Wananchi na Wanachama wote huku kwangu wanamuunga mkono sana Tundu Lissu,
Wameniambia kama sitamchagua Lissu basi wao hawatakuwa tayari kuendelea na Ujenzi wa Chama,
Lakini kwenye huu Uchaguzi Mimi sipigi kura peke yangu nafanyaje?
Basi kama Mbowe atashinda Mimi nitajiunga tu na CCM Kwa sababu Sina Cha kuwaeleza hawa wajumbe.
ROHO INAUMIA SANA.
Dalili mbaya imeonekana Bawacha .
Mbowe akishinda chama kutakuwepo lakini kitakua kama CUF ,NCCR na UDP.
Wananchi kwa kweli na viongozi wa chini hawatakua na uwezo wa kukabiliana na CCM .
Mbowe hatapata hasara maana kama ni pesa anazo na pia kiu yake ya kukaa kwenye kiti Muda Mrefu itakuwa imetimia .
Watakaopata hasara na kuumia mioyo yao ni wanachama wa kawaida ambao hawanufaiki na chochote zaidi ya kupinga ufisadi unaonufaisha wachache . Hata Morali wa kupiga Kura utapotea .
Hata Mgombea urais CHADEMA watakosa itabidi Mbowe agombee mwenyewe au agombee Wenje au Sugu au Bony Yai 😂😂😂😂😂😂😂.
Mpaka hapo chama kimeshakufa. Bawacha wamechemka wameweka msaliti wa wazi .
Mwakani CHADEMA litakua na wabunge wachache sana chini ya Mbowe tena wa viti maalumu akiwemo mwenyekiti wa Bawacha ambaye pia atapata uteuzi wa mama Samia . Hata pakiwa na Tume huru CHADEMA haitapata viti vingi maana vijana wengi na wasomi wengi hawataipigia kura maana hakuna watu wenye uwezo wa kuongoza nchi chini ya Mbowe. Lisu hawezi kukubali nafasi yoyote ya uongozi chini ya Mbowe ,hata kugombea ubunge chini ya Mbowe ni kupoteza maana kama amesema hafai kuongiza kwa sababu hana busara unampaje uongozi ?
Lakini Lisu akishinda basi ni wazi CHADEMA itapata viti vingi vya Wabunge hata wa viti maalumu watakua wengi.
Wasira hawezi kukabiliana na Heche milele.
Lakini kwenye uadilifu Wenje hawezi kukabiliana na Wasira .
Mbowe hawezi kukabiliana na Samia kwenye jukwaa wala Wasira maana ni wasafi kuliko Mbowe.
Mbowe akishinda hata kwa haki bado wananchi hawamtaki na hawataki kabisa kusikia habari za CHADEMA ya Mbowe.
Mbowe ajiulize Mbona Lipumba ni yule yule Profesa wa uchumi duniani lakini ameshindwa kuifufua CUF na hana ushawishi kabisa wa kuifufua CUF milele .
Wanaomshabikia Mbowe wanatumiwa kumpotosha ili kuiua CHADEMA . Na watafanikiwa kwa asilimia mia moja endapo wajumbe wataingizwa na Tamaa ya fedha . CCM wana jeuri ya pesa . Hata wakiamua kugawa bili. moja kwa kila mjumbe wanaweza kwa sababu waleshagundua kuwa Mbowe naye ana tamaa ya madaraka kama wao . Sasa ni bora wawape pesa halafu wasipate shida kwenye uchaguzi .
CHADEMA imevamiwa na Rushwa . Kwa sasa wananchi hawana nguvu tena ile waliyokuwa wanabiwa nguvu ya umma . Hakuna cha nguvu ya umma zaidi ya umimi .