! Japan in 1950s walikuwa kama tulivyo sasa ila waliamua na WAMEWEZA kulikoni sisi? Watanzania tuamue kuitoa CCM madarakani na hakika tutaweza!