NITASIKITIKA NA KULAANI NIKISIKIA TARURA WAMEREJESHA MABILIONI WAKATI KWETU NJIA MBOVU.

NITASIKITIKA NA KULAANI NIKISIKIA TARURA WAMEREJESHA MABILIONI WAKATI KWETU NJIA MBOVU.

ofisa

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2011
Posts
4,340
Reaction score
4,069
Nimekuwa nafuatilia ripot ya CAG na tunasikia fedha zinarudishwa kwa kukosa matumizi.
Ikiwa imebaki miezi miwili naomba wahusika kuanzia serikali yangu ya mtaa wa bomba la mafuta kingolwira,CCM,Diwani wangu, mbunge wangu wa Morogoro na mamlaka ya TARURA.
Nimewataja hao wote ili washirikiane kwa pamoja bila kuogopana kwani Mama aliahidi barabara za changalawe zinazopitika msimu wote lakini hicho kieneo chetu na dongo lake lilivyobaya linahitaji haswa barabara isiyoyumbishwa na mvua.
Barabara tulizonazo ni mbovu hazitamaniki na Diwani wetu yupo tu,mwezie wa mafiga anajenga hoja amepitishiwa lami kila upande yaani ndani ya mita 500 kuna lami kila upande na stand. sisi huku ni tope na utelezi tu.plus mashimo ma kongoro.CCM kama mnatupenda kingolwira basi wakemeeni viongozi wenu mliowaweka warejee kwenye mstari kwani mvua ikinyesha ni hofu tunafikaje makazini kwetu.
Nimesema mapema nisije sikia fedha zimetumika mpaka zinarudi .Tarura nawaomba sana salio litakalo baki au mnaloona linabaki basi njooni mwage kifusi tu ili tuweze kupita hatuhitaji lami ni kifusi sahihi cha kutufanya tusijute kujenga mikoani.
Inafika wakati tunajiuliza na kujilaumu kwa nini tunajenga mikoani badala ya kupanga tu mjini.tunajilaumu tunatumia mafuta mengi na kufanya tulipe kodi nyingi za mafuta,
Tunajilaumu kwa nini tumejenga halafu hatupati maji,tunajilaumu hakuna hata patrol ya polisi kulinda mali zetu,tunajilaumu hakuna serikali ya mtaa mpaka utembee kilometa 3.na mwenyekiti hatujui watu wake.
 
Back
Top Bottom