Hahahahah mifumo sindio hio imeuawa mzee! Tarura by cash, Tanesco nayo walitaka kuichezea watu wakaropoka sana wakakausha. Sahizi usishangae hii GePG nayo ikafa au waka hack mchongo hela ilawa inavuja mahali kabla ya kuingia hazina😅
Tanzania hata ije katiba mpya wahuni wataendelea kufanya yao na kulindana tu😅 sababu ni mchezo wameuzoea!
Kuua chain ndio njia pekee. Katiba ianishe kabisa watoto wa viongozi wastaafu hamna kushika senior positions waishie kwenye level za ukuu wa Idara tu huko incase wataingia serikalini moja kwa moja.
Yani aidha uraisi, ukurugenzi,uwaziri,ded,rc ama position yeyote ambayo wanakuwa final say wasiruhusiwe kufika kuwe na ukomo! Kama watafanya kwenye kampuni binafsi ni sawa hata wakiwa ma CEO!
Hii ndio itasaidia kuleta sura mpya kwenye system ya nchi. Sio baba kwa vile alikuwa raisi anafosi mazingira na mwanae awe raisi. Miaka nenda rudi itakuwa raisi Ally Hassan Mwinyi, Mtoto nae raisi Hussien Hassan Mwinyi, Mjukuu nae raisi Hassan Hussein Mwinyi! Style inakwenda kama vile nchi ya kifalme!