Nitamwachaje?

Nitamwachaje?

pisces

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2010
Posts
240
Reaction score
61
ndugu zangu, nimepata mpz miezi minne sasa, mwanzo nilimwamini but kadri siku zinavyozidi kwenda nashindwa kumwelewa. Namkuta na msg za kimapenzi na jamaa yake wa zamani, nikimuuliza sababu hazieleweki. Anapigiwa simu usiku wa manane na jamaa zake wa ofisini nikimuuliza anadai ni masuala ya kikazi. Aliomba chuo akajiendeleze tukajaribu apate hapa hapa dar but ikawa bahati mbaya kapata mkoani, nikahuzunika baby atakua mbali but yeye karurahia sana. Nilipomuhoji anadai anapenda kukaa mbalia na mimi ili anipe muda wa kujijenga kimaisha. Naanza kudhani ana uhusiano tena na mwanaume zaidi ya mmojakwa kuwa mara nyingi kuna simu akipigiwa hujing'ata ng'ata tu. Akili yangu inaniambia hanifai, ila je nitumie mbinu gani kuachana nae kabla sijapoteza muda mwingi zaidi. Nishaurini ndugu zangu.
 
Mega kwa mara ya msho kisha jigawe! Mwana haachwi kwakumkashifu au kumtusi,au kumpiga! Utashindwa kupata huduma siku ukikwama kaka, mwache kisport nae tena atafurahi!
 
miezi minne tu pole sana ..

duuhhh
kama uliyosema ni kweli basi
mtakuwa mnadanganyana..

mwambie tu ukweli ...( msipotezeane muda)
kama hamna future pamoja
haina maana kutokuambiana ukweli.......
unless mnatumia tu kwa sex...
 
Yani umemla uroda weeeeee,leo unataka kumuacha!
 
kama ulivyoamua kumtongoza ni kwaababu alikuvutia ila sasa amekutibua bas amua kumwaga
 
Utamwachaje?? kwani ulimuanzaje???
hata kama huwezi soma basi ielewe picha mtu wangu,, sioni unachosubiri hapo
 
Bado unasubiri nini hapo sasa? Ujasiri wako ndio utakuokowa na kifo au hujui kuna HIV na VVU!
 
Asikupotezee mwambia kua tabia yake na yako haziendani kwahiyo ajipange,na wewe usonge mbele na maisha utampata asiekupa Bp.
 
Amefurahia kwenda kusoma mbali na wewe kwa kudai kwamba atajijenga, baba ushakuwa kikwazo cha maendeleo ya mtu kimbia kama huna miguu ili mtu apandishe chati ya maisha.
 
Mwambie tu kwa lugha nyepesi kuwa tabia zake zimekushinda ashike njia aende tu.
 
Unamuogopa au?! Yaani ana tabia na mienendo usiyopenda halafu unashindwa kumwambia?! Sasa hapo unategemea una future naye?! Jifunze kuwa muwazi kwenye maisha yako ya mapenzi. Mwambie kwa ustaarabu kabisa kuwa huwezi kuendelea naye kwa sababu 1, 2, 3. Ila usimkashifu wala kumtukana kabisa.
 
post yako inaonyesha kuwa wewe na huyu binti mlishaanza kuishi kama mtu na mke maana unajua simu zake za usiku wa manane n.k.n.k. Ushauri yangu wa bure ni kuwa uwe makini sana.... miezi 4 ni michache sana sana kwa mwanamume aliye serious na maisha na hata anayejali afya yake, kuamua kuchukua uamuzi wa kulala na kuamka na mpenzi aliekutana nae miezi 4 tu iliyopita!!! kama umemchoka subiri akienda huko chuo cha mkoani iwe ndio byebye halfu next time ujifunze na uwe makini zaidi
 
Dah nimecheka kweli kwani kukaa mbalimbali ndio kuna mwezesha mtu kujipanga kimaisha?? mkuu hilo nalolinahitaji phd?
 
fanya maamuzi magumu, jivue gamba hilo kaka, asikupe shida huyo kuwa km simba mwituni, windo moja likiingia chaka jipange upya! anza na windo jingine lenye uhakika. ukiona mwanamke anafurahia kukaa mbali na wewe ujue mpo wengi hapo!
 
Back
Top Bottom