Uchaguzi 2020 Nitawashangaa sana wafuatao wakipigia kura CCM

MANILABHONA

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2015
Posts
462
Reaction score
350
1. Watumishi wa Umma, kwa sababu hawajapewa mishahara na posho zinazostahili kwa miaka zaidi ya 6 iliyopita ukiacha wale wachache wateule.

2. Wanafunzi wa Vyuo vya elimu ya juu kwa mateso wanayopata kupewa mikopo ya kujisomesha.

3. Wazazi wenye watoto maskini waliofaulu kwenda vyuo vya elimu ya juu wakashindwa kuendelea na masomo kwa kukosa mkopo au wzazi wakalazimika kuuza kila walichonacho ili mtoto aende chuo.

4. Wananchi wa mikoa ,hasa iliyoko nyuma kimaendeleo wanaoshuhudia maendeleo yakipelekwa kwa wenzao Chatto, Geita, Mwanza, Simiyu, Shinyanga na maeneo yanayofanana na hayo kwa kukiachwa patupu au kwa kudanganywa kwa peremende, nitakupa pipi n.k (mkandarasi yuko saiti, nitaweka wakandarasi 6 waigawane hiyo barabara, umeme bure kwa sh. 27000/= tu..,tutamtua ndoo mama.

ENDAPO WATAIPA CCM KURA!

Hii itadhihirisha kuwa kweli wako pembezoni/'?/012@#$%
 
Wafanyakazi wote wameongezewa mshahara labda wewe umeajiriwa Chadema kule hawaongezewi
Hawajaongezewa miaka yote minne hata uikiwaongezea leo ina maana gani?

Ujinga tu unakusumbua wewe. Watu hawajaongezewa mishahara miaka yote tena tukiwa hatupo vitani.wengine wakiwa wametolewa kazini kwa majina hewa ilishindikana nn kuongeza mishahara sasa?

KWAKUWA WATUMISHI WA UMMA WAPO TANZANIA INGEKUWA NCHI NYINGINE MNGEJUTA
 
Hawa nafikiri wana jambo lao hapo 28/10. Siri yao na Mungu wao
 
Wewe km umefukuzwa kazi kwa vyeti vya kugushi pole

Kazi sio lazima ofisini tu, kufuga hakuitaji cheti
 
Si ajabu kumkuta Mtumishi wa uma hampendi Magufuli, lakini kura akampa Magufuli kuiokoa CCM.

Kwa sababu CCM yapaswa kuwepo mpaka taifa litakapokuwa imara kukidhi uwezo kutoyumbishwa na badiliko la chama.

Akina LISU na Membe ni wazuri kiuongozi ila vyama vyao kitaasisi viko very very weak kwa kujaza watu wenye mizuka na kimuhemuhe isiyozingatia Objectivity.

Lazaro Nyalandu ameonekana kukulia vizuri kwenye aina ya watu wanaofaa kuwa wengi CHADEMA.

Katika CCM inaonekana wazi kuwa wanaheshimu watu wa aina zote ila kwenye nafasi za kimaamuzi ya ujenzi na usalama wa chama, wapo watu watulivu, isipokuwa tu nafasi ile ya Nnauye, inamfaa mnauye (mwenye uwezo huo), pole pole haina speed ya chama!!!
 
Naunga mkono hoja. Ifikie wakati hiki kikundi kinachojiita ccm, kiwekwe kando ili kipate wasaa mzuri wa kujitafakari. Kwa sasa kimejichokea na kinaiendesha hii nchi kijanja janja tu kupitia porojo na propaganda zilizopitwa na wakati.

Haiwezekani kampeni za mwaka huu ziwategemee wasanii tu ili kuwavutia wasikilizaji. Mgombea wao hana jipya, kila siku stori zake ni zile zile! Elimu bure, sijui kuongeza ndege!!

Cha kufurahisha zaidi, tangu nianze kuzifuatilia hotuba zake, sikumbuki kama kuna siku aliwahi kuwaongelea watumishi wa umma na wale wahitimu wa vyuo anao wasotesha mtaani bila ajira kwa miaka yote hii mitano.
 
Ongezea
5.Wananchi Wa Kagera walioambiwa "Sijaleta tetemeko Mimi"

6.Waathirika Wa bomoabomoa Kimara na Mbezi huku Mwanza wakiachwa kwa sababu walimpa kura "Kamongo".

7. Waathirika wa Korosho na namna walivyokula msoto kwa maamuzi ya kijinga ya bwege mmoja hivi.

8. Wahitimu wa vyuo vikuu wanaosota kitaa bila ajira tangu 2015! Eti wajiajiri!
 
Kwanini wanafunzi wa elimu ya juu wasipige kura kwa Magufuli wakati bajeti ya mikopo imeongezeka!
 
Wafanyakazi wote wameongezewa mshahara labda wewe umeajiriwa Chadema kule hawaongezewi


Kuwa na akili, acha use.nge. Labda limeongezwa TAKO lako, siyo mishahara. Watu wanasota sana kimaisha.
 
Wacha uongo wewe! Waongeze mishahara halafu washindwe kujinadi kwenye kampeni kwamba wameongeza mishahara? 😳😳

Wafanyakazi wote wameongezewa mshahara labda wewe umeajiriwa Chadema kule hawaongezewi
 
Wafanyakazi wote wameongezewa mshahara labda wewe umeajiriwa Chadema kule hawaongezewi

Maccm ni changamoto kwenye hili Taifa! Yaani kupunguza PAYEE kandamizi kwenye mshahara wa mfanyakazi, ndiyo kuongeza mshahara!! Hovyo kabisa wewe.
 
Si ndiyo mnawaita wajinga?

Nchi haiendeshwi kama genge la nyanya hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…