Utakuwa kiongozi mjinga kama utang'ang'ania kuwa unasimamia sheria za kodi halafu kila siku biashara zinafungwa na uwekezaji unaanguka.
Kama unayoyasema ni kweli, basi alitakiwa ufanye detailed study ya kujua kodi inayolipika, halatu ndiyo hiyo usimamie kikamilifu.
Ghana VAT 5%, Tanzania 18%! Marekani VAT 0%. Sasa utakaposimamia kikamilifu VAT ya 18% tena kwa sasa katika utekelezaji wameingiza kila kitu wakati sheria haisemi hivyo, ni lazima utaua biashara.
Kitakachoongeza pato la serikali na ajira ni kuongezeka kwa biashara na uwekezaji. Biashara zinasinyaa, ukuaji wa uwekezaji unaanguka, wewe unafurahia na kusema, mimi nasimamia sheria ya kodi, wewe utakuwa ni kiongozi mwenye akili?
Biashara na uwekezaji vikiisha, hiyo sheria utaenda kusimamia majumbani kwa watu? Kiongozi mzuri ni yule mwenye kuona athari kabla ya kutokea.
Sent using
Jamii Forums mobile app