Nitakuwa wa mwisho Kuuamini huu Upuuzi ambao naona Simba SC yangu wanaanza kutaka Kuutumia kama sababu ya Kushindwa

Achana na huyo jamaa kwanza haelewika anabadilika badilka tu hajulikan anasimamia kitu gan
 
Mh,nani atafanyia kazi assumptions?!?.ni kupoteza muda kulalamikia hili hata kama una haki ya kulalamika.cheza mechi akuonee ndio ulalamike!!.ukienda mchezoni na wazo hili hata akichezesha vizuri namba gani na ukapigwa5 bado utaona umeonewa!!!.kuna kipindi malalamiko yalipelekwa mpk FIFA kwamba mnahujumiwa and what was the result??!!??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye dunia ya Leo huwezi kuita hiyo ni figisu,were jiandae kucheza katika mazingira yoyote.nchi zililalamika FIFA world cup QATAR kwani FIFA wamebadili chochote!!!!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
siamini kama Simba wameshatolewa bado wana nafasi kama watakuwa makini na kuweka nidhamu ya mpira natamani Nyoni ndio angekuwa nahodha kwani ni mtulivu na anaiongoza vyema timu uwanjani tatizo ni hawa wanasiasa wanaleta siasa zao kwenye mpira ukichukulia mpira wameujulia ukubwani siasa zao wasituletee kwenye mpira
 
Mtoto wa kinondoni katika ubora

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si kila jambo unaweza kulizungumzia, mengine yaache yapite. Upande huu nimekuona mtupu kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye dunia ya Leo huwezi kuita hiyo ni figisu,were jiandae kucheza katika mazingira yoyote.nchi zililalamika FIFA world cup QATAR kwani FIFA wamebadili chochote!!!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni shabiki wa yanga kwa bahati mbaya sana huujui hata mpira wa mdomoni, fatilia nimeanzia wapi na mleta uzi kisha uje uweke mahoja
 

Kama na Wewe hizo ' Figisu Figisu ' unazijua kwanini hukumchezesha TP Mazembe Saa 11 Alfajiri au Saa 2 asubuhi? Ni Wewe tu Mpuuzi mmoja ndiyo hujajua mpaka leo kuwa GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE ni Mwana Simba Sports Club tena wa Kindakindaki kama siyo Lialia kabisa. Tatizo lenu Watanzania wengi huwa mnapenda Kupakwa Mafuta tu na Kusikia Habari nzuri ambazo zinawapendeza ila akijitokeza Mtu ' Neutral ' kama Mimi na ambaye sina Unafiki wala Mahaba niue ya Kipumbavu nikisema ukweli mnanichukia na kuanza kusema kuwa Mimi ni Yanga FC. Kwa kukusaidia tu ni kwamba naijua Simba Sports Club yako na mambo yake ya ndani kuliko Wewe na nimeshahatarisha Maisha yangu sana kwasababu ya Kuipigania Simba SC yangu na kama haitoshi Wachezaji wako wa Simba SC tena wale ' Waandamizi ' kabisa waliokuwa Team B iliyokuwa huko nyuma chini ya Rafiki yangu mkubwa Nahodha mwenye Mafanikio makubwa Simba SC Suleiman Abdallah Matola a.k.a Mzambia a.k.a Veron na Meneja wa sasa wa Simba SC Patrick Rweymamu wengi Wao Mimi ndiyo Mshauri wao na hupenda Kuniita Kaka Mkubwa. Huyu Haruna Niyonzima unayemuona sasa hivi amerudi katika ' Form ' hivyo nisingejitolea kwa Kushirikiana na Watu baadhi wa ndani wa Simba SC hadi Yule Mkuu wa Itifaki Makoye ( Mvaa Suti ) ili kumsaidia alikuwa ndiyo amemalizwa hivyo. Na sijataka Pesa yoyote ya Asante kutoka Kwake au kwa Simba SC ila nimefanya tu kwa Mapenzi yangu makubwa Kwake. Sasa najipanga tena kutoa aina hiyo hiyo ya Msaada wa Mchezaji wa Kigeni wa Kizambia Clatous Chota Chama ambaye nae pia anaanza Kupotea.
 

Siku zote huwa nachukiwa kwakuwa tu nasema ukweli na Mimi sina damu au chembe chembe za Unafiki Mkuu. Hebu muulize huyo ' Mpumbavu ' mbona mara kwa mara nikiwa naanzisha hapa ' Threads ' za Kuisifu na Kuipongeza Simba SC yetu huwa simuoni akinipongeza? Ila leo GENTAMYCINE ' nimenyooka ' naonekana Adui, Mbaya na mwana Yanga SC.
 
Kweli kabisa!!.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kujitapa hujui lolote mtu wa Mbande wewe, mimi ni mwanachama wa SSC nafahamu mambo ya SSC
 

Kwahiyo hiyo Bahati ya Angola ndiyo unadhani nawe Mtanzania utakuwa nayo? Hivi kwanini bado kuna Watu wa ' hovyo hovyo ' hapa duniani? Na ulivyo mgeni na Mshamba wa Mpira umesema tu ni Timu ya Angola ila hujaiweka hapa na Mimi nilitaka uiweke hapa ili tuichambue Kiuwezo yenyewe na Simba SC yetu.

Bado nasisitiza na sitotengua haya maneno yangu kwamba Simba SC si Timu mbaya na nawashukuru mno Wachezaji, Benchi la Ufundi zima likiongozwa na Kocha Mkuu Patrick Aussems, Viongozi Wakuu na Mdhamini Mkuu ila ukweli utabaki pale pale kuwa kwa Kikosi hiki cha Simba SC hakiwezi Kushidana na Vilabu vilivyopo katika hatuao hii ya Robo Fainali hasa kutokana tu na aina ya Wachezaji ilionao.

Kikubwa tu Timu iende Kucheza na TP Mazembe kwa malengo makubwa mawili tu ambapo lengo la Kwanza liwe la Wachezaji wa Simba SC kukazana wacheze vizuri ili ikiwezekana basi TP Mazembe au hata Vilabu vingine viwasajili kwa Vitita vikubwa wakacheze nje ili idadi ya Wachezaji wetu wa Kigeni iongezeke Tanzania na lengo la Pili Timu iutumie huo Mchezo kama sehemu yake ya Kuzidi Kujikomaza zaidi Kimchezo ili izidi kuendelea kufanya vizuri katika Ligi ya TPL ambayo naweza kudiriki kusema kwamba kwa aina ya Kikosi cha Simba SC hiki cha sasa kwa Ligi ya TPL hakuna Timu ya Kuisimamisha na kwamba Simba SC inaenda Kuutetea tena Ubingwa wake tena mapema mno huku ikimzidi atakayemfuatia kwa Alama ( Points ) nyingi tu.
 
Mpemba wako kasèmaje kuhusiana na badiliko hili?

Maelezo yangu tu katika huu ' Uzi ' ni jibu tosha Kwako kama Simba SC itashinda au itafungwa hiyo Jumamosi. Rudia tena Kuzisoma ' posts ' zangu zote katika huu huu ' Uzi ' ili uweze kujua Je Simba SC atashinda au atafungwa kwani tayari nimeshaweka kila Kitu wazi japo sijataja tu idadi ya Magoli tutakayoyahifadhi katika Kikapu chetu huko Lubumbashi.
 
Achana na huyo jamaa kwanza haelewika anabadilika badilka tu hajulikan anasimamia kitu gan

Mpumbavu kama Wewe na Wenzako baadhi kamwe hamna ' IQ ' ya Kumuelewa vyema GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE.
 

Hata huyo Erasto Nyoni wako hapo Simba SC anaoneka mzuri na katulia kwakuwa huwa analindwa vizuri mno na ' Unsung Hero ' Kiungo ' Mtifuaji ' Mghana James Kotei ambaye ndiye huwa anahakikisha ' back line ' yote ya Simba SC iko salama na haipati madhara yoyote. Mchezaji wako mwenyewe mahiri kabisa Kiungo Jonas Gerald Mkude anakuambia hirizi yake inayomfanya awe anang'aa vyema na kutembea vizuri pale katikati huku akizitupa huku na kule na zile Kampa Kampa tena ni pale tu nyuma yake akiwa anazibwa na James Kotei ambaye hadi sasa ndiye Mchezaji pekee wa Simba SC anayeongoza Kukimbia umbali mrefu ndani ya Uwanja kuliko Mchezaji yoyote mwingine wa Simba SC hii ya sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…