Pre GE2025 Nitawashangaa CCM mkiruhusu Serikali hii iendelee mpaka 2030. Hata 30% ya ilani 2020-2025 haijatekelezwa!

Pre GE2025 Nitawashangaa CCM mkiruhusu Serikali hii iendelee mpaka 2030. Hata 30% ya ilani 2020-2025 haijatekelezwa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

instanbul

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2016
Posts
12,037
Reaction score
17,212
Habari zenu.

Mimi sio mwanasiasa lakini leo kama mtanzania mpenda maendeleo nilidownload ilani ya CCM 2020-2025. Ili walau nipate hope na serikali ya Sasa na kama kweli wanatimiza walichoahidi mwaka 2020 kuelekea 2025.

Aisee nimesikitika sana. Kwa hali hii hatuendi popote kama nchi.

Nimeangalia kipengele kimoja tu cha Ujenzi wa miundombinu katika majiji hasa jiji la Dar. Hakuna kilichotekelezwa kulingana na ilani ya CCM.

Tazama hizi flyover zote zilizoahidiwa kujengwa Dar kati ya 2020 hadi 2025. Na huu ni mfano tu kuwa CCM wajitafakari wakija kuchagua Serikali yao 2025.

Screenshot_20240710-174232.png

Kati ya flyover saba mbili tu ndo zimejengwa na kukamilika. Na leo ni 2024 july.
Ujenzi wa Barabara Dar es Salaam kama wanavyosema kwenye ilani hazijajengwa hata robo yake.

Screenshot_20240710-174348.png

Hebu oneni wenyewe mipango kabambe iliyo kwenye ilani ya CCM 2020-2025. Kama imetekelezwa.

Huko huko CCM mjitafakari kama mtaruhusu serikali hii ya sasa mnayoisimamia kuendelea kutawala mpaka 2030. Tuangalia future ya Taifa hili sio matumbo yetu. Hope mnasikia Wajumbe wa CCM 2025


Ilani yote ya 2020-2025 hii hapa. Isomeni na mlinganishe yaliyotekezwa mpaka sasa mwaka mmoja ukiwa umebaki muda kuisha 2025
 

Attachments

Kwani ni mara ya kwanza, 2020 nilichambua humu jinsi ilani ya CCM haikutekelezwa hata 50% ikiwemo ahadi ya meli 5 kubwa za uvuvi bahari ya hindi na ajira elfu 50 za moja kwa moja kupitia meli hizo!! Lakini CCM sio tu ilirudishwa ila ilishinda kwa 88%!! Kwahiyo hata 2025 mambo ni yale yale itaandaliwa ilani mpya bila kwanza kufanyika tathmini ya mafanikio ya ilani na NEC itawapa ushindi wa 90%!!

Bila katiba mpya hakuna ilani itatakelezwa
 
Ni vile Watanzania hawana akili na hawajui jinsi sisiemu inavyo buruza hii nchi.
NAAIDI TANZANIA TUTAKUWA MASKINI MILELE niko pale ikiwa bado tutakumbatia Chama hiki chenye viongozi hawa
Sijajua kama hata vijana wa Taifa hili wanaisoma hii ilani na kujua kinachoendelea

Solution. Vyombo vya habari ndo kazi yake hio kuhabarisha watu kuhusu hizi ilani kwa watz wote ili wachague na kuassess wenyew
 
Mwanasiasa mzuri ni yule mwenye uwezo wa kuelezea kwa nini hajafikia lengo, na kuonyesha the way forward. Ukishindwa hilo, achana na siasa.

Mbowe alishawahi kuahidi chadema isipochukua nchi anaachana na siasa, chadema haijachukua nchi, na Mbowe anadunda tu katika siasa baada ya kujieleza
 
Miradi ni mingi mno ni over ambitious mno.
Hapana, miradi yote ingetekelezwa kwa fedha za ndani (kodi) na zile za mikopo nafuu.

Lakini kama TRA waziiba fedha za walipa kodi kiasi cha mtu kuficha nyumbani kwake bilioni 7 hii si dalili nzuri.

Ni wazi kuwa mafisadi wasingeweza kumruhusu hayati JPM atekeleze Ilani ya uchaguzi 2020-2025.

Ndo maana walianza mapema kumpiga vita.

Weye wadhani wasanii wangekwenda Korea Kusini wakiandamana na hayati JPM wakitumia fedha za walipa kodi?

Watanzania na waafrika ni watu wa ajabu sana na ndo maana twaonekana wa ajabu hivyohivyo.
 
IIsiendeeeeeeee uipelekeeee wapiii

Tuwapee wale wahunii wa kinoklain??

Ur nt serious ogga
 
Sijajua kama hata vijana wa Taifa hili wanaisoma hii ilani na kujua kinachoendelea

Solution. Vyombo vya habari ndo kazi yake hio kuhabarisha watu kuhusu hizi ilani kwa watz wote ili wachague na kuaccess wenyew
Bado wapiga kura wa nchi hii wana muda hadi uchaguzi wa 2025, hatujachelewa.

Wasome wapitie kila kipengele na kampeni zikianza wamuulize kila mgombeawa eneo husika ni jambo lipi ametekeleza na kama hajafanya hivyo ni kwanini?

Kisha wapiga kura waamue wamchague mgombea huyo au wamchague mwingine.

CCM kwa sasa imejiweka katika wakati mgumu kuliko nyakati zingine zozote.
 
Miradi ni mingi mno ni over ambitious progammes.
Kama waliiandika kwenye plan inamaana waliona wamauwezo wa kuitekeleza na ndo maana watu waliwachagua.

2025 ni kujieleza kwa nini hawajaitekeleza na kwa nini tuendelee kuwachagua
 
Back
Top Bottom