Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 2,331
- 7,733
Huyu ni miongoni mwa trusted lieutnants wa Rais Samia. Kuna sakata la wafanyabiashara linaendelea hapo kariakoo.
Wafanyabiashara wametoa ya moyoni, wamemkaanga kisawasawa na kumtuhumu Waziri wa Fedha kama kikwazo katika biashara zao.
Wafanyabiashara wakaenda mbali sana na kudai waziri huyo ni jeuri sana na ana dharau za kutosha.
Sasa turudi upande wa pili wa shilingi, Mwigulu ametikiswa na Serikali imetikisika. Wananchi wanasubiria kama atatumbuliwa na Rais Samia.
Tupunguze matarajio hayo, sidhani kama Mwigulu ataondolewa hapo, kwakuwa yupo hapo kwa kazi maalum hivyo ni ngumu kumuondoa, kama unabisha muda ni mwalimu mzuri utatuambia.