Maandamano hayasaidii, yanazidi kumpa sifa Mama kimataifa katika duru za demokrasia, kwakuwa inafahamika wazi dunia nzima kuwa:
1. mama amepokea kijitti kutoka kwa mtangulizi ambae alikuwa "dikteta" wa demokrasia. Sasa kuna nafuu kubwa kuliko huko nyuma.
2. Ughali wa maisha uko dunia nzima, ikiwemo Marekani.
3. Nchi imetulia, amani imetamalaki, hakuna hata sisiminzi anaepoteza uhai wake kwasababu ya siasa.
4. Vita vya Ukraine, Gaza, DRC, Sudan, Somalia, Ethiopia, Afrika ya kati na kule Niger, Burkina faso na Mali vinafuta malalamiko yote ya tz kuonekana kuna tatizo.
5. Inafahamika kuwa vyama vya upinzani vimejaa wahuni; waunga juhudi za chama tawala, walafi na money mongers. yaani wanatumia wananchi kisiasa kujipatia mahekalu, mahoteli, mashamba, magari makubwa na kusomesha watoto wao ng'ambo. Hapa tunazungumzia vyama vya upinzani kuwa na watu kama akina nassari, tumbili, akina Mdee, sugu, lema, sumaye, Slaa, Lipumba; Lowasa, Mrema, na Membe (RIP) na wengine wengi ambao wapenda mageuzi waliwaamini na kuwapa kura zao lakini hatimaye wakarudi na kwenda CCM na wengine kujenga vitega uchumi vyao binafsi badala ya kuimarisha vyama vya upinzani nchini.
6. Hawana hoja za msingi na zinazoeleweka za kulisogeza taifa mbele, ni watu wa matukio tu.
7, Waapinzani walihusika na kuvuruga mchakato wa kupata katiba mpya yenye afadhali kuliko iliyopo kwa kung'ang'ana na aina ya muungano kwenye katiba.
Wapinzani wanayo kazi kubwa ya kufanya kurejesha upinzani pahala pake. Mimi binafsi sijui nani kama nikimchangua hataenda CCM kuunga juhudi za mwenyekiti. Ni heri wananchi wote twende bure wenyewe tukaunge juhudi za Rais kuliko kumchangua mtu ambae atakwenda kuunga juhudi za rais kwa kupewa pesa nyingi.