Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Mimi me 30/10
Yeye ke 1/1
Wewe ni Maji ya moto na yeye ni mchanga wa pwani;
Hisia zako zote kali na zenye nguvu hukaribishwa na kutulizwa hapa. Wewe ni maarufu kwa kuwa mtata sana kwenye mapenzi unagubu ambalo si rahisi kuonekana wazi lakini kadri unavyozidi kuwa na huyu mwenzio ndivyo atakavyozidi kukutuliza kwa maana ana asili ya utaratibu na kumezea mambo mengi na vile vile yeye ni mtu mzazi sana vile vile matukio yake ya kusisimua hukufanya kuwa ni mwenye kuvutiwa nae zaidi na kufanya uhusiano wenu uwe na huba ndani yake kwa maana yeye pia huvutiwa na hupenda tabia yako ya kumuonea wivu japo anaweza kukuthibitishia hilo au kisiri ambalo hili humfanya ajihisi yupo kwenye mahusiano ya kueleweka na kujihisi analindiwa mapenzi yake.
Nyote wawili mnahusiana vizuri na mnaonekana ni wenye kuwa na mtizamo mmoja linapokuja suala la kimtizamo.
kwa maana nyinyi ni wenye tamaa moja, nia moja na mtizamo mmoja mnapoingia kindoa na kuwajibika pamoja kila mtu kwa nafasi aliyopo mna nafasi kubwa ya kufanikiwa kindoa kuliko uhawara hata mafanikio ya kiuchumi kubwa tu mnatakiwa kushirikishana na kuwa wawazi kila mtu kwa mwenzio ukifanya kitu usimfiche vile vile na yeye.

Rakims
 
Mimi me 12/2 jina S
Yeye ke 18/12 jina T
 
Mkuu Rakims;

Mimi ni mwanaume, jina langu linaanzia na herufi N, nimezaliwa tarehe 22/12.

Huyu ni mwanamke natarajia kumuoa, jina lake linaanzia na herufi W, amezaliwa tarehe 29/11.

Aminia sana mkuu!..
 
Anza na baba na mama yako. Acha ukumbaff hapa. Utakuta wewe unaishi kwenye mahusiano mabovu ambayo ni moto. Onyesha busara na ujuzi badala ya ujinga na ukumbaff mwanangu
 
Mkuu Rakims;

Mimi ni mwanaume, jina langu linaanzia na herufi N, nimezaliwa tarehe 22/12.

Huyu ni mwanamke natarajia kumuoa, jina lake linaanzia na herufi W, amezaliwa tarehe 29/11.

Aminia sana mkuu!..
Unapendelea sana kufanya kinyume na maumbile lakini pia huna hela kenge wewe
 
Mimi me 12/2 jina S
Yeye ke 18/12 jina T
Wewe una Asili ya Upepo wa kimbunga hali ya kuwa yeye ana asili ya moto wa nyasi nyote wawili mpo vizuri kitabia za nyiota hasa ukizingatia kuwa nyota yako ni thabiti na yake ni yenye nyuso mbili yaani baina ya Mutable na fixed hii hupelekea mtizamo wenu kinyota kuwa mzuri Nyie wawili mnaendana sana katika mahusiano kiasi kwamba hata likija suala la kufanya mapenzi basi kila mtu anatarajia maandalizi makubwa kutoka kwa mwenzie kuanzia usafi na utendaji mnapofika chumbani watu wangekuwa wanawaona basi wasingesita kulipia ili kuwaona mkifanya tena na tena.
Kila mmoja kati yenu anamvutia mwenzie kiakili na mko radhi kuendana kiroho bila nyinyi kuzungumza lakini roho zenu zinakuwa zina makubaliano teyari.
Hasa ukizingatia ya kwamba wewe una mawazo ya mbali sana na ya uvumbuzi ukija kwake ni Mwenye matumaini na maono vile vile mafanikio kwenu ni rahisi sana labda kama ataingilia mtu katikati hasa pia tukirejea katika herufi ya jina lako inatawala nyota ya Samaki na ya kwake inatawala Kaa basi hapo hata negative energies zenu zipo sawa kwa maana zote zinatabia ya maji hivyo hata ugomvi ukitokea kwenu ni mwepesi sana kuzimwa na kuendeleza maelewano
Ingawa maono yako mara nyingi yanakuwa na ukweli usiopingika, hiyo haimkwazi yeye ambaye muda mwingine anaonekana mbishi kiasi kwa utundu tu na baadae anaelewa.
Nyote wawili ni watu wa watu na wenye kupendwa na watu wanaowazunguka, nyote mnapenda kutembelea maeneo mapya na mko teyari kufanya lolote lisilotabirika katika mapenzi yenu ili tu kuyakomaza japo kuwa inaweza kuwa ngumu kuelewana mwanzoni mwa mahusiano.
Kipande kizuri kuhusu nyie ni either mmoja kati yenu huwa na wivu pale ambapo mwingine anakuwa hayupo nyumbani.

Rakims
 
Anza na baba na mama yako. Acha ukumbaff hapa. Utakuta wewe unaishi kwenye mahusiano mabovu ambayo ni moto. Onyesha busara na ujuzi badala ya ujinga na ukumbaff mwanangu
Neno unakuta ni Dhana, Mkuu ikiwa nimekukwaza kuweka post hii niwie radhi lakini mlengwa ulikuwa sio wewe vile vile Jamii forum is WHERE WE DARE TO TALK OPENLY hivyo kama unakwazika na ninachokiandika pimwa kwanza akili,
*Vile vile Baba na mama wanafika vipi hapa?
Unapozungumzia busara elewa na kumbuka
"Sifa za mtu duni haonyi vitendo vyake hata umtie chupani atatoa kidole chake" ingawa unaigiza jina la hapa Jamii forum lakini ukweli wako utabaki kuwa wako tu, lisikuhadae jina la kutumia mtandaoni ukahisi Dunia haina Karma sijakudhuru kwa lolote hivyo kuna kitu nimeongea hapa kitakuja kukutesa sana baadae kiakili ukikaa ukatulia kumbuka MWANANGU as how you call me, neno likishatamkwa halirudi tena kinywani vile vile mzazi wa mwenzio ni wako tu ukisema baya kwa mzazi wa mwenzio ndivyo ulivyosema baya kwa mzazi wako.
Jitizame ulivyomjinga kiasi gani makala ya kuandika tu mtandaoni inakuumiza roho kiasi kwamba unatamani hata ningekuwa karibu ungenipiga kibao. Tafuta sehemu nzuri ya maombi ujiombee Mungu akuongoze ukae sawa mdogo wangu yasikuharibu akili maisha ya Duniani.
Nyie wenye username zaidi ya moja mnajidanganya sana na ulimwengu wa sasa.

Rakims
 
Waulize wagagnga wenzio.
Mnaoshirikiana kuharibu maisha ya watu.
Sawa mkuu nimekuelewa. mimi unaona naharibu ndio maana upo wewe unaetengeza maisha ya watu, vile vile hizi thread kama hazikufai rejea kwenye zile unazopenda kuchangia za ushoga pamoja na huyu mwenzio kule ambapo kutukana mama zenu ni bora zaidi kuliko kufuata nyota ambazo zimeumbwa ili kuwa muongozo wa kuwatoa watu kwenye kiza cha bara na baharini.

Rakims
 
Mimi mme 14/12
Yeye mke 24/02
Baina ya nyie wawili wewe ni Moto wa nyasi na yeye ni Maji ya kisima kwa maana hii yeye atavutiwa zaidi kwako kulingana na nguvu yako ya utafutaji wa maisha, na vile vile wewe utavutiwa nae zaidi kwa mtizamo wake wa kiimani na mambo ya kiroho.

Ukweli ni kwamba katika mahusiano wewe unahitaji mwenza ambaye ni kama mshkaji na yeye anahitaji mwenza ambaye ni kama mwenye ndoto za mapenzi yaani mapenzi muda wote mfano mwanaume wa ndoto zake nyote wawili hamuendani kwa maana kati yenu hakuna anaeweza kumsaidia mwenzie katika mahitaji yake

Asili yako ya roho ya uthubutu na kujitoa utakuta inakwamishwa sana na yeye ambaye ni tegemezi zaidi kwako na uoga wake pia

Yeye ambaye huwa na hisia kali sana muda wote hata kuona unamapenzi nae zaidi ya kumtaka akutimizie haja zako kingono tu, vile vile atakuona ni mtu ambaye hujatulia mambo mengi na vile ulivyo ni mtu wa kupenda uhuru basi moja kwa moja utajiwekea akilini kuwa huyu ni wa kuwa nae tu kwa muda kisha utatafuta mwingine lakini mahusiano yenu taratibu huanza kuzama mfano umemwaga maji kwenye mchanga kila mtu ataangalia uelekeo wake. ndio ndoa hizi mara nyingi watu wanakuwa pamoja ajili ya kuangalia matumizi na watoto tu lakini ni ndoana.

Rakims
 
Me 20/4/ erufi A
Ke 29/6/ erufi H
Nyote wawili mna mengi mnayoendana.

Wote ni wenye kupenda maisha ya nyumbani, wapenda hisia, na hasa kwenye kufanya mapenzi.

Wewe ni mwenye kupenda kwenda pole pole na na vile vile kupenda vitu asilia ambapo ni mvuto mkubwa kwake katika ugonjwa wake wa kuwa na mood zenye kubadirika badirika, ingawa muda mwingine kupenda kwake kuongea kwa uwazi kunakutaka wewe kuwa makini sana kutokumharibu hisia zake kwa maana ni mtu yupo kihisia zaidi na ukimuingia ndani zaidi utaona ni mtu wa kupenda kulia, yeye anataka mtu ambaye ni mwenye nguvu mwenye nyota yako kwa ajili ya kumtegemea kwa kila jambo, baadae utaona ukimtimizia atakupa uaminifu mkubwa wa mapenzi na kukwambia kila siri yake hata wanaomtaka atakuorodheshea, wewe ni mwenye kubana uchumi na kutunza vema na yeye pia ni mtu mwenye kupenda kujibana na kutunza akiba hivyo nyote wawili mna lengo moja au malengo sawa.

Masilahi yenu pamoja na matamanio yenu sawa basi huleta uhusiano mzuri wenye baraka, ukimuoa huyu hujapoteza.

Rakims
 
Mimi: 14 Feb
Wife: 04 Feb
Baina ya wawili nyie ni sawa na kidole na pete

Nyote mnakuwa ni wenye kutamaniana yaani kila mmoja ana tamaa na mwenzie, na hasa katika kufurahia ucheshi wa kila mtu na mwenzie

Uvumbuzi, maendeleo, kuvutiwa upya kusiko na kifani kwa kila mmoja kati yenu ni jambo la kawaida sana na vile vile mnafaana katika tendo na wenye kushirikiana kwa maslahi mapana

Nyote wawili kila mmoja wenu anajihusisha na yote kwa mwenzie na katika shughuli zote na urafiki pia na kushirikishana kama ni wacheza kamari basi mngecheza pamoja pia kulingana na mnavyoendana.

Mambo mengi ya kujishughulisha kwa nje mnaweza kuwa mbali katika kufanya mambo yenu lakini hilo sio tatizo kwenu. hamna kitu ambacho mnachobishana sana zaidi mwisho wake ni kukubaliana nyote mpo kibusara zaidi kuliko kihisia. mapenzi yenu hayatakuwa mazito sana lakini yatakuwa ni yakuvutia yaani hampo deep sana lakini mtu vema.

Rakims
 
Wengine username si rahisi kujua nani mwanamke nani mwanaume fafanua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…