Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Binafsi watu kama wewe huwa nawapa pole hapa hapa online kwa maana wanaandika kitu wasichokijua na baadae kinakuja kuwadhuru wao wenyewe;

Hivyo pole sana na mwenyezi Mungu atakuongoza
Sijakusoma,unasema🤔.Au wewe ndio mwenye kilinge chako unakitangaza humu jf,🤔. Halafu ajabu na kweli unaweza kuwa umeweka tangazo la biashara kinyume na taratibu,au ukilipia gharama za tangazo la biashara,,🤔
 
Utangamano;

Mahusiano yenu hapa huwa ni sawa na Mfalme na Malkia wanapokutana,
Vichwa hugeuka kwa maana wawili nyie wote ni Simba na mahusiano haya ni sawa na simba dume na simba jike. Wawili nyie hapa ni wenye kuwa na uaminifu mkubwa sana,
Mahusiano haya pande zote mbili huwa ni zenye shauku kubwa sana katika mizani wa kila mmoja kwa mwenzie. Wote wawili nyie ni wenye mapenzi makubwa na mko romantic sana.
Kila mmoja kwa mwenzie, wenye rangi za kupendeza na furaha kubwa katika maisha yenu ya sasa na ya baadae na wenye uwezo mkubwa sana wa kufikishana kileleni.

Swali kubwa la kujiuliza hapa ni; Nani kati yenu atakae kuwa mtawala?
Ni ngumu sana kwa Simba mmoja kumuachia nafasi mwengine kutawala na kujiona muhimu na kujistahi kuliko mwingine.
Lakini hilo ndio kubwa linalohitajika zaidi kwenye mahusiano haya.
Kila mmoja wenu hata taka tu kukaa kwenye kitu ya ufalme huu isipokuwa kila mmoja atataka aonyeshe mabavu yake pia.
Kwa ushindani wa kuridhishana kitandani nani atakae mridhisha mwenzie, Nani atakae muhudumia vizuri mwenzie, nani atakae mpa zawadi mwenzie, nani atakae pendeza zaidi ya mwenzie, nani atakaejali zaidi wazazi wa mwenzie, nani atakae mbembeleza zaidi mwenzie.
Yaani ni ushindani wa mahaba makubwa na heshima kubwa hakuna mfano na umejaa hisia kali na kila mtu atakae waona atataka kuwaiga.
Wawili nyie ni sawa na mkaa unaopika chakula ukaongezewa mkaa mwingine, wawili nyie ni sawa na jua moja likaongezewa lingine yaani nyie ni watu mnaendana kuliko kawaida unless mmoja wenu awe kadanganya details;

Binafsi nayapenda mahusiano baina ya Simba na Simba maana wakiungana wanakuwa ni kivutio cha utalii na pia ni nyota pekee katika unajimu zinazoendana sana kuliko zingine kwa maana wote mnatawaliwa na sayari ya jua na hakuna anaeendana na mwingine isipokuwa jua mwenzie ni jua, simba mwenzie ni simba na vile vile mfalme mwenzie ni malkia.

Basi kama bado hamjafunga ndoa mnasubiri nini?

Nyie ni Grand lovers and interesting rivals (wapenzi wakuu na wapinzani wa kuvutia).

Rakims
Wow....

Nilikua nahofia zaidi hapo kwenye nyota, kumbe tunaweza endelea

Asante mkuu

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Negative kwa maana ipi wakati wanakuuliza kilinge chako? We majnun tena sakaran wa kutupwa. Sitaghafiru mara hata mia lakini wewe ni mujurumuun wa hali ya juu ibn muthinaq mkubwa
Pole sana na Mwenyezi Mungu akusamehe
 
Hufanyi bure unajenga mazingira na kutangaza upuuzi wako ili baadaye utafutwe na kuwaibia wajinga na washirikina wenzako. Wote huanza hivi. Kimsingi JF wanapaswa kukuban kwani unatumia jukwaa lao kutangaza upuuzi waka bila malipo.
Na ungekuwa umeanzisha hii network hakuna mtu angekaa member hata wiki mbili una roho ya kwanini mkuu. Mtoto wa kiume hutakiwi kuwa hivyo jiangalie kwenye kioo halafu jipige pige kifua sema hakika mimi ni mchawi.

Rakims
 
Sijakusoma,unasema🤔.Au wewe ndio mwenye kilinge chako unakitangaza humu jf,🤔. Halafu ajabu na kweli unaweza kuwa umeweka tangazo la biashara kinyume na taratibu,au ukilipia gharama za tangazo la biashara,,🤔
Karibu tena kwa kuchangia makala zijazo asante
 
Umenitaka nikakutaa sasa unanibadilisha jinsi wakati wewe ni sengeee tu la kawaida linalobabaisha maisha. Kama mie ni mtam... basi baba yako zaidi
Wacha niwa report maana mnanichafulia mada
 
Me 01/05
Ke 17/09
Details zako zikiwa fupi na maelezo yanakuwa mafupi.

Kwenu mapenzi huanza pale mnapoonana tu mara ya kwanza.

Nyote wawili ni wapenzi wa maisha ya nyumbani zaidi kuliko mitoko inapokuja kwenye mahusiano, na ni wenye kushare malengo aina moja na kutafuta mafanikio sawa yaani kwa akili moja, wewe ni mkakamavu na yeye ni mwenye akili ya haraka haraka wawili nyie mna combination nzuri ya team moja yenye mafanikio makubwa, na wewe ni mwenye kuweka umakini sana katika matumizi

kitu ambacho kinamvutia sana yeye, ingawa mnaonekana kuwa na asili tofauti za kuyaindea maisha au mitindo tofauti hakuna anaetaka kujiweka juu ya mwenzie. mnatakiwa kuongeza mvuto katika ufanyaji wa tendo la ndoa kwa maana kimahusiano huo ndio udhaifu wenu, kwa maana kwako tendo la ndoa ni kimwili zaidi na kwake ni hisia zaidi baadae utamuambukiza kuwa kimwili zaidi kwa maana hisia zake yeye mara nyingi huwa zimelala mengineyo mnaendana.
 
Jitizame ulivyo na roho mbaya Astaghfirullah yaani unashadadia Quotes ambazo zipo Negative zingine huoni? kweli wewe ni:
"Sum mum bukmum umyum fahum la yarjiun"
Vile vile "Indeed, it is not the sight that becomes blind but the heart that becomes blind'.
Una roho mbaya na nyeusi sana kwanini usiquote watu waliokubali ni kweli na kuwaambia mnadanganywa unaenda kumquote mfalme wako wa ujinga?

Rakims

Msaada
ME 30/05 P
KE 09/06 M
 
Me 4/12
Ke 29/7
Katika mahusiano yenu wewe unaonekana ni mwenye asili ya moto wa nyasi na yeye ni moto wa mkaa mnaendana vema kila mmoja kati yenu anamuona mwenzie anamfaa zaidi.

Kuna mambo mengi ya kusisimua yatakayo kuja kuwatokea kwenye mahusiano yenu, yeye mwenye kujiamini inatoa uhakika kabisa kwamba atafungua hisia zako zote za tamaa ulizonazo katika mapenzi, na mapenzi yenu ni ya maajabu sana, nyote mnafurahia kusafiri pamoja, kukutana na watu wapya, na kila mmoja kati yenu anafurahika kuwa karibu na mwenzie yeye ni mwenye kupenda uhuru sana ikiwa ni pamoja na wewe,

Hivyo katika mahusiano yenu kutakuwa hakuna matatizo ya wivu ikiwa ni pamoja na kutawaliana ni couple moja nzuri sana mkipatana.

Wewe una mwanga mzuri wa kuendana nae kimazungumzo na vile vile ni mwenye uwezo mkubwa wa kukabiliana na Gubu lake.

Hakuna maelezo mengi kuhusu mausiano yenu isipokuwa jambo kubwa moja ni kwamba nyie ni Grand mating.

Ukimpoteza huyo kumpata wa hivyo huwa kazi.

Rakims
 
Me 24/12 E
KE 01/03 I
Mahusiano haya ni baina ya mchanga wa pwani na maji ya kisima kuna visima pia vinakuwa na mchanga wa bahari au mweupe chini hivyo couple hii inawezekana.

Mtizamo:

Wewe ni mwnye uwezo wa kutoa na kumpa katika kila sector ambayo yeye anatamani katika mahusiano kuanzia kumtimizia na kumkamilishia yale yote anayotamani katika mapenzi au kutoka kwako na wala hilo kwako sio tatizo hata katika kumfikisha kwenye tendo kwako ni rahisi sana na yeye kufurahia zaidi na husikia raha pale tu unapoonyesha dalili za kumtaka kimwili hata kama kakasirika utaona anaanza kulegeza uzi,

Nae pia ni mwenye kukutamani na hakuna kitu wewe unapenda kama kutamaniwa na yule uliyenae kwenye mahusiano yaani akionyesha tu hata kukutizama kwa jicho la huba wewe hoi.

Kama ilivyo kwa nyota yako kuwa na kutambulika ni nyota ya watu wa serikalini au viongozi basi ndivyo ulivyokiongozi mzuri kwake ambaye yeye hata ikitokea kampoteza hujihisi kuchanganyikiwa na huona maisha yake yameharibika kama kapoteza mzazi, ndio maana wengine utakuta wanakuwa wagumu kuingia kwenye mahusiano kwa kuhofia siku ya kuachana. Lakini yeye anakuwa na nia ya dhati ya kukufuata kwa yale unayomuongoza.

Ingawaje mtasumbuka sana kwenye malezi ya watoto na matatizo ya uzazi lakini ikitokea hili limeenda sawa basi katika watu ambao watakao tamba kwamba oeni mpate kutulia na kufarijika wewe utakuwa ni mmoja wao.

Ladha yake ya ajabu katika mapenzi inaweza kukuathiri kisaikolojia pale mnapogombana ukaona mambo hayaendi ni vile utamu wake utakugusa sana rohoni kuliko kimwili. Mapenzi yake ukarimu na hisia zako kali za uaminifu vinachanganyika na kufanya kila mmoja ajisikie yuko salama na analindwa katika mapenzi na mwenza wake.

Hakika nyinyi ni watu wawili tofauti ambao mtakuwa mmekutana na mwenza sahihi kwa maana kila mmoja atakuwa ni mwenye kuvutika na kujiona kapata kwa mwenzie mtu sahihi.

Rakims
 
Me 22/08-I
Ke 17/08--C
Utangamano;

Mahusiano yenu hapa huwa ni sawa na Mfalme na Malkia wanapokutana,
Vichwa hugeuka kwa maana wawili nyie wote ni Simba na mahusiano haya ni sawa na simba dume na simba jike. Wawili nyie hapa ni wenye kuwa na uaminifu mkubwa sana,
Mahusiano haya pande zote mbili huwa ni zenye shauku kubwa sana katika mizani wa kila mmoja kwa mwenzie. Wote wawili nyie ni wenye mapenzi makubwa na mko romantic sana.
Kila mmoja kwa mwenzie, wenye rangi za kupendeza na furaha kubwa katika maisha yenu ya sasa na ya baadae na wenye uwezo mkubwa sana wa kufikishana kileleni.

Swali kubwa la kujiuliza hapa ni; Nani kati yenu atakae kuwa mtawala?
Ni ngumu sana kwa Simba mmoja kumuachia nafasi mwengine kutawala na kujiona muhimu na kujistahi kuliko mwingine.
Lakini hilo ndio kubwa linalohitajika zaidi kwenye mahusiano haya.
Kila mmoja wenu hata taka tu kukaa kwenye kitu ya ufalme huu isipokuwa kila mmoja atataka aonyeshe mabavu yake pia.
Kwa ushindani wa kuridhishana kitandani nani atakae mridhisha mwenzie, Nani atakae muhudumia vizuri mwenzie, nani atakae mpa zawadi mwenzie, nani atakae pendeza zaidi ya mwenzie, nani atakaejali zaidi wazazi wa mwenzie, nani atakae mbembeleza zaidi mwenzie.
Yaani ni ushindani wa mahaba makubwa na heshima kubwa hakuna mfano na umejaa hisia kali na kila mtu atakae waona atataka kuwaiga.
Wawili nyie ni sawa na mkaa unaopika chakula ukaongezewa mkaa mwingine, wawili nyie ni sawa na jua moja likaongezewa lingine yaani nyie ni watu mnaendana kuliko kawaida unless mmoja wenu awe kadanganya details;

Binafsi nayapenda mahusiano baina ya Simba na Simba maana wakiungana wanakuwa ni kivutio cha utalii na pia ni nyota pekee katika unajimu zinazoendana sana kuliko zingine kwa maana wote mnatawaliwa na sayari ya jua na hakuna anaeendana na mwingine isipokuwa jua mwenzie ni jua, simba mwenzie ni simba na vile vile mfalme mwenzie ni malkia.

Basi kama bado hamjafunga ndoa mnasubiri nini?

Nyie ni Grand lovers and interesting rivals (wapenzi wakuu na wapinzani wa kuvutia).

Rakims
 
Msaada
ME 30/05 P
KE 09/06 M
Kwa mtizamo mnaonekana nyote wawili ni wenye asili ya upepo wa pumzi hivyo katika vitu vyenu vingi nyie ni kama pacha wa kiroho lakini hiyo haimaanishi kuwa mmekamilika kwa sababu mnaendana kwa asilimia 83%
ingawa mna thamani kubwa ya muendano mtizamo wenu unakuwa
Hakuna mfano wa mahusiano kama yanapokuwa yamejengwa na watu wawili wenye mtizamo huu wa upepo ulio wa kuendana vizuri kwenye haiba,
wenye msisimko na furaha kama wa wewe na mwenzio mnaonekana ni watu ambao hamtawahi kuchoshana au kuchokana kirahisi kwa maana nyie ni kama mapacha na ni wenye nia moja kwa kila jambo ;-
kasi yenu katika mahusiano inashika namba za juu mkiwa pamoja na mnakuwa ni sawa na mfano wa kuigwa kwa mahusiano ya wengine ndio hawa mkikutana utasikia ndoa zingine zinawapigia mfano kuwa unawaona fulani na fulani.

Nyote ndoto zenu kila mmoja kwa mwenzie ni kubwa na hakuna kati yenu anaweza kumkatia tamaa mwingine.
Pia ni wenye mazungumzo ya kuvutia hata chat zenu mtu mwingine akitizama anaweza kutamani jinsi mnavyojibizana na jinsi mnavyoweza kuelewana katika maongezi pia mahusiano yenu yanaonekana kuwa na marafiki wengi na pamoja mnaweza kuwa mnafanya makaribisho ya chakula au sherehe mkiwakaribisha watu wanakuwa wanawatamani sana.
Sex ni mchezo mzuri na uliojaa matani mengi kwenu lakini ndio mahusiano yenu kuna kipindi yanaweza kuwa kama ya juu juu, yasio imara, na msiokuwa na utulivu hasa mkiondoka mazingira ya nyumbani /chumbani na mkikaa muda mrefu bila kukutana na kucheza cheza kimwili basi kila kitu kinakuwa machafuko mkikosa tendo kwa muda ikiwa mnajua au hamjui basi huzuka chokochoko za ugomvi wa maneno.

Rakims
 
Back
Top Bottom