Uchaguzi 2020 Nitashangaa Wafanyabiashara kumnyima Magufuli kura

Uchaguzi 2020 Nitashangaa Wafanyabiashara kumnyima Magufuli kura

Na kila ukikumbuka biashara zilivyodorora, Mafrem yalivyofungwa kila mahali, TRA wanavyotupia kodi za ajabu na umati wa raia waliokuwa wanunuzi wa biashara hizo kukosa hela (uwezo) wa kununua tena biashara unajisikiaje kuhusu shaka na utimamu wake mkuu?
wafanyabiashara wa Dar badala ya kwenda china kufuata bidhaa sasaiv wanaenda Kampala, yaan baada ya kuyumba kimtaji
 
Umetumwa kupima upepo? Kamwambieni huyo kibwengo wenu kuwa HATUMTAKI. Na nawakilisha wafanyabiashara 90+% wadogo (SMEs) wa nchi hii.
Sector binafsi imekuwa domant, vitisho,kodi isiyo na uiano, uhakiki kodi miaka ya nyuma,wengi wamepoteza ajira na ajira mpya chache. Wengi wanafanya unafiki bendera ccm, biashara kushuka wengi wamefilisika,madeni bank nk...wengi watainyima kura ccm.
 
Wafanyabiashara ni watu smart hawewezi kuchugua ile mihemuko ya ubeligiji
 
Hawa hawa wafanyabiashara ambao njia za kuingia katika maduka yao wamewekwa machinga kwa kitambulisho cha elf ishirini?
 
Mbona mnatuchanganya?!

Hao wafanyabiashara Kwani siyo sehemu ya taasisi binafsi zilizompongeza anko Magu juzi kati kwa kufikia uchumi wa kati?

Kama ndivyo kwanini wasimuunge mkono kwa kumpa kura za ndiyo?!
 
Hali mbaya mgombea anaombewa kura,kajenga sgr ya kifisadi, kanunua ndege kifisadi ila anahemea ventilator machine. Watanzania hawamtaki
 
Usiwe na house. Wafanyabiashara wote wanakwebda kumchagua Dkt Magufuli kwa kura nyingi. Wanajua mazuri waliyofanyiwa na Rais huyu mpenda maendeleo.

Kama wewe ni kufanyabiashara ungana na kundi la ushindi kwa kumpa kura yako Dkt Magufuli,. Tafadhali chagua maendeleo ya biashara yako.
 
Mimi ni victim wa hilo ninalosema hadi leo hii, lipo kwenye baraza la kodi, tunavutana!! Licha ya punguzo kubwa walilopunguza bado halikubariki!! Mwishowe imekuwa kama biashara 'sasa unasemaje unataka kulipa ngapi' 'mtu ana kuta ana deni eti la bilioni tatu!!! Hahaaa, kuna maneno aliyasema zitto japo ni makali ila ndio ukweli, GENGE LA WAPORAJI
Kashtaki, una haki hiyo. Huo ni uonevu wa wazi. 15 years back?
 
Kila nikikumbuka miaka ya nyuma nilivyokuwa napata pesa nyingi kwenye mzunguko wa biashara zangu.halafu kuanzia 2016 tu mambo yamekuwa mabaya.sitaki hata kumsikia Magufuri.. Mimi sio mpiga dili wala nini.nafanya biashara zilezile za halali..
 
Nenda segerea utashangaa zaidi kukuta wafanyabiashara kule wakisota.ukimaliza urudi utuambie Kura za wafanyabiashara apewe Nani .
Kwani wamekamatwa na shria au na rais wewe vipi! Zamani watu wenye pesa mliwasema kuwa hawtii sheria na hawafungwi kwa sababu wana pesa iweje leo unalalamika. Kwa akili zako watu wenye pesa ni waovu sana mfano: mfanyabiashara el chapo wewe unavyoonekana ungekuwa rais ungemwacha bila kujali madhara ya biashara yake.
 
Nitawashangaa sana wafanyabiashara na watumishi wa serikali wa kada mbalimbali watakaompigia kura mtu aliyewakandamiza kwa miaka mitano mfululizo
 
Nazungumzia kipindi cha korona kwani mlizuiliwa kufanya biashara.
Inshu hapo sio kuziiliwa kufanya biashara, miaka mitano misingi ya uendeshaji biashara umeuawa, bila hata janga la corona, sembuse uongeze corona??!! Ni mfanyabiashara gani aliyepata hata faida kidogo kipindi cha corona?

Bora hata nchi nyingine mfano RWANDA, kuna kodi ziliondolewa huyo eti rais wa wanyonge, Kodi za pango zilibakia pale pale, TRA, bill za maji, umeme, uzoaji taka, leseni.

Ingekuwa na huruma si wangesema hata kodi ya mapato kwa miezi walau sita, isamehewe?!! Usiongee kama kiumbe asiyekuwa na kichwa bwana!!! Unatonesha vidonda vya watu!! Kila kitu mnakifanya siasa, MPAMBE UNA PAMBA HADI BOSI ANACHUKIA!!!
 
Wale waliokesha mitandaoni wanaomba ajira hewa za ualimu unadhani watampa kura nani??Biashara mtaani ni vumbi tupu people have no money anymore.
 
Kama wafanyabiashara wangekuwa ndio wao pekee wanapiga kura, Jiwe kabla hata hajaamka, angekuwa kesha safirishwa Chato
 
Kila nikikumbuka maamuzi magumu ya Rais Magufuli kuhusu Corona, sina shaka na utimamu wake na ujasiri...
Magufuli hakuzuia corona acha kumpa ujiko na sifa bure, Kilichosaidia corona Tanzania ni bidii ya watanzania kunywa Tangawizi Limau vitamini C kupiga Nyungu kwa Pamoja tena kwa bidii kubwa na uzuri Limau ni fresh na Tangawizi ni fresh zinapatikana Tanzania, hii ndiyo imeisaidia Tanzania siyo magufuli, acheni kumsifia uongo kwani kama siyo bidii binafsi za watanzania kungekuwa na maafa kama kenya na South Africa
 
Back
Top Bottom