Nitamsaidia Humphrey Polepole kutaja wahuni(Hooligans) ambao sio tu hawakumalizwa bali waliongezeka awamu ya tano mara 100 zaidi

Nitamsaidia Humphrey Polepole kutaja wahuni(Hooligans) ambao sio tu hawakumalizwa bali waliongezeka awamu ya tano mara 100 zaidi

Anawajua maana waliwapandikiza Bashiru, yeye Polepole, Bashite na mwendakuzimu, kwa hiyo awataje wahuni wao, kutesa kwa zamu, wamewatelekeza keki ya taifa wanakula wengine, wao macho kodo.
Wateeseke na wao, shenzitaipu hao.

Everyday is Saturday................................😎
Wahuni wengine huko Bandarini Beseni limepinduka.
 
Ndani ya Nissan nyeupe na Noah nyeusi walikuwa Kingai, Mahita, Goodluck na Jumanne.

Sabaya na mwenzake wa Dar hawakucheza mbali.

Ninaunga mkono hoja, Polepole:

"Mnavuna mlichopanda. Na bado!!"
Ndio Kamanda Mhina kawataja
 
Upumbavu wake ni upi??? Hoja haipigwi rungu...hujibiwa kwa hoja
Je si kweli kwamba wabunge na madiwani wa upinzani walinunuliwa kwa kuhonga pesa, kurudishiwa ubunge na vyeo??? Mashinji ni nani sasaivi????
Je siyo kweli kwamba KOROSHO Za wakulima ziliporwa na baadhi yetu tuliitwa kangomba kwa kuwatetea wakulima!
Je siyo kweli kwamba mlidanganywa kwamba mnajenga miradi kwa pesa za ndani KUMBE URONGO juzi NAPE Kauliza ukaguzi wake kila mtu Anamkebehi ajuavyo KISA inakopa MAGUFULI raisi wa PROPAGANDA NA UONGO
Je siyo kweli kwamba mli ua na kutesa mliowaita WAPINZANI? Ben Sanane yupo wapi, Anzory Gwanda yupo wapi?( rejea yanayosemwa na kina Adamoo hapo mahakamani??)
Ulipaswa kusema mtoa mada ni mpumbavu kwa kujibu facts siyo unawaita watu wapumbavu bila facts.
Asante kwa kusoma
Hao wahuni sana Polepole kawaweka wazi.
 
Wahuni ni wengi na muda ni mchache!Treni iko wapi sasa?😁😁😁
 
Anawajua maana waliwapandikiza Bashiru, yeye Polepole, Bashite na mwendakuzimu, kwa hiyo awataje wahuni wao, kutesa kwa zamu, wamewatelekeza keki ya taifa wanakula wengine, wao macho kodo.
Wateeseke na wao, shenzitaipu hao.

Everyday is Saturday................................😎
Wahuni leo watalala na viatu. Jumba bovu la Bandari mama katupia jiwe fatuma.
 
Mh Polepole naona anazunguka sana kuwataja majina na level zao wahuni ambao anadai Serikali ya Awamu ya Tano ilishindwa kumalizana nao.

Kwanza Polepole anakubali kuwa Wahuni hao ni wanachama wa ccm.

Pili Mh Polepole hakatai kuwa Wahuni hao( Hooligans) ni viongozi ndani ya chama na wengine wameshika nyazifa mbali mbali ndani ya serikali.

Mh Polepole anakubali kuwa hao wahuni ni watu walioaminiwa na wananchi wakapewa dhamana ya kuongoza.

Katika kipindi cha miaka 5-6 tumeshuhudia uhuni mwingi waliofanyiwa watanzania. Hasa chanzo kikiwa ni kutoka ndani na nje ya chama cha mapinduzi ambacho Polepole anakiri wahuni wako huko.

Sasa wahuni hawa Hapa. Polepole acha kuzunguka mbuyu. Hata wewe ni Mhuni. Hujamalizwa ile umekatwa mabega yalitaka kuzidi kichwa. Sasa ule uhuni umekutoka unaona wivu kwa wahuni waliobaki. Uhuni ni sifa ndani ya chama chenu kama ulivyofafanua.

1. Wahuni walidiriki kudanganya watanzania kuwa pesa za miradi ni za ndani kumbe walikuwa wakikopa kimya kimya na hatujui kama hizo pesa wahuni waliweka kwwnye miradi zote au zingine zilidondokea mifukoni mwa wahuni

2. 2019 Tanzania ilishuhudia vurugu( political hooligans) ikifanyika wakti wa uchaguzi wa serikali za mitaa. Ule ni uhuni wa karne.

3. Wahuni hawa walijaa kila kona ya nchi wakitembelea Noah Nyeusi na Nissani Nyeupe. Kiukweli yeyote aliyekutana nao hadi leo hajasahau kama hajfa basi kabaki na ulemavu wa kudumu. Wahuni wanatoka ccm kwa mujibu wa Polepole na wengine ni viongozi ngazi mbali mbali.

4. Wahuni wana tabia za kuharibu na kupora mali za waungwana. Kumbuka korosho za mtwara, Nyumba za kimara Dar es Salam na pesa za rambi rambi za Bukoba.

5. Polepole akiwa kiongozi wa wahuni anatuhumiwa kuendesha kampeni za kihuni za kununua na kuuza wabunge kutoka vyama mbali mbali vya siasa. Kama kawaida ya wahuni hawakununui kwa pesa tu bali kwa vitisho kutaka kukua, kukuharibia mali, kukuachia ulemavu na Kukufunga kwa kesi ngumu ngumu.

7. Wahuni sio watu wazuri. Wamebomoa mali za machinga.

8. Wahuni wanapenda politoical violence and intimidations. Mwaka 2020 oktoba ni mwaka wa shetani na mwaka wahuni. Wahuni hawa wanapenda kutumia nguvu za dola kuanzisha vurugu, unyama na utesaji. Kama tulivyoshuhudia uhuni wakti wa kampeni hadi uchaguzi watu waliunguziwa nyuma, kupigwa na kuuawa. Wahuni hawakumalizwa bali walitengenezwa na kuwa wengi zaidi.

9. Wahuni hawapendi kuleta huduma za jamii hutumia pesa nyingi kujilinda na kukandamiza wengine. Wakati tunakaribia uchaguzi huona wahuni wakiagiza magari mengi ya washa washa kuliko magari ya Kuhudumia wagonjwa Ambulamce. Mwaka 2014 pekee yaliagizwa magari 700.

10. Kwa mara ya kwnza ktk bara la afrika wahuni walizima internet tanzania nzima na twitter tar 27 October. Wahuni hawapendi ukweli na uwazi. Matendo yao hupenda yafichwe yawe siri yasiongelewe.

11. Polepole wahuni mliwatengeneza sasa wamewageuka. Wewe na Bashiru ni miongoni mwa waathirika kutokana na vitendo vya wahuni.

Mnavuna mlichopanda. Na bado!!

wewe uliyea andika hii hoja wewe ndio muhuni namba moja yoote uliyoogea ni uongo mtupu mnajua sana propoganda
 
Back
Top Bottom