Kwenye nchi moja bila kujali itikadi za siasa, dini wala kanda zetu lazima wote tukubaliane katika vitu vya msingi ambavyo havina haja ya kuhojiwa maana hivyo ni vya kwenu wote na nilazima vibaki hivyohivyo hata kama wewe huvipendi. Tanzania kuna vitu ambavyo woooote lazima tuvienzi kama vilivyo bila kubadilisha nukta. Vitu hivyo ni kama vile dini zetu, wimbo wa taifa, kiswahili, bendera, muungano na mipaka yetu ya nchi. Kila mtu bila kujali itikadi yake lazima avivumilie kama vilivyo hata kama havipendi. Mtu anapopanda jukwaa la kisiasa na kuanza kuhoji muungano, dini za watu, wimbo wa taifa, makabila au mipaka ya nchi yetu hatakiwi kuitawala nchi hii na itamchukuwa muda mrefu kufanikiwa kuitawala nchi hii. Wazee wetu kuna vitu vingi wamevipatia na kuvikosea kwaajili yetu kama vile wazazi wetu walivyokosea na kupatia katika kutupatia majina yetu. Aliyesema nchi yetu iitwe Tanzania alifanya hivyo kwa niaba yetu, hatutakiwi kumlaumu. Hata wazungu tunaosema wameendeleaa kuna vitu vilivyokosewa hawavihoji wala kuruhusiwa kuvihoji. Waingereza kuna watu wangependa kuhoji kwanini familia moja tu ya kifalme ndio inakula keki kubwa ya nchi milele, lakini hawana nafasi ya kuhoji, kule marekani kuna watu wanaohoji kuhusu majimbo yao hasa inapofika wakati wa uchaguzi wa marekani lakini watu hao hawapewi nafasi ya kuhoji maana babu zao walishaamua iwe hivyo kwa niaba yao na wajao.
Kitu cha msingi kinachowachelewesha vyama vya upinzani nchini kuingia Ikulu ni kuhoji Muungano wetu kila wanapopata nafasi ya kupanda jukwaani, ni kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali kinachowaudhi baadhi ya wananchi, hii husababisha nchi yetu ibaki nyuma kwenye maeneo fulani. Mfano, wapinzani wanatafuta kura kwa kupinga machinga wasiondolewe barabani na kwenye mitaro, wanapinga barabara kutanuliwa, wanapinga wamasai kuhamishiwa sehemu nyingine ili kupisha wanyama, watu kuhamishwa mabondeni, wanapinga ubinafsishwaji wa bandari, wanapinga bomba la gesi na mafuta visijengwe, wanapinga kila kitu kama mtaji wao wa kupata kura. CCM nao kwa kuogopa kukosa kura za hao watu wanaamua kuacha kuwapanga bodaboda, machinga, nk