SALOK
JF-Expert Member
- Sep 20, 2011
- 3,364
- 2,001
Kwanza hongera kwa kufaulu hatua hiyo ya kwanza, safi sana!!Asante kwa mara nyigine tena,
Na nimeshajisajili tayari, kwahyo ninakwend kwa hao wakala wakuu wa selcom wananiwekea salio,na je nawapataje ao mawakala wakuu? au kuna option y kuwapata kwenye menu kama mpesa?
nisamehe kichwa kigumu hiki
Kuongeza hazina yako si lazimakwenda kwa wakala mkuu.. Ila wakala mkuu n njia mojawapo unayoweza kununua hazina.
Tumia Mpesa, Tigopesa, Airtelmoney au Eazypesa kununua hazina!!
Jinsi ya kuongeza Salio la hazina.
Ni rahisi sana!!
Mfano kwa airtel money..
Ingia kwenye manu ya airtelmoney (piga *150*60#),
Kisha chagua 5, (lipia bili). Chagua 4 (namba ya kampuni), Utaingiza tarakimu hizi 500600.
Kisha utaweka namba ya kumbukumbu, ambayo ndiyo hiyo uliyojisajilia. Kisha weka no ya siri. Utapata ujumbe wa uthibitisho kulingana na salio/hazina uliyonunua. Msg itatoka airtelmoney na Selcom paypoint...
Ukifungua app utaona balance yako imeongezeka.