Nitajie wachezaji watatu waliokuhamasisha kuupenda mchezo wa soccer

Pia Kuna super sub wa Liverpool Ryan Babel..

Huyu jamaa Dunia inamtambua kama SUPER SUB OF ALL THE TIME

Aliwai kupiga shuti akiwa katikati ya uwanja na mpira ukaingia kimyani..

RYAN BABEL
 
Haha golikipa Petr Cech anaifahamu shughuli ya David Beckham
 
Haha golikipa Petr Cech anaifahamu shughuli ya David Beckham
Na mimi nikajifunza kupiga kama yeye, siku moja kwenye michezo shuleni sekondari wakati wa mazoezi mwalimu akatenga mpira akaniambia nipige, alishika kichwa hakuamini!
Aliniambia “Nifah, hata wavulana kwenye kikosi chetu hawapigi hivi. Kwanini hukuwa mwanaume?, hiki ni kipaji” Heheee
 
Kuna mdada wa kuitwa Catherine umenikumbusha tumecheza nae sana sanaaa alikua na huwezi mkubwa sanaa uwanjani😀😊😊
 
Jorge Alberto González Barillas aka el-magico' wakati amesajiliwa na Cadiz mwaka 1982 pale spain. Alianzia Segunda division ...jamaa alikuwa anajua mpira zaidi ya Maradona.

Yaani maradona akasome kwa el magico. Mbaya ni kuwa jamaa alitokea taifa maskini la america ya kati..el salvador na hakutaka kuchezea klabu kubwa barani ulaya.
 
Mwingine aliyenifanya nipende mpira miaka ile ya mwanzoni 80...alikuwa ni mtambo wa magoli pale spain akifahamika kama Hugo sanchez marquez...vijana wa sasa hamwezi kumjua huyu...jamaa alisajiliwa kwa mkopo pale atletico madrid kisha baada ya kukiwasha wakamchukua huyu jamaa mazima ..alikuwa ni hatari sana ktk kuzifumania nyavu mpk Real madrid ikamsajili na akakiwasha vilevile....jamaa alikuwa ni fundi wa kukaa kwenye nafasi na alikuwa na magical touch aisee tulioangalia la liga miaka ya 80 tulifaidi sana kuona vipaji vya mpira ambavyo havitakaa vijirudie.
 
Miaka ya 2009 kama skosei nilikuwa shabiki kindaki ndaki wa Yanga aliyenifany niwe shabik wa yanga enzi hizo alikuwa ni Mrisho ngassa na Jerry tegete,

Siku zikaenda katk harakati za ukuaji nikajikuta tu napotezana na mpira wa Bongo maan enzi hizo mpira kusikiliza mpak kwenye redio mi nkaona kero hii lakin ghafla katk kurejea ten kushabkia mpira wa bongo miaka ya 2019 hivi nkajikuta nimeibukia tu kuwa shabiki wa Msimbazi mpak leo hii.

Kuhusu soka la nje Zaman nlkuwa shabiki wa man utd ila baad ya kumuuza ronaldo nkaona hapa pameshakuwa Bondeni tayari ni kuhama mapema kabla mafuriko hayajaja kuezua mabati, nikahamia Liverpool sijajutia uamuzi huo maan Hat nyie wenywe mnaujua moto wa mijogoo ya Landani.

Aliyenfanya niupende mpira ni Fundi ronaldinho na ricardo kaka maan enzi hizo ndo walikuwa wanatamba sana kabla ya kuja mwenye mpira wake Messi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…