Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ee namba unayopata unaifanyaje, je na ikiwa ni namba kubwa said ya idadi ya nyota unaifanyaje labda ukapata 14 au 25Umezaliwa 17-05-1978
1+7+0+5+1+9+7+8=?
Nyota ya Kwanza niUnatumiaje tarehe mwaka na mwezi uliozaliwa ,utajuaje
Nyota ya Kwanza ni
NYOTA YA PUNDA AU KONDOO (ARIES)
Hii ni nyota ya kwanza katika mlolongo wa nyota 12.
Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21st March na Mpaka tarehe 19 April ya mwaka wowote.
Sayari yao ni Mars (Mariikh)
Siku yao ya bahati ni Jumanne
Namba yao ya bahati ni 9
Rangi yao ya Bahati ni Nyekundu.
Asili yao ni Moto.
Nyota ya Pili
NYOTA YA NG'OMBE
(TAURUS)
Hii ni nyota ya pili katika mlolongo wa nyota 12.
Wenye nyota hii ni wale ambao wamezaliwa kati ya tarehe 21 April na Mpaka May 20 ya mwaka wowote.
Sayari yao ni Venus (Zuhura).
Siku yao ya bahati ni Ijumaa.
Namba yao ya bahati ni 6.
Rangi yao ya bahati ni kijani.
Asili ya nyota yao ni Udongo.
Nyota ya Tatu
NYOTA YA MAPACHA (GEMINI)
Hii ni nyota ya tatu katika mlolongo wa nyota 12.
Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21 Mei na Mpaka 20 Juni ya mwaka wowote.
Sayari yao ni Mercury (Attarid).
Siku yao ya bahati ni Jumatano.
Namba yao ya bahati ni 5.
Rangi yao ya bahati ni njano na bluu isiyoiva.
Asili ya nyota yao ni upepo.
Nyota ya nne
NYOTA YA KAA (CANCER)
Hii ni nyota ya nne katika mlolongo wa nyota 12.
Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21 Juni na Mpaka tarehe 20 July ya mwaka wowote.
Sayari yao ni mwezi (moon).
Siku yao ya bahati ni Jumatatu.
Namba yao ya bahati ni 2 na 7.
Rangi yao ya bahati ni Nyeupe.
Asili ya nyota yao ni Maji.
Nyota ya Tano ni:
NYOTA YA SIMBA (LEO)
Hii ni nyota ya tano katika mlolongo wa nyota kumi na mbili.
Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21Julai na mpaka 21 Agosti.
Sayari yao ni Jua (Sun).
Siku yao ya bahati ni Jumapili.
Namba yao ya bahati ni 1 na 4.
Rangi yao ya bahati ni Njano au rangi ya Dhahabu.
Asili ya nyota yao ni moto.
Nyota Sita ni:
NYOTA YA MASHUKE (VIRGO)
Hii ni nyota ya sita kwenye mlolongo wa nyota 12.
Wenye nyota hii ni wale wote ambao wamezaliwa kati ya tarehe 23 Agosti na Mpaka 22 Septemba ya mwaka wowote.
Siku yao ya bahati ni Jumatano.
Namba yao ya bahati ni 5.
Rangi zao ya bahati ni Njano na Bluu isiyoiva.
Asili yao ni Udongo.
NYOTA YA SABA::
NYOTA YA MIZANI (LIBRA)
Hii ni nyota ya saba katika mlolongo wa nyota 12
Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 23 September na mpaka 22 Oktoba ya mwaka wowote.
Sayari yao ni VENUS (ZUHURA).
Siku yao ya Bahati ni Ijumaa.
Namba ya Bahati ni 6.
Rangi ya Bahati ni Kijani isiyoiva.
Asili ya nyota hii ni Hewa.
NYOTA YA NANE:::
NYOTA YA NG'E (SCORPIO)
Hii ni nyota ya 8 katika mlolongo wa nyota 12.
Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 23 October na mpaka 21 Novemba ya mwaka wowote.
Sayari yao ni MARS (MARIIKH).
Siku yao ya Bahati ni Jumanne.
Namba yao ya bahati ni 9.
Rangi ya bahati ni Nyekundu isiyoiva au Maroon.
Asili yao ni MAJI.
NYOTA YA TISA:::
NYOTA YA MSHALE (SAGITTARIUS)
Hii ni nyota ya tisa katika mlolongo wa nyota 12.
Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 22 November na mpaka 21 December ya mwaka wowote.
Sayari yao ni Jupiter (Mushtary).
Siku yao ya Bahati ni Alhamisi.
Namba yao ya Bahati ni 3.
Rangi yao ya Bahati ni Hudhurungi.
Asili yao ni MOTO.
NYOTA YA KUMI:::::
NYOTA YA MBUZI (CAPRICON)
Hii ni nyota ya kumi katika mlolongo wa nyota 12.
Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 22 Dec na 19 Jan ya mwaka wowote.
Sayari yao ni SATURN (ZOHAL)
Siku yao ya bahati ni Jumamosi.
Namba yao ya bahati ni 8.
Rangi yao ya bahati ni rangi ya Kijivu au Nyeusi.
Asili yao ni Udongo.
NYOTA YA KUMI NA MOJA:::
NYOTA YA NDOO (AQUARIUS)
Hii ni nyota ya kumi na moja katika mlolongo wa nyota 12.
Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 20 January na 18 February.
Sayari yao ni SATURN (ZOHAL).
Siku yao ya bahati ni Jumamosi.
Namba yao ya bahati ni 8.
Rangi yake ya bahati ni Nyeusi.
Asili ya nyota hii ni Hewa.
NYOTA YA KUMI NA MBILI:::
NYOTA YA SAMAKI (PISCES)
Hii ni nyota ya 12 katika mlolongo wa nyota 12
Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 19 February na mpaka tarehe 20 Machi.
Sayari yao ni JUPITER (MUSHTARA)
Siku yao ya Bahati ni Alhamisi.
Namba yao ya Bahati ni 8.
Rangi yao ya Bahati ni Zambarau au Kahawia iliyochangamka.
Asili ya nyota yao ni Maji.
Tosheka na hayo maelezo yangu kwa leo.
Kama hujuwi tarehe yako ya kuzaliwa na mwezi pia haujuwi basi tumia jina lako na jina la mama kama nilivyo weka hiyo video ufanye hesabu wee mwenyewe.Mkuu kunasehemu umesema MTU anweza tumia jina LA kwake na LA mama take, he hapo tunatumia majina kamili yani langu na LA baba angu na mama angu na baba ake ama ? ikibiditoa mfano ili nielewe zaidi
UmezaliwaTarehe 17-05-1978 nyota yako ni nyota ya N'gombe aka Taurus unatizama nyota ya N'gombe Aka Taurus.Umezaliwa 17-05-1978
1+7+0+5+1+9+7+8=?
Nashukuru mkuu,sema niliomba utoe mfano kidogo ili nielewe zaidiKama hujuwi tarehe yako ya kuzaliwa na mwezi pia haujuwi basi tumia jina lako na jina la mama kama nilivyo weka hiyo video ufanye hesabu wee mwenyewe.
Njia za kujuwa nyota yako Njia ya kwanza ni jina lako herufi yako ya mwanzo ndipo utajuwa nyota yako kwa kutumia herufi ya mwanzo wa jina lako. Njia ya pili ya Kwa Kujuwa nyota yako unachukuwa Tarehe yako ya kuzaliwa na mwezi uliozaliwa ndipo utakapoweza kujuwa nyota yako ni ipi? Na Njia ya 3 Njia ya mwisho kujuwa nyota yako kwa kuchukuwa jina lako na jina la mama yako kwa idadi ya herufi za Abjadi unajumlisha herufi za jina lako na jina la mama yako.Kisha una gawa kwa 12%12 itakayobaki ndio itakuwani nyota yako. Kwa Mfano imebaki namba 1: nyota yako ni nyota punda ikibaki namba 2: nyota yako ni nyota ng'ombe ikibaki namba 3: nyota yako ni nyota ya mapacha. Ikibaki namba 4: nyota yako ni nyota ya kaa. Ikibaki namba 5: nyota yako ni nyota ya Simba.Ikibaki namba 6: nyota yako ni nyota ya mashuke ikibaki namba 7: nyota yako ni nyota ya mizani ikibaki namba 8: nyota yako ni nyota ya nge. Ikibaki namba 9: nyota yako ni nyota ya Mshale .Ikibaki namba 10: nyota yako ni nyota mbuzi. Ikibaki namba 11: nyota yako ni nyota ndoo. Na ikibaki namba 12: nyota yako ni nyota ya Samaki. Jifunze kusoma Herufi za Abdjadi kwa kuangalia Video hapo chini.Nashukuru mkuu,sema niliomba utoe mfano kidogo ili nielewe zaidi
Uchawi upo au haupoSiku zote mambo yaliyo juu ya ukawaida wa mazingira na mazingara ya binadamu imma yawe ya kweli au yawe ya kusadikika yanastajaabisha na yanavutia kwa wakati mmoja na ndicho kilichokuwa kwa huyo Mzee.
Yule mzee hakuwa na elimu ya astronomy hii ambayo ya kuchunguza maumbile asili ya anga na kutambua mienendo ya juu bali alikuwa na elimu ya unajimu (astrology).
Elimu hii ni elimu inayotaka kuhusiana au kuendana na elimu ya astronomy ila utofauti wake ni kuwa astrology inaelezea sana mwenendo wa viumbe hai kwa ujumla na inahusisha viumbe hai na anga. Ila elimu ya astronomy inaelezea elimu ya anga peke yake.
wanajimu wanaamini elimu ya anga ambayo ni nyota, sayari na mwezi zina uhusiano wa kitabia, kiasili, kimaumbile, kimaisha, kimali, kimaradhi, kitiba na kifo na kimajira ya sayari ya dunia na vilivyomo. Wanajimu wanaamini Mungu aliumba vitu na viumbe kimahesabu, mahesabu hayo yanakani inayoingiliana na mwenendo wa maisha ya viumbe hai alivyoviumba Mungu.
Kwa kuwa vilivyomo angani na magimba na sayari zilizokusanya na nyota kwa kuwa zinakwenda kimahesabu maalumu: Kwa hayo wanajimu wanaamini Mungu aliumba asili 4. Asili ya vilivyo na moto, udongo, upepo na maji. Wao wanaamini asili hizi nne(4) ziliweza kuzaa asili saba (7) na matawi yake mawili (2) ambayo Mungu aliumba mbingu saba (7), ardhi saba(7) kwa tabaka, bahari saba (7), mabara saba (7), sayari kubwa zipo saba(7): kwa hayo wanajimu wanaaamini vitu hivyo saba vinatokana na asili hizo nne.
Kwa hayo mahesabu wanaamini kwa dhati kabisa ya kwamba; Bahati, raha, shida, mafanikio, maradhi, kifo na maisha yote kwa ujumla yanayomwangukia binadamu qadar/dira/uongofu wake yanahusiana kwa dhati kabisa na mzunguko wa nyota, sayari na mwezi.
Wanajimu wanachokifanya ni ramli! Ni udanganyifu, ni utapeli. Hata huyo marehemu alishindwa kutabiri kifo chake, walau hata mahali atakapofia au siku pengine. Hayo yote alishindwa. Hiyo elimu inafika mbali kabisa inajihusisha na ushirikina. Kwa sababu marehemu miaka ya nyuma kabisa huko kabla ya kujikita rasmi kwenye hiyo elimu alikamatwa akiwa pamoja na mwalimu wake aliyemfundisha huo unajimu.
Mwalimu wake alimuaga anaondoka kwa kujigeuza umbile kuwa chura na kutoka ndani ya selo.
ndo walewale hebu tuambie hyo njia ukiifanya unafka hyo sayari? kama sio ushirikina ni ninKuna Sayari inaitwa "Alama simsima." Haihusiani na masuala ya mahesabu ya kiunajimu.
Allah subhanahu wataala baada ya kumuumba Adam A.S kutokana na udongo huo huo akaumba mtende. Kwa udongo huo huo uliobaki akaumba "Alama simsima".
Hii ni sayari! "Akrimuu ammatakumunakhla" Mtume S.A.W aliuita mtende kwa kuupa sifa ya ndugu wa binadamu. Hii sayari ni kubwa! Kuna watu wanaishi kama mimi na wewe na kuna njia ukiifanya unafika na kuingia kwenye sayari. Kuna Malaika pia