Wengi waliofunga biashara zao sababu ya kodi ukikaa watakuambia ukweli walovyokuwa wakikwepa kodi kwa kutoa rushwa. Mfumo ulipoanza kufanya kazi sawasawa wamejikuta na mzigo mkubwa wa kurudisha biashara kwenye ukweli. Kumbuka hapa Ile chain yote inatakiwa kufuata utaratibu kwa sasa kitu ambacho kimepeleka mzigo mkubwa kwa mfanya biasha aliyekua akilipa kodi ya pango 1.5m kwa frame moja ambayo hiyo kodi pia haikua sawa.
Wenye frames za biashara nao wanalia imebidi wakubali kushusha bei baada ya wateja kushindwa. Ungewashauri kufanya restructuring, wapunguze gharama za uendeshaji wa biashara tuu ili kuendana na ukweli maana hamna namna ya kumkwepa kaisari
Kuna waliowahi wakakimbia nchi kabisa kuukwepa mkono wa sheria kwa kujua makosa yao, kuna kampuni ambazo zimetelekezwa na kufungwa kwa kukosa wamiliki, Walio segerea uchunguzi ukikamilika watapata haki zao
Kweli biashara zimedorora ila kuna maswali mengi ya kujiuliza hapo.
Na sio biashara za bidhaa tuu zilizodorora hata za huduma pia. Wapo waliokua wanafanya biashara za nyumba kupangisha wanalia, wapo waliokua wanauza ardhi viwanja na mashamba wanalia pia, wauza nyumba nao hivyohivyo.
Tulikua kwenye ulimwengu ambao sheria zipo lakini hazikua zikifuatwa, vyombo husika havikua vikifanya kazi zake inavyotakiwa.
Kama kwenye biashara ardhi valuers wametuingiza mkenge kwa kushindwa kuweka na kusimamia bei elekezi matokeo yake ni hizi stress tunazopitia sasa Mtu nilinunua eneo 2014 kwa 20M leo nina shida siwezi kuliuza japo kwa nusu bei. Wenye mali wanalia, taasisi za fedha wanalia ila yote ni sababu mfumo ulikua mbovu regulators hawakua wakifanya kazi zao kwa weledi
Tulikua na uchumi wa ajabu sana ambao umevurugika sasa, hakuna asiyeumia na haya mabadiliko hata tanzania ila hakuna namna
Wote tunapata maumivu ya mabadiliko lakini ni mabadiliko yenye heri
Mjep cocochanel Kawe Alumni Bia yetu Themagufulianz BUSH BIN LADEN mugah di mathew tameer IDEGENDA NAWATAFUNA Msengapavi Next Man Nguseroh minyoo Wakudadavuwa
stakehigh Daby Erythrocyte
Extrovert
GENTAMYCINE