Nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba Israel Patrick anamzidi chochote David Kameta

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Kitendo cha kumtoa kwa mkopo beki David Kameta Duchu, kwenda Biashara United, na hatimaye sasa anaichezea timu ya Geita Gold na kumpisha Israel Patrick Mwenda mwaka 2021, kwa maoni yangu suala hili Viongozi wa Simba SC hawakulitazama kwa upana wake.

Nithubutu kusema kwamba nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba Israel Patrick Mwenda ni beki bora kwa upande wa kulia kuliko David Kameta Duchu na kuamini kuwa ni masaidizi sahihi wa Shomari Kapombe ambaye ni beki bora kuliko wote Tanzania kwa wakati huu.

Duchu Performance yake ni nzuri sana uwanjani, anakaba na kushambulia, na Krosi nzuri, energy ya kutosha kabisa, kuliko Mwenda ambaye back pass ni nyingi na Krosi ambayo asilimia kubwa zinapotea.

Ni wakati umefika sasa kwa Kijana kurudi kwake Unyamani, Simba SC.
 
Kocha mpaka akupange unaekuza kiwango na ligi ilivoyamoto sijui lini. Kwahiyo Ni Bora kukuza sehemu unayokua na uhakika wa namba.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Ndo maana nikasema kwa kiwango chake hamzidi chochote Israel Patrick

Kwa Kocha Pablo Franco anavyowamini vijana akina Banda, Patrick, Sakho, Jimmyson...Sioni kama anaweza kukosa nafasi kwa baadhi ya michezo.
 
Simba ina kikosi kipana bhana. Sidhani kama pengo lake linaonekana pale. Si hata mkongwe Erasto Nyoni anaweza kucheza full back 2?
 
Simba ina kikosi kipana bhana. Sidhani kama pengo lake linaonekana pale. Si hata mkongwe Erasto Nyoni anaweza kucheza full back 2?
Yes, hakuna pengo lake, lakini nilikuwa naangalia kuwa usahihi wa msaidizi wa Kapombe kuwa Patrick kwanini asiwe Kameta
 
Kila mmoja ana uzuri wake na udhaifu wake... David Kameta Duchu ni mzuri kushambulia lakini si mzuri kukaba awali Mohamed Hussein alikuwa hivyo lakini akafanyia kazi udhaifu huo

Patric Israel Mwenda Mzuri sana kwenye kukaba shida yake iko kwa majalo kumwaga maji kwake ni mtihani.

Mimi ningefanikiwa kukutana na Duchu ningemshauri abadiliahe position acheze kiungo au winga.
 
Kucheza timu kubwa ligi ya bongo Kuna la zaidi kuliko hata kipaji Cha mchezaji...
Kipaji bila jitihada sawa na hakuna, mfano Ajibu Migomba ana kipaji lakini hana jitihada.

Kama Duchu atazidisha jitihada basi ubora utaongezeka na mapungufu yataisha.
 
Kipaji bila jitihada sawa na hakuna, mfano Ajibu Migomba ana kipaji lakini hana jitihada.

Kama Duchu atazidisha jitihada basi ubora utaongezeka na mapungufu yataisha.
Cha zaidi ya kipaji hapa bongo ni kujitambua .. upo sawa.
 
Duchu alishindwa kuonesha alichonacho Ila hata mkopo kwenda Biashara alitolewa ili akakomae kimataifa
 
Tatizo jina nadhani,walifikiri ni Zuchu,kazi yake ya Jana ilikuwa balaa,kama siyo weledi wa wananchi angeibuka shujaa.
 
Kocha wa simba wa wakti ule hakujua kuishi na wachezaji nje ya ile regular lineup..kila mechi ni zimbwe na kapombe; VPL haohao, CAF haohao, FA haohao sijui mapinduzi nk matokeo yake yanaigharim simba hata leo sabab ya prolonged fatigue..replacement wao hawakosekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…