Uchaguzi 2020 Nitashangaa Wafanyabiashara kumnyima Magufuli kura

Uchaguzi 2020 Nitashangaa Wafanyabiashara kumnyima Magufuli kura

Wafanyabiashara wanahasira na mgombea kutoka ubeligiji ambaye anataka kuwaribia mfumo wao wa kufanya biashara
BOT imewapora pesa zao nyingi walizotumiwa toka nje ndiyo maana wengi wamehamishia pesa zao Uganda Zambia kenya ambapo Benk kuu za huko hazina mambo ya hovyo kama BOT, wengi wamebambikiwa kodi TRA wakapewa kesi za uhujumu uchumi na wengine wamefirisiwa hakuna mfanyabiashara mkubwa hata wa kawaida anataka kuisikia CCM, wanaichukia mno
 
Kama wafanyabiashara wangekuwa ndio wao pekee wanapiga kura, Jiwe kabla hata hajaamka, angekuwa kesha safirishwa Chato
Hakuna mfanyabiashara anaipenda CCM hata mmoja wote wanataka CCM ifutwe kwenye ramani za siasa ya Tanzania
 
Uchumi upi unaozungumzia? Tuanzie hapo.
nikikumbuka maamuzi magumu ya Rais Magufuli kuhusu Corona, sina shaka na utimamu wake na ujasiri.


Kwa kipindi kama kile ambacho nchi nyingi ziliamua kufunga biashara na shughuli nyingi za kiuchumi, mtu huyu aliamua kwamba wafanyabiashara waendelee na biashara zao na shughuli nyingine ziendelee.

Hakuna biashara iliyofungwa, lakini watanzania hawana shukrani wanasahau yote kisa mtu ambaye kwa ninavyomtazama mlengo wake si wa kimisimamo binafsi bali ya kuongozwa na anaowaamini.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Magufuli anastaili kukamilisha kipindi cha miaka 10, uongozi si wa kubadilisha kama nguo. Tukipata kiongozi mzuri basi tumuache amalize awamu zote mbili.
 
Tena msitukumbushe machungu wafanyabiashara hatuwezi kumchagua huyo jamaa ametuumiza sana.
BOT imewapora pesa nyingi walizotumiwa toka nje ya Nchi na walipojaribu kupiga kelele wakawatishia kuwabambikia kesi za uhujumu uchumi utakatishaji fedha na mengineyo ya hovyo, Utawala huu umewatesa wafanyabiashara mno hata wale wamiliki wa maduka ya kubadili pesa za kigeni ndiyo wanamchukia magufuli kupita kiwango baada ya kuwa wameporwa pesa zao na BOT kwa njia haramu za kishetani wakati walikuwa na mikopo na mali zao kuuzwa na mabenk
 
"Mlo moja pia umekuwa ni Shida kwa Watanzania" Sheikh Ponda Issa Ponda
 
Uchumi upi unaozungumzia? Tuanzie hapo.
Uchumi haukui tena kwa sababu wafanyabiashara wote wakubwa hawaweki pesa zao Tanzania kwa hofu ya usumbufu wa BOT waliopewa Amri na mtukufu magufuli kuwasumbua wafanyabiashara wakubwa
 
Sector binafsi imekuwa domant, vitisho,kodi isiyo na uiano, uhakiki kodi miaka ya nyuma,wengi wamepoteza ajira na ajira mpya chache. Wengi wanafanya unafiki bendera ccm, biashara kushuka wengi wamefilisika,madeni bank nk...wengi watainyima kura ccm.
Hakuna mfanyabiashara mwenye Akili timamu anaweza kuipigia CCM kura
 
Kila nikikumbuka miaka ya nyuma nilivyokuwa napata pesa nyingi kwenye mzunguko wa biashara zangu.halafu kuanzia 2016 tu mambo yamekuwa mabaya.sitaki hata kumsikia Magufuri.. Mimi sio mpiga dili wala nini.nafanya biashara zilezile za halali..
Mpiga dili ni CCM yenyewe sasa ndiyo maana wametafuna trilion 1.5 wakamtoa CAG kafara Ndungai akapiga dili bilion 12 akiwa India peke yake, wafanyabiashara wanataabika kuteseka tu kwa uonevu unyanyasaji wa mtukufu magufuli na watu wake
 
Kila nikikumbuka maamuzi magumu ya Rais Magufuli kuhusu Corona, sina shaka na utimamu wake na ujasiri..
Kama wewe si mfanyabiashara bora ukae kimya,katika watu wenye uchungu na awamu ya tano basi ni wafanyabiashara ambao awamu hii wameteseka sana,awamu hii watu wamefirisika na kufirisiwa hovyo.

Awamu hii sheria zinabadilishwa hovyo kiasi ambacho kilichohalali leo kesho kinaharamishwa,hili limepelekea wafanyabiashara kuishi kwa mashaka kwani hawajui kesho kutaamka na kipi.

Nakukumbusha yule mfanyabiashara aliyejipiga risasi dodoma baada yakukutwa na kutaifishiwa pombe aina ya viroba yenye thamani zaidi ya mil500 ambayo kabla ilikua halali na gafla ikawa haramu.

Huu utawala umeumiza sana watu hasa wafanyabiashara.
 
Wakulima, watumishi wa umma, wafanyabiashara, wavuvi, vyeti feki, nk wote watampigia
 
Wafanyabiashara ninaowajua mimi wa type ya Kariakoo hawawezi kumchagua JPM wameshachoshwa. Wengi wao wapo hoi wanaomba amalize muda aondoke maisha yaendelee TRA kwao ni kama mtoa roho!!
 
Kama wewe si mfanya biashara bora ukae kimya,katika watu wenye uchungu na awamu ya tano basi ni wafanyabiashara ambao awamu hii wameteseka sana,awamu hii watu wamefirisika na kufirisiwa hovyo...
BOT imewapora pesa zao walizotumiwa toka nje huku wakiwatishia kuwabambikia kesi za utakatishaji fedha, wafanyabiashara wa Tanzania wanaongoza kwa kumchukia Rais kuliko wafanyabiashara wote Duniani
 
Wafanyabiashara ninaowajua mimi wa type ya Kariakoo hawawezi kumchagua JPM wameshachoshwa. Wengi wao wapo hoi wanaomba amalize muda aondoke maisha yaendelee TRA kwao ni kama mtoa roho!!
Wengine walipewa pesa tokea nje lakini BOT imewapora kwa njia haramu za kishetani, kwa kifupi utawala huu ni utawala Hatari kwa usitawi wa wafanyabiashara wote
 
Kwahio umeona corona tu hio hoja moja ndio mnataka kujificha nayo kwenye mwamvul wa umasikini wa Tanzania ?
 
Back
Top Bottom