Uchaguzi 2020 Nitashangaa Wafanyabiashara kumnyima Magufuli kura

Hawa hawa ambao waliambiwa wanatakiwa kuishi kama mashetani au kuna wengine?
 
Magufuli babalao kwa kweli
Wahenga walisema yenye uchungu ndio tiba.
 
Na kibaya zaidi watekekelezaji Sheria huingiza tamaa zao humo ikiwemo kusaka Rushwa uonevu kuwakomoa watu na mambo mengineyo mengi ya hovyo
 
Hawa hawa ambao waliambiwa wanatakiwa kuishi kama mashetani au kuna wengine?
Ni kweli sasa wanaishi kama mashetani ndiyo maana wafanyabiashara wakubwa wamehamia Uganda Zambia kenya baada ya BOT nayo kuwa inawapora pesa zao wanazotumiwa toka nje kisha kuwatishia kuwabambikia kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi
 
Wenye mamlaka wanatumia fursa hii chini ya udikiteta kuwapora wafanyabiashara mali zao kwa visingizio vya kudaiwa kodi zisizo na Maelezo ya kueleweka, hakuna mfanyabiashara anaipenda CCM tokea moyoni bali wengi huzuga Usomi tu ili kulinda mali zao wasije kubambikiwa kesi
 


Wahenga walisema - Yenye uchungu ndio tiba
Tuvumilie tuu
 
Sababu pekee ni mapato/kodi yake yasiathirike na sio kuwajali wafanyabiashara,wafanyabiashara wameteseka kwenye awamu hii kwa kubambikizwa makesi ili mali zao zichukulie, kubambikizwa makodi,na wengi walifilisika na kufunga biashara zao,labda kama unaongelea nchi nyingine sio tanzania
 
Wafanyabiashara wakubwa na wadogo wametaabika wameteseka mno kwenye utawala huu hata BOT imewatesa mno kwa kuwapora pesa zao pindi wakitumiwa tokea nje ya Nchi na ikitokea mfanyabiashara akapiga kelele humtishia kumbambikia kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha
 
Kabisa, huyu mtoa mada atakuwa anaongelea tanzania ya ulaya labda,au katumwa kuja kuandika huu upuuzi
 

Ukiniambia Mbona USA wana VAT 0%
Na Mimi ntakuuliza
Mbona Russia wana VAT 18% japo kwenye Children goods,Medication na medicines imepunguzwa
Mbona UK wana VAT 20% as Standard VAT with other VAT rates 10% na 5% kwenye baadhi ya bidhaa na huduma nyingine
Na China wanayo 16%

Na Hayo yote ni mataifa makubwa yanayo jitosheleza Kwenye kila kitu

Kwanini ushangae Sisi Tanzania kuwa na VAT ya 18% Kwenye bidhaa na huduma isipokua 0% VAT rates Kwenye exportation
ikiwa Sisi ni Nchi changa Sana (imagine Jiwe ni Raisi wa 5)
Serikali itapata Wapi pesa za kujenga Miundombinu afya, barabara, shule nk kwa wananchi wake ?
Hatuwezi kujifananisha na Marekani mkuu
Huko Kwenye VAT ndogo hatujafika bado

Ni biashara gani hizo zinazokufa Mbona unaziona wewe tuu ni Tathmini yako Binafsi siwez kukuzuia kusema
Lakini ukumbuke biashara kufa ina factors nyingi sana Ushindani, Eneo baya, mtaji mdogo, kufirisika na nk hizi zote zina ua biashara

Hivyo Sio kila biashara inayokufa ni Magufuli kaua ,HAPANA
 
Wafanyabiashara wadogo(machinga,mamantilie) walipigwa elfu 20,kama rushwa, ili wasisumbuliwe na mgambo!
 
Tatizo la Tanzania wala sio hizo kodi,sijui VAT n.k. Tatizo ni mfumo wetu wa kufikia kiasi na namna ya kulipa.

Kwanza, hujaanza hata biashara unalipa kodi. Yaani kodi inabidi uiweke kabla hata hujapata hiyo faida. Ukisajili kampuni tayari unalipa kodi.

Pili,kodi zetu bado zipo kwenye makadirio. Sasa hii unaweza ukasusa mzigo pale bandarini.Unaagiza watu wanaanza kukupa makadirio makubwa kuliko uhalisia.

Mfumo ungekuwa mzuri, kodi watu wangelipa fasta tu.
 
Huyo alieandika mada hii ana utimamu wa akili au ndio kuamua kutumika ??, mfanyabiashara/mkulima/mfanyakazi/ atakayempigia kura magufuri atathibitisha mwenyewe kuwa na mtindio wa ubongo, watu wamefilisiwa mali walizokuwa wamechuma kwa jasho kwa kubambikwa makesi eti uhujumu wa uchumi
 

Hii ni kweli kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…