Nitawaleteeni makala nzuri kuhusu ulaghai wa wazungu kwa walibya na majuto waliyonayo hii leo ili msije kunasa kwenye mtego uliowanasa Walibya

Nitawaleteeni makala nzuri kuhusu ulaghai wa wazungu kwa walibya na majuto waliyonayo hii leo ili msije kunasa kwenye mtego uliowanasa Walibya

Bro kwani unatuona hatuna akili au vipi?
Mkuu, kuna vitu ambavyo ni very obvious,lakini CCM wanakuwa kama wana mgando wa fikra! Mtu anakwambia mbona Katiba tumeitumia toka kipindi cha Nyerere! Kwa hiyo haihitaji kuangaliwa upya? Najaribu kuvaa miwani ya CCM kuangalia politcs za nchi yetu, nashindwa kuona yadi moja mbele!
 
Ndugu zangu Watanzania,

Wakati wowote ule kuanzia Kesho Nitawaleteeni Makala Nzuri sana ,makali ya kuvutia ,makala ya kutoa Elimu ,makala ya kuwafumbueni Macho ,makala ya kuwaondoeni upofu wa akili na macho. juu ya ulaghai wa Wazungu kwa Walibya na Libya katika Mtego uliotegwa na kuwanasa miguu na mikono Walibya.

Nitawaleteeni Makala na andiko hilo lenye kuonyesha Libya ya Ghadafi ilivyo kuwa Nchi yenye Umoja , mshikamano ,amani ,utulivu , maendeleo na kila aina ya Maendeleo Mpaka kufikia Libya ya leo yenye mgawanyiko na kila aina ya shida na matatizo.

Nitawaelezeni hadithi tamu tamu na maneno matamu matamu waliolishwa ,kukaririshwa na kumezeshwa Walibya ili wampindue na kumuondoa madarakani Hayati Muamari Gaddafi. Kiongozi aliyekuwa na Ndoto na kiu ya kuiunganisha Afrika na kuifanya kuwa Dola moja lenye Nguvu. Kiongozi aliyekuwa na Ndoto ya kuona Afrika inaondokana na utegemezi kwa wazungu na badala yake Afrika itumie rasilimali ilizonazo kuupiga teke umaskini ,kuondoa njaa na kila aina ya utegemezi kwa wazungu.

Kwa bahati mbaya Ndoto hizo zilizimwa kwa mikono ya Walibya wenyewe kwa kudanganywa na mabeberu ambao siku zote hawajawahi kuwa na maombi mema na Afrika tangu enzi na enzi. Hawa Mabeberu waliotesa na kuuwa Babu zetu siku zote hawapendi na kumpenda kiongozi mwenye msimamo,kujitambua na mwenye kutaka kuona Taifa likijitegemea na kuondokana na utegemezi. Ndio maana wakiona kiongozi Mwenye maono na ndoto kubwa aina ya Rais Samia watampiga kila aina ya mawe ,kutoa matamko yenye uongo , uchochezi na chuki tu kama ilivyo kwetu.

Leo hii Walibya wanatamani hata siku zirudi nyuma ili wamlinde Rais wao Gadaffi kwa wivu mkubwa sana. Lakini kwa bahati mbaya hawana nafasi hiyo. Leo wanakesha wanabubujikwa na machozi ya majuto . Kwa kuwa wanashuhudia Taifa lililogawanyika mapande mapande likiwa halina usalama wa kutosha wala utulivu. Leo Libya haina hata kiwanja cha ndege kikubwa kwa kuwa vyote wameharibu kwa mikono yao wenyewe kwa mihemko.

Leo wanamkumbuka namna Gaddafi alivyowapa Elimu bure hadi vyuo vikuu ,huduma bora za afya na maono makubwa ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama ule wa man made river kwa ajili ya upatikanaji wa maji ya uhakika kwa ajili ya matumizi ya binadamu na kilimo .leo wanapitia mateso ya kila aina huku ardhi yao ikiwa ni makazi na maficho ya vikundi vya Kigaidi.

Naomba usipange kukosa makala hiyo kwa kuwa utakuwa umekosa kitu kikubwa sana katika maisha yako. Utapata somo ambalo Walibya walikosa mtu wa kuwapatia. Lakini wewe utabahatika kulipata.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Wasanii wanaamini ccm ni ya milele, shida ndio inaanzia hapo
Cannabis: Mwashambwa kasema CCM itatawala mpaka mwisho wa dunia...@Mwashambwa



 
Ila binadam ni wabinafs sana aisee,yaan mpaka nashangaa

Yaan ccm mpaka leo wanajiona wapo sahihi,aiseee!
CCM ni chama kinachobadilika kulingana na mazingira na wakati na ndio maana kinaendelea kukubalika na mamilioni kwa mamilioni ya watanzania
 
20251206_184735.jpg
 
Mkuu, kuna vitu ambavyo ni very obvious,lakini CCM wanakuwa kama wana mgando wa fikra! Mtu anakwambia mbona Katiba tumeitumia toka kipindi cha Nyerere! Kwa hiyo haihitaji kuangaliwa upya? Najaribu kuvaa miwani ya CCM kuangalia politcs za nchi yetu, nashindwa kuona yadi moja mbele!

CCM kwa muda mrefu si kuongoza, wametawala Tanzania kwa vitisho na ukandamizaji. Sera yao kubwa ni mama mkanye mwanao kama ulivyomsikia kiongozi wao juzi. Silaha yao kubwa ni kuwanyima watazania haki ya kuhoji na kuuliza maswali.
 
Back
Top Bottom