Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu ukipata muda niangalizie hapa kabla sijamuweka ndani huyu mwali
Mimi ni mwanaume
Jina: J
Kuzaliwa: 20 mwezi 08
Yeye
Jina: E
Kuzaliwa: 02 mwezi 04
Haya [mention]Rakims [/mention] Sijawahi kuamini kwenye mambo ya nyota ila kama ukipatia hapa lazima niamini na ntakutafuta
Mimi Me : 03/01 (Herufi ya kwanza D)
yeye ke : 25/09 (Herufi ya kwanza H)
Mkuu mrejesho tafadhaliKe 13/04 H
Me 24/12 S
Shukrani sana mkuuUtangamano
![]()
Katika mahusiano haya wewe ni mwenye moto wa mkaa na yeye ni mwenye moto wa jaha hivyo moja kwa moja nyote wawili ni wenye kuendana vema hasa ukizingatia tabia zenu ni kama washindani wawili wenye kushindania mahaba...
Wawili nyie ni sawa na Watu maarufu kinyota kwa maana ni wenye kuendana sana na hasa linapokuja kwenye suala la chumbani ni wenye mapenzi ya kushangaza.
Ni wenye kufanya kila kitu kinachohusu mapenzi kama ushindani yaani nani mshindo ni wenye kupenda matani ya mara kwa mara. Ingawa wewe ni mwenye Mood swing na yeye ni mwenye kupenda kuwa mood off.. lakini muda mwingi utakuta ni watu wenye mapenzi makubwa.
Kwa uaminifu wewe ni muaminifu katika mapenzi lakini kwa upande wake punda ni punda tu hivyo utatakiwa umfanye atulize kishwa.
Linapokuja swala la kujamiiana kwenu ni vita. Kila mtu anakuwa kajiandaa vya kutosha ingawa face expression muda mwingine inaweza ikawa haijitoshelezi..
Lakini moyoni ni wenye kujiambia hapa sikubali kushindwa, Ni watu ambao mnachangia kupendezewa na vitu sawa.
Kwako hufikia umri ambao utajikuta ni mtu mwenye kupenda sana kwenda sinema na yeye ni mwenye kuvutiwa zaidi kufuatilia sinema..
Mara nyingi movies zako pendwa ni Sci-fi na Fantasy na yeye ni Actions and Intelligence hivyo ni wenye kuvutika kila mmoja wenu na mwenziwe anachopenda.
Hivyo hivyo hata kwa vitu ambavyo hampendi navyo hufanana kwenu. Tatizo lenu kubwa kwenye mahusiano haya ingawa mnaendana sana ni jambo moja.
Kila mmoja wenu anagubu la asili na kupenda kulalamika kwa kitu kidogo hasa kwa upande wako ambaye kila kitu wewe hupeleka moyoni.
Kila mmoja kati yenu ni mwenye kutaka kumtawala mwenzie..
Wewe ni kama mfalme kutawaliwa ni jambo ambalo halikuvutii hata katika historia ya maisha yako na yeye ni kama Amir Jeshi Mkuu.. Kutawaliwa kwake ni Mwiko..
Ili mahusiano yenu yaweze kwenda kila mmoja huvutiwa zaidi na mwenzake akiwa atampa uhuru wa maamuzi na kujitawala.
Shida nyingine katika nyumba yenu. Wewe ni Mtu utakuwa mwenye kupenda watu yeye atakuwa hataki watu hata kidogo.
Either atakwambia au hata kwambia mwisho wa siku kila anaekuja kwenu yeye atakuwa anamtoa kasoro ili tu ifikie sehemu aone vibaya awaache.
Rakims
Na je? Tunaangukia mlango wa ngapi kweye ndoa?Mkuu ukipata muda niangalizie hapa kabla sijamuweka ndani huyu mwali
Mimi ni mwanaume
Jina: J
Kuzaliwa: 20 mwezi 08
Yeye
Jina: E
Kuzaliwa: 02 mwezi 04
Mlango wa 6... ambao ni mlango wa huduma na Afya..Na je? Tunaangukia mlango wa ngapi kweye ndoa?
Utangamano:
Mahusiano haya ni sawa na watu wawili waliokosa uelekeo. hawa ndio ukiskia mtu kakosea kuoa au kuolewa.
Wewe ni mchanga wa bahari na yeye ni upepo wa juu.
Licha ya kutokuendana hata kukaribiana hamkaribiani, hili utajionea maana ya ile kauli kwamba unaweza kukaa kwenye uhawara miaka 10 lakini mwaka mmoja wa ndoa ukakushinda.
Mtizamo upo hivi:
Wewe ni mtu mwenye kuvutiwa na yeye kwa sababu ana mvuto ambao wewe unajikuta ni mtu wa kumbembeleza pamoja na kubembelezea mapenzi.
Upendo mlionao unaweza kukuokoa kwa kipindi fulani lakini hizi ndio ndoa ambazo wenza huwa wanarushiana ngumi maana ni uvumilivu hadi una fikia hatua ya kukata tamaa.
Japo mtafanikiwa kupata watoto kirahisi na mtazaa watoto wazuri kwa kuwa tu mnaingia mlango wa 5 kwenye ndoa yaani kizazi na mali lakini mateso ni makubwa kuliko mapenzi.
Yeye ni mtu mwenye tamaa na wewe kwenye mahusiano kwa muda huo ambao utakuwa nae au mtakao kuwa pamoja.
Elewa ya kwamba mahitaji yake katika mapenzi kuna jinsi na hali atakazo kuwa anataka uwe na wewe hutakuwa na uwezo wa kumpatia, Kikubwa wapo ni hisia haijarishi utafanya nini kwake hataona ukweli wa hisia zako kumpenda na ataona ni maneno tu.
Pia kutoshelezana kwenu ni kwa uchache sana yeye anapenda sana mauno na wewe magoti kidogo itafikia sehemu itakuwa ni mtihani kipindi hiki kwanza utakua huelewi elewi utakuwa unaona kama ni mtu asiyesomeka,
Baadae mwezi wa 9 hadi wa 10 kama hujamuoa anaweza kukwambia anaona uelekeo wa maisha hauoni na kuna uwezekano mkubwa mwezi huo wa mwaka huu akaanza kujihusisha na mtu mwingine na pia utapata habari kupitia mawasiliano yake kwa hivi sasa.
Atapenda mambo ambayo hutaweza kumtimizia kwa wakati anaoutaka sio kwamba huna uwezo wa kutimiza na akiwa tofauti na mtu mwingine utaona hiyo tabia hana atakuwa nayo kwako.
Na katika hali za kujionyesha na kuwaonyesha watu kuwa ana jambo fulani ni tabia ambayo wewe huna kitu ambacho yeye hupenda mtu aliyenae awe hivyo
Na utakuwa ukimuheshimu kwenye mahusiano na yeye atakuwa anakuchukulia kama ni mpuuzi atakuona mbinafsi na unakosea na mapenzi hayapo hivyo na utatolewa kasoro kila mara.
Baada ya hapo kwenye mahusiano hukugeuka na kuanza
kuangalia mahali pengine na kukuweka uwe na wivu nae kwake ni starehe yake japo ni jambo litakalo kuwa linakutesa.
Japo kuwa ni mtu mzuri kwa watu wengine kwako wewe mahusiano haya ni Kichocheo cha maafa (Sijataka kwenda deep sana kwenye case ya wazazi ambayo ndio inanifanya nikwambie ni mtu asiyekufaa.
SEHEMU YA HISIA:
Kiuno chake ndio sehemu inapotawala hisia yake utaona analalama kiuno kinasumbua ili tu kupata kupapaswa na kukandwa eneo hilo.
Rakims
Vitu vyote vinavyotegemea nyota ni kuacha kushirikiana mfano biashara kila mtu afanye yake..kwahyo suluhisho ni lipi.
Mana ikitokea watu wamekuwa pamoja kwa muda mwingi na kuzaa watoto haiwezekani kuvunja ndoa kisa hamjaendana.
Suluhisho ni lipi hapa ili kuenenda pamoja
asante.
Shukrani Kwa ilimu mkuukwahyo suluhisho ni lipi.
Mana ikitokea watu wamekuwa pamoja kwa muda mwingi na kuzaa watoto haiwezekani kuvunja ndoa kisa hamjaendana.
Suluhisho ni lipi hapa ili kuenenda pamoja
asante.