Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,015
- 2,493
Salaam wanaJF.
Kauli ya Kada wa Chadema, Mdude Nyangali kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anatafuta roho yake ni kauli nzito mno isiyotakiwa kupuuzwa hata kidogo na vyombo vya ulinzi na usalama.
Mdude amesema straight bila kumung'unya maneno kwamba Samia anataka atekwe, ateswe, auawe na kutupwa kama ilivyokuwa kwa Mzee Ally Kibao huko Ununio jijini Dar es salaam.
Kwamba Mdude ameuambia dunia kwamba Rais Samia Suluhu Hassan anaua raia wake. Inafikirisha sana. Ni vizuri Jeshi la Polisi limkamate Mdude na kumfikisha kortini athibitishie dunia ile ile kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ni muuaji. Tuhuma hii ni nzito mno.
Ikumbukwe kwamba endapo kutakuwepo na ukweli katika tuhuma hii basi Samia anaweza kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC ya nchini Uholanzi kujibu mashtaka ya kuua raia wake aliyoapa kuwalinda.
Polisi kazi kwenu. Simamieni sheria. Hii haiwezi kuwa kesi ya kubumba. Ameandika barua ya wazi kwa umma. Kila mtu amesoma dunia nzima.