Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Nimeona baadhi ya mashabiki wa Yanga na wengine wa upande wa pili wakiwaponda Yanga kwamba tayari wametolewa kwenye mashindano na Al hilal. Mpira hauko hivyo waungwana, bado Yanga anayo nafasi ya kusonga mbele tena kubwa sana.
Katika mechi ya Jumamosi sikuona kitu cha ziada ambacho Al hilal aliizidi Yanga ndani ya uwanja. Tamaa ya yanga kutaka kufunga goli la 2, kuliwafanya wajisahau kuwa makini katika ulinzi. Wametengeneza nafasi 3 za wazi wakashindwa kuzitumia, hiyo tu ni ishara ya timu ambayo inaweza kufanya lolote kwa wakati wowote ndani ya dk. 90.
Yanga anakwenda Sudan akiwa na chaguo la kushambulia mwanzo mwisho, na sitegemei kwamba Al Hilal watakaa nyuma muda mwingi kufanya mashambulizi kama walivyofanya kwa Mkapa. Watafunguka wakiwa kwao na mianya itapatikana, na kwa namna ambavyo nimewaona wanacheza Yanga wanayo nafasi ya kufunga magoli.
Kumbuka ushindi kwa Yanga utawavusha, na sare yoyote ya kuanzia goli 2 unawavusha, kwaiyo Al Hilal ndiyo wenye kibarua aidha walinde goli lao la ugenini ama wafunguke kutafuta goli jingine. Na hapo ndipo ilipo faida kwa Yanga.
Na mechi ijayo nafikiri Nabi amrejeshe kwenye kikosi Mwamnyeto halafu Bangala arudi kucheza namba 6 yake, Aucho asogee 8 na Aziz Ki aanzie benchi. Aanze Fei Toto namba 10 maana ni mechi ya kutafuta matokeo na si vinginevyo.
Binafsi yangu bado naiona nafasi ya Yanga kutinga makundi, kwani bado naziona dk. 90 za moto pale Omdurman, Sudan.