Nitamwamini na kumuunga mkono Rais Samia atakapotatua suala la fao la kujitoa

Nitamwamini na kumuunga mkono Rais Samia atakapotatua suala la fao la kujitoa

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Sasa ni awamu ya 6 kwa mujibu wa Rais mwenyewe na serikali yake. Rais Samia Suluhu nitakuunga mkono kama utaondoa dhuluma hii kwa vijana.

Kumnyima kijana asichukue fedha yake kwenye mfuko wa kijamii mara baada ya ajira yake kukoma ni dhulma isiyovumilika.

Hebu vuta picha kijana aliyeajiriwa kwenye mradi na mradi ukaisha baada ya miaka 4 anaambiwa asubiri umri wa kustaafu ndipo apewe chake.

Je, thamani ya fedha husika leo italingana na miaka ijayo?

Sometimes wengine hupewa nusususu. Mara 30%, mara % ngapi itamsaidiaje kuondokana na umaskini?

Vijana wanaogopa kuacha kazi kwa sheria hizi za kinyonyaji.

Kama hii ni njia bora ya kuboresha maisha ya Watanzania kwanini wabunge ambao wengi ni over 40 wasichukue marupurupu yao ya kustaafu watakapotimiza miaka 60?

Kama hili Ni gumu, kwanini msipitishe sheria itakayoruhusu wabunge walioshindwa kuingia bunge linalofuta tu ndio wachukue fedha zao?

Kama Rais hatasolve hili nitamwona hana upendo na uzalendo kwa vijana zaidi ya maigizo tu yakumjenga na kumuimarisha kisiasa.
 
Ina maana kila baada ya ajira ya mkataba, utadai mafao yako? Leo miaka minne kampuni A... Then kampuni B miaka 6 n.k

Basi itakuwa ni mwendo wa kudai mafao kila baada ya mkataba kuisha!

Labda ungemwomba SSH aanzishe unemployment benefit ili wakati unatafuta ajira nyingine uwe na kadhaa za kukutosheleza kwa mwezi..
 
Rais Samia Suluhu nitakuunga mkono kama utaondoa dhuluma hii kwa vijana.
Kumnyima kijana asichukue fedha yake kwenye mfuko wa kijamii mara baada ya ajira yake kukoma ni dhulma isiyovumilika.
Mimi nitamuunga mkono akibadilisha katiba.
 
Ina maana kila baada ya ajira ya mkataba, utadai mafao yako? Leo miaka minne kampuni A... Then kampuni B miaka 6 n.k

Basi itakuwa ni mwendo wa kudai mafao kila baada ya mkataba kuisha!

Labda ungemwomba SSH aanzishe unemployment benefit ili wakati unatafuta ajira nyingine uwe na kadhaa za kukutosheleza kwa mwezi..
Is it wrong with that ?

Mbona wabunge wanachukua kila wakimaliza miaka 5.

Wakishachukua wanagombea tena.

Tena wanazoa pesa ambazo hata hawakuchangia huko kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
 
Is it wrong with that ?

Mbona wabunge wanachukua kila wakimaliza miaka 5.

Wakishachukua wanagombea tena.

Tena wanazoa pesa ambazo hata hawakuchangia huko kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
Wale ni wanasiasa na sio wafanyakazi..
 
Fao la kujitoa ni muhimu kwa vijana ,enzi za kikwete ndani ya wiki tatu unachukua mzigo wako ,alivyoingia "JIWE" akalizuia kwa tamaa zake za fedha na ndio lililochangia kupoteza mzunguko wa fedha mitaani.

Vijana wanaachishwa kazi halafu hawana mtaji mpaka wafikishe miaka 55 ndio wachukue mafao yao! yaani kijana wa kiaka 28 au 30 asubiri miaka 25 hadi 27 aje kupewa milioni nne aliyoidunduliza kwa miaka mitatu kwenye mifuko.
 
Ina maana kila baada ya ajira ya mkataba, utadai mafao yako? Leo miaka minne kampuni A... Then kampuni B miaka 6 n.k

Basi itakuwa ni mwendo wa kudai mafao kila baada ya mkataba kuisha!

Labda ungemwomba SSH aanzishe unemployment benefit ili wakati unatafuta ajira nyingine uwe na kadhaa za kukutosheleza kwa mwezi..
kwani shida iko wapi zile ni pesa za mfanyakazi. Si za mtu yeyote ni jasho la mtumishi.
 
Fao la kujitoa ni muhimu kwa vijana ,enzi za kikwete ndani ya wiki tatu unachukua mzigo wako ,alivyoingia "JIWE" akalizuia kwa tamaa zake za fedha na ndio lililochangia kupoteza mzunguko wa fedha mitaani...vijana wanaachishwa kazi halafu hawana mtaji mpaka wafikishe miaka 55 ndio wachukue mafao yao! yaani kijana wa kiaka 28 au 30 asubiri miaka 25 hadi 27 aje kupewa milioni nne aliyoidunduliza kwa miaka mitatu kwenye mifuko.
Kwakweli hii akili ya viongozi wetu wanaijua wenyewe
 
Ina maana kila baada ya ajira ya mkataba, utadai mafao yako? Leo miaka minne kampuni A... Then kampuni B miaka 6 n.k

Basi itakuwa ni mwendo wa kudai mafao kila baada ya mkataba kuisha!

Labda ungemwomba SSH aanzishe unemployment benefit ili wakati unatafuta ajira nyingine uwe na kadhaa za kukutosheleza kwa mwezi..

Hata kuidai kila baada ya mwezi si ya kwako? Watunga sheria wenyewe wakimaliza tu miaka mitano wanachukua fao lao mbona hawaachi? Mtu analipwa mil 12 na mikopo hadi milioni 800 halafu yeye kajitungia sheria achukue fao lake kila mkataba wake ukiisha ila wavuja jasho wanaolipwa hela ya kula tu wamewatungia sheria wasichukue mafao yao mpaka wafikishe miaka 55.
 
Hata kuidai kila baada ya mwezi si ya kwako? Watunga sheria wenyewe wakimaliza tu miaka mitano wanachukua fao lao mbona hawaachi? Mtu analipwa mil 12 na mikopo hadi milioni 800 halafu yeye kajitungia sheria chukue fao lake kila mkataba wake ukiisha ila wavuja jasho wanaolipwa hela ya kula tu wamewatungia sheria wasichukue mafao yao mpaka wafikishe miaka 55.
CCM imejaa watu wa hovyo sn
 
Ina maana kila baada ya ajira ya mkataba, utadai mafao yako? Leo miaka minne kampuni A... Then kampuni B miaka 6 n.k

Basi itakuwa ni mwendo wa kudai mafao kila baada ya mkataba kuisha!

Labda ungemwomba SSH aanzishe unemployment benefit ili wakati unatafuta ajira nyingine uwe na kadhaa za kukutosheleza kwa mwezi..
Hujawahi kuajiriwa sekta binafsi wewe.
 
Back
Top Bottom