pisces
JF-Expert Member
- Dec 20, 2010
- 240
- 61
ndugu zangu, nimepata mpz miezi minne sasa, mwanzo nilimwamini but kadri siku zinavyozidi kwenda nashindwa kumwelewa. Namkuta na msg za kimapenzi na jamaa yake wa zamani, nikimuuliza sababu hazieleweki. Anapigiwa simu usiku wa manane na jamaa zake wa ofisini nikimuuliza anadai ni masuala ya kikazi. Aliomba chuo akajiendeleze tukajaribu apate hapa hapa dar but ikawa bahati mbaya kapata mkoani, nikahuzunika baby atakua mbali but yeye karurahia sana. Nilipomuhoji anadai anapenda kukaa mbalia na mimi ili anipe muda wa kujijenga kimaisha. Naanza kudhani ana uhusiano tena na mwanaume zaidi ya mmojakwa kuwa mara nyingi kuna simu akipigiwa hujing'ata ng'ata tu. Akili yangu inaniambia hanifai, ila je nitumie mbinu gani kuachana nae kabla sijapoteza muda mwingi zaidi. Nishaurini ndugu zangu.