Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Nitakuwa wa mwisho kwa akili zangu kuamini kua Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Mhe Freeman Mbowe ni GAIDI kwa sababu zilizo wazi kabisa. Mbowe hana chembe chembe za ugaidi na ni ajabu kuamini eti yeye ni gaidi.
Sababu za kunifanya niamini kua Mbowe si gaidi ni hizi:
1. Mbowe ndiye kiongozi pekee wa upinzani ambaye mbinu nyingi ovu za kumfifisha zimeshindwa.
2. Mbowe ameharibiwa mashamba na mali zake zote lakini hakuwahi kushuka kisiasa
3. Kupishana kwa kauli ya Msemaji wa polisi na hati ya mashtaka kua alikua na njama za kupanga kuua viongozi wa juu wa serikali, hizi zilikua tuhuma za uongozi za polisi kisha DPP akaondoa.
4. Kauli tata za wenye Mamlaka kua Mbowe alifunguliwa kesi toka mwaka jana na wengine wemeshshukumiwa wakati si kweli.Kesi ya Mbowe imefunguliwa mwaka huu.
5. Kauli aliyosema ameisikia Mbowe toka kwa RPC wa Kinondoni ndugu Kingai kua mara hii hachomoki. Hii inatoa taswira kua Ugaidi wa Mbowe ni wa kupewa.
6. Kauli ya IGP kua Mbowe naye ni binadamu anatenda makosa, hii ni kauli tata maana makosa huangaliwa kwa records za mtu na dhamira ya moyo wake. Hapa IGP alitaka kutuaminisha tuamini kua Mbowe ni gaidi.
7. Kauli ya Rais kua polisi walikua wanawabambikia watu kesi. Kama ikiwezekana hivyo,kwanini isiwe kwa Mbowe?
8. Kukamatwa viongozi wengine wa CHADEMA wanaozungumzia katiba. Kwani kuna dhambi gani kujadili katiba?
Kwanini tusiamini kuwa hili ndilo linalomweka Mbowe mahabusu hadi sasa?