Nitasimama na SIMBA yangu daima

Nitasimama na SIMBA yangu daima

Kipofu kaona mwezi leo mtaani hapatoshi
FB_IMG_1699204689107.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilijitambua kuwa mimi ni SIMBA mwaka 1982, almost miaka 41 hivi iliyopita.. Ni shabiki kindakindaki wa SIMBA sports club .. Mimi si shabiki maandazi
SIMBA ni timu kubwa sana Tanzania, Afrika na duniani kote.. Simba imekuwa role model kwa timu nyingi kwa mengi mazuri iliyoyafanya.. Ina mafanikio mengi kitaifa na kimataifa. Inaheshimika na kutambulika sana kuliko hata mpinzani wetu.. Ni mojawapo ya timu maarufu popote uendapo
Kwa sifa zote hizo
Kwa mafanikio yote hayo
Kwa ukongwe wote huo
Kwa umaarufu wote huo.. Nitaanzaje kuichukia timu yangu hii kwa changamoto ndogo ndogo za kupita?

Kwenye maisha kuna kupata na kuna kukosa
Kuna nyakati za mafanikio na kuna nyakati za maanguko
Kuna nyakati za furaha na kuna nyakati za huzuni pia

SIMBA tunapitia kipindi kigumu lakini si kama maadui zetu wanavyoaminisha watu mitandaoni.. Ni changamoto za muda hazitakuwepo milele.. Ni nyakati za nzige.. Tunazitafakari...hatukati tamaa tunapambana tutazishinda na kuwa imara zaidi.. Washindi zaidi wakubwa zaidi na zaidi

Soka lina matokeo matatu
Kushinda
Kushindwa
Kutoa suluhu
Kwasasa sisi ni washindwa wa muda.. Tunaachia nafasi za furaha kwa wengine wanaokua.. Ni muhimu kufanya hivi pia.. Huwezi kuwa mshindi daima .. Maisha yana pande mbili nasi kwasasa tuko upande wa pili

Acha kwasasa adui afurahi lakini hili nalo litapita kama mengine yote yalivyopita
Viva SIMBA.... Viva Forever.[emoji173]View attachment 2525426

Kwa kweli!
 
Makolo kwisha habari yenu, we si unajifanya mganga humu haya yaroge matokeo yabadilike, kolo wahedi wewe
 
Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA leo limetaja timu ambazo zipo katika nafasi ya kuweza kuwania kucheza fainali za kombe la Dunia kwa vilabu 2025.

Tanzania na Afrika Mashariki ni Simba SC pekee ndio imekidhi vigezo vya kuwa katika timu 12 zenye nafasi ya kupambana kwenye mchujo huo.

Mfumo mpya wa Kombe la Dunia la Vilabu utahusisha jumla ya timu 32 kutoka mabara yote kwa Afrika ni timu nne pekee ndio zitafuzu kati ya 12 zilizotajwa na FIFA.
#MillardAyoUPDATES
20231228_052725.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom