Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Mimi : Mme
Tar: 9 April jina R

Yeye : Mke
Tar: 28 April jina A

Rakims

Status : uchumba sugu
 
Mke 18 Feb 1972 jina N
Mme 21 July 1968 H
Mahusiano haya ni baina ya Upepo wa kimbunga na Maji ya bahari.

Mwanamke ni Upepo wa kimbunga na mwanaume ni Maji ya bahari kwa mtizamo tu hapa kitakachotendeka ni Tornado hivyo baina ya nyie wawili kati yenu hakuna heri na kuna nafasi kubwa mkatengana kwa shari.

Utangamano
Mahusiano haya ni baina ya Nyota ya maji ya bahari na upepo wa kimbunga, Kiasili wawili hawa wakiwa pamoja kwa upole basi utaona kila mtu anapenda mapenzi yao ya awali na kila mtu atawaonea tamaa mahusiano yao.
Lakini ukweli ni kwamba upepo wa kimbunga na bahari siku zote mapenzi yakitaka kuwa moto moto basi Dhoruba hutokea.

Ukiwatizama wawili hawa yeye ni mwenye nyota ya Kaa anakuwa na tabia za uchangamfu, kujituma basi utaona ni mwenye kupatiana sana na wewe Ndoo ambaye ni mwenye tabia ya kujitawala.

Kwa upande mwingine utaona yeye ni mwenye kung'ang'ania vitu ni tabia ambayo itakuonyesha waziwazi na hukufanya wewe (Aquarius) ujisikie umebanwa na unakosa uhuru binafsi kama awali.

Na kwa kuwa wewe ni mwenye akili ya haraka, usiyetabirika, atakuona unaanza kupapatika na tabia yake ya kung'ang'ania vitu, yeye (Kaa) ana ubishi na ujeuri wa asili na pia huwa ni king'ang'anizi.

Na kwa yeye mwenye roho ndoo ni rahisi sana kuumizwa na masihara yako ya kutaka kumcheka yaani anaweza kuleta hisia na wewe ukawa unacheka ama kuonyesha kutokujali,

Yeye binafsi ni mtu ambaye atajikuta hakuelewi wewe hasa ukizingatia kwamba yeye ni mwenye kupenda kujihisi amelindiwa mapenzi yake na yupo karibu na mwenza wake, lakini wewe ambaye ni mtu wa ajabu na matukio hukufanya ukihisi kukosa ukaribu nawe kulingana na visa vyako.

Wewe kwako ni sawa na mbwa mwitu kwake, kwenye sex mnaendana sana isipokuwa kuna kitu kinakosekana kikubwa kwenye mahusiano haya.

Rakims
 
Back
Top Bottom