Haya tuambie UN watafanya nini kwenye jambo lenu? Yaani UN iache kuhangaika na Gaza, Ukraine, Sudan, DR Congo, Somalia, Libya, Iraq, N. Korea, Burundi, Ethiopia, Yemeni, Sahara, Niger, Mali, Burkina Faso, na kwingine wanakopigana wahangaike na watu wanaolala na wake zao vitandani mwao? Wahangaike na watu wanaoshiba, wanaotibiwa, watoto wao wanakwenda shule, barabara zinajengwa, mabwana ya umeme yanakamilika, watalii wanafurika, mameli makubwa yanatia nanga kwenye taifa, kilimo kinakwenda vizuri na timu nyingine zinachezea mechi zao kwenye nchi ya Tanzania kutoka na amani iliyoko. Unadhani UN ni wajinga kama nyinyi? Haya mmeshapeleka ujumbe wenu UN tusiwasikie tena maana mmeanzia UN (kubwa zaidi) kesho mtasema mnapeleka wapi maandamano? Ni heri mngeanzia kwa mjumbe wa nyumba 10, kesho serikali ya mtaa, kesho kutwa kwa mtendaji kata, mtondogo kwa katibu tarafa, wilaya, mkoa, EAC, Sadc, hadi UN. Mazuzu nyie, no plan, Sasa hivi mmewapa sababu ya kuwapiga kama mkiandamana maana hata UN haitawatetea tena.