Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Mkuu mbona wengine unaturuka
Mie Me jina E tarehe 12 August
Yeye Ke jina I tarehe 12 January
Ni wapenzi
Hapo sasa sawa,
Kwa mtizamo mnaonekana wewe ni moto wa mkaa na yeye ni mchanga wa pwani hivyo kwa mtizamo huu tu kuendana kwenu ni mtihani na itafikia sehemu kila mmoja ataangalia pengine kwa maana kinachowabeba ni maongezi tu yaani mnaongea vizuri lakini kwa kuendana ni asilimia 20 tu.
Hivyo wewe mapenzi yako yanaonekana ni ya hali ya juu yaani ni mtu mwenye kutapa mapenzi ya gharama na kujitanua ambapo yeye utakuta ni mtu wa kujibana bana na tahadhari na atakuwa anakunyima uhuru mwingine. unakuwa wewe ni mtu huru lakini yeye anataka kujibana na kukuambukiza kujibana na kujinyima kitu ambacho kwa asili zote za moto huwa zinapingana nacho.
Nyote wawili mnakuwa na mvuto kingono lakini mkiwa na tofauti za kimsingi.
Wewe unakuta ni mtu mwenye kusambasa upendo lakini yeye anakuwa hataki na pia hata katika tendo unaweza kukuta unajinsi unavyotaka na yeye hataki itafikia sehemu utaanza kumfikiria ni mchoyo wa mapenzi labda ukifanya kitu atabadirika lakini usijidanganye. Yeye ni bahiri wa mapenzi kuyatoa na kugawa kwako vile unavyotaka.
Asili yako kwenye mapenzi ni mtu wa kutaka kutukuzwa na kusifiwa kwa huyu ni mtihani kwako na hakuna kati yenu atakae kuja kukubali kuwa chini labda tu ni maigizo ya awali kisha baadae atageuka tu.
Mahusiano yenu mtatia nanga kabla hata ya meli kuanza safari.

SEHEMU ZAKE ZA HISIA;

Hisia zake zipo miguuni pamoja na hisia zake za kimapenzi na wewe hisia zako zipo moyoni na kwenye kifua chako sasa hapa utaumia tu.
 
Hii inakuwa sio thread yake mkuu.
Mkuu naomba unijibu, nimeongeza details tayari

Mimi ni Me jina linaanza na A na tarehe ya kuzaliwa ni 28/8

Mpenzi (Ke), jina linaanza na M tarehe ya kuzaliwa ni 22/7,

Tumezidiana miaka miwili, mimi Me ni mkubwa kwake

Ni wachumba
 
Mkuu Mimi naona unaniruka na naandika mara ya 4 sasa

Mimi ni me 26/06 herufi E
Yeye ni je 04/04 herefi L
Kama ulikuwa unatafuta mahusiano au ndoa basi kwa huyu unakuwa umepata kwa maana mnaendana kwa asilimia 95 na pia mnaendana kwa nafasi kubwa sana kama mnamahusiano tu kama ulivyosema basi muombe akuoe hata kesho kwa maana hapo hujakosea na upo sahihi sana pia wewe maji ya bahari na yeye ni mchanga hivyo kila mtu hufurahi na hupenda kuona bahari jinsi ilivyo mnaendana sana huyu anakubeba kwa asilimia kubwa na wewe unamtakasa kwa asilimia kubwa na watu wakiwatizama pamoja mnakuwa hamchoshi

kwa mtizamo mnaonekana nyote wawili mnahitaji ulinzi na mahusiano ya moja kwa moja na nyote mnapendana na mmeridhiana na wenye shauku. ukimtizama yeye mara nyingi akikuona tu mihemko yake ya sex huamka na yeye ni mtu mwenye mapenzi kama ya kujidekeza kwa mahaba kwako.
Nyote ni watafutaji na wenye nafsi za kutafuta pesa na mafanikio yenu na pamoja mnaonekana ni wenye kupenda mazingira ya nyumbani na afya zenu na kujaliana.
Yeye ni mtu mwenye kupenda kuhudumiwa na kuonyeshwa upendo na wewe. na kila muda huonana wapya au kama mnaanza upya na yoyote kati yenu akitaka jambo basi mwingine anakuwa ana support.

SEHEMU ZA HISIA:
Sehemu yake ya hisia ni shingoni nimeshaelezea ufanye nini kama mwenza wako anahisia sehemu hii

Rakims
 
Hawezi kuja huyo, lengo lake sio kutoa msaada humu bali ni kiwapiga pesa. Na ndio maana katoa maelezo mengi halafu kaweka na namba za simu ili wakuingia kingi aingie kwa kumtafuta kwenye simu. Angekuwa mtoa huduma angewajibu watu humu ila ni mtumia fursa huyo
Unachoandika huna tofauti na mtu anaeandika bila fikra unaropoka kwa kuwa wewe huna kazi ya kufanya sio wote kwa maana ungekuwa na kazi ya kufanya ungefikiria mara mbili kabla ya kuquote pumba hakuna mtu anaefanya kazi au anaeanzisha biashara ili agawe sadaka acha kufikiria kama vile una ubongo wa funza huna unachojua zaidi ya matope.
Yaani mimi sina kazi zingine za kufanya time yote niwe online?
Usiwe kizazi cha jorowe kijana ubongo wako usiishie kwenye mipira tu una mengi ya kuutumia kung'amua mambo.
Bado ungekuwa mstaarabu ungemshauri asubiri au wewe usubiri uone nini kinatokea. Ningekublock lakini naona ipo siku nitapost elimu itakusaidia acha nikuache uendelee kuongea pumba.

Rakims
 
Rakims mimi ni mwanaume jina linaanza na S na nimezaliwa tarehe 17 july 1984 na wife jina linaanzia herufi A amezaliwa tarehe 21 October 1987. Nahitaji uchambuzi wako mkuu.
Kwa mtizamo ni kuwa wewe una asili ya maji ya bahari na yeye ana asili ya maji moto hii inawaweka kuwa ni watu wenye kuendana vema kwani wewe humpandisha hisia na kumjaza hisia za upendo kwa maana yeye ni mtu wa nguvu na shauku nyingi na hii ni kwa sababu wewe unakuwa na sifa kuu ya uaminifu na ni mwepesi kuaminika, hiyo hupelekea kwa yeye mwenye asili ya wivu kuliko asili zingine 12 kuwa mwenye utulivu na kujihisi kwako kafika.
Unaonekana ni mtu mwenye kupenda pia ushupavu wake na yeye anakuwa ni mwenye kuamini kabisa kwamba wewe ukiamua au kuridhia jambo basi inakuwa ni mtu mwenye msimamo nyote wawili mnaonekana ni wenye hisia sana ambazo zinaweza kumkidhi mwingine.
Pamoja ni wenye uwezo mkubwa wa kujenga mahusiano yenu hadi watu wengine pembeni wakawa wanawaonea wivu mnaendana sana
Uhusiano huu una urafiki mkubwa,mtamu, na wenye kina kirefu.
Mambo yanakuwa mazuri tu kikubwa muda.

SEHEMU ZA HISIA;
Huyu sehemu zake za hisia ni sehemu za siri kama utajua jinsi ya kucheza nazo vizuri basi utamteka hadi kuzikana. Unaniwia radhi napata ugumu kuandika maelezo mengi ningekuelekeza jinsi ya kucheza nae pia swaum 😉

Rakims
 
KWA WALE AMBAO MNAWEKA DETAILS NUSU NIMECHOKA KUWAELEWESHA UKIONA SIJAJIBU JUA DETAILS HAZIJATOSHA
 
Nitarudi...................................................!
 
Nitarudi...................................................!
Mkuu ukirudi naomba uanze na mimi

Mimi ni Me jina linaanza na A na tarehe ya kuzaliwa ni 28/8

Mpenzi (Ke), jina linaanza na M tarehe ya kuzaliwa ni 22/7,

Tumezidiana miaka miwili, mimi Me ni mkubwa kwake

Ni wachumba
 
Mimi ni mwanaume
ME ,herufi ni Z tarehe 27/January
KE,herufi ni A tarehe 13/April
 
Back
Top Bottom