Nitajie viongizi watatu tu wa Upinzani waliopigana vita ya Kagera kwa namna yoyote ile ukimuondoa mzee Mrema!

Kwa hiyo kizazi cha walioshiriki moja kwa moja kikimalizika itabidi tuanzishe tena vita nyingine? Kuna mataifa hawajawahi kupigana vita vizazi na vizazi. Je hawana uongozi ktk mataifa hayo?
 
Nyumba za umma za Tanzania ziliuzwa kwa mahawala na waliopigana vita wakiongozwa na chizi wa taifa
 
Wakati wa hivyo vita Mbowe alikuwa na miaka 20 na alikuwa mwanafunzi, Lisu miaka 12, na Zito miaka mitano.
Mbowe alikuwa anatoroka usiku kwenda vitani asubuhi anarudi shuleni huku kachokaaaa.
 
Hivi kwenye CCM kuna aliyepigana vita ya Majimaji?
 
Mliziomba wenyewe, tena inavyoonekana mtumbua macho ndio alikuwa kiti cha mbele
 
Kwa hiyo kizazi cha walioshiriki moja kwa moja kikimalizika itabidi tuanzishe tena vita nyingine? Kuna mataifa hawajawahi kupigana vita vizazi na vizazi. Je hawana uongozi ktk mataifa hayo?
Hujaelewa swali bwashee!
 
Hiyo vita ya Kagera tulipigana sisi kama nchi wote kwa ujumla wetu wakubwa kwa wadogo, wazee na vijana. Hata wale ambao wlaikuwa hawajazaliwa wamepigana kwa namna moja ama nyengine kwakuwa wote tulipitia hali ngumu baada ya ile vita na uchumi ukadorora.

Mwalimu aliyekuwa anafundisha shuleni wakati inaendelea nae alipigana, wlaiochangia mihogo na mahindi walipigana na wale wafanyabiashara waliotoa magari nao walipigana.
 
Hata watoto wanaozaliwa leo wanakutana na mapambano ambayo yamesababishwa na hiyo vita nao wanapigana.
 
Swali lako limekaa vibaya, bora lingekuwa utajiwe viongozi gani wa sasa walioshiriki kumng'oa Idd Amin! Ni karibu miaka 40 sasa tangu ile vita iishe, kweli unategemea viongozi (upinzani au utawala) wawemo kwenye hio orodha, hawa walikuwa watoto wakati wa vita! Trash huu uzi!
 
Wapo wengi tu bwashee!
 
Wote waliokuwa wameisha fikisha umri wa miaka 18 wakati huo walipigana vita wengine walitumia muda mwingi kuzalisha chakula naduwa ili jeshi letu lipate ushindi kupigana vita sio mpaka ubebe bunduki wengine walipigana kwakuliunga mkono jeshi na kulinda nyumba zao
 
Aisee, huyu naye anataka watu wapoteze muda kumjibu!!!! Vita vya Kagera unajua vilikuwa mwaka gani? Unajua vyama vingi vilianzishwa/kurudi mwaka gani? Ukijibu hayo maswali mawili, sasa nijibu na hili: Mwaka huo (wa vita) Zitto, Lissu, Mbatia etc walikuwa na uwezo wa kuingia vitani kwa umri waliokuwa nao???? Makaburasha mkubwa wewe!!!!!!!
 
Kupigana sio kuvaa uniform za jeshi na kwenda vitani, mm nimepigana vita ya kagera but kazi yangu ilikuwa ni kufanya kazi ya Hao wanaovaa uniform iwe rahisi zaidi

So it's very possible kuwa wapinzani wapo ambao walipigana ila ni ngumu kuwajua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…