Nitoeni hofu, mke wangu amepitiliza mda wa kujifungua

Mparee Halisi

Senior Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
104
Reaction score
8
Habari Wana JF,

Naombeni mnitoe hofu tafadhali, mke wangu amepitiliza mda wake wa kujifungua na makisio yake yalikua tar 28/05 ila mpaka sasa bado na hahisi maumivu yoyote licha tu ya mtoto kucheza ndani.

Mpaka sasa yupo hospitali na ameambiwa njia ziko vizuri na mtoto ameshashuka tayari.
 
Habari Wana JF,Naombeni mnitoe hofu tafadhali,Mke wangu amepitiliza mda wake wa kujifungua na Makisio yake yalikua tar 28/05 ila mpaka sasa bado na hahisi maumivu yoyote licha tu ya mtoto kucheza ndan

Aende kwa doctor, lakini kama haijapitiliza week mbili toka maksio siyo ya kuhofia sana
 
Usifanye masihara na hayo mambo kama imeshindikana kuzaa kawaida apasuliwe la sivyo unaweza poteza viumbe wote wawili!! The early the better.
 
Hapa utapata speculations tu mkuu. Feasible solution ni physical examination ya daktari na kama hakuwa amepiga ultra sound kwa mda mrefu nyuma, ni vema kujua positioning ya mtoto. Wengine huwa wanajisokota na umbilical cord hivyo inawazuia kutoka normal
 
Yupo Hospital almost 2 weeks sasa,Kashaambiwa kua Mtoto yupo tu vizur na hakuna shida yoyote,kinachosubiriwa ni Uchungu tu na zikipita 2 wks kama bado watafanya mikakati mingine
 
wiki ijayo haipiti atakuwa ashajifungua, kama njia iko vizuri na mtoto ameshageuka na kushuka.
 
wiki ijayo haipiti atakuwa ashajifungua, kama njia iko vizuri na mtoto ameshageuka na kushuka.
Mbona kama vile mbal Bro maana makisio yalikua tar 28/05 na mtoto alishuka tangu jmos tar 7/05
 
Ni kawaida mkuu,we sibiri siku yake ikifika atapata uchungu

muda mwingne cc tnakosea kusema uligota lini kuona siku zako wale wanahesabu mie nilienda clinic wakanambia ntajifungua trh kumi na moja nkajifungua kumi na7..
nilikuwa natembea na card ya hosp!!
nenda akacheck na doc sometimes inavuta had wiki 2,doc ndo suluhisho,na usihofu
 

Ina maana Ultra Sound huwa zinadanganya sometimes!?.
back to topic kasema yupo hospital two weeks now.
 
Ina maana Ultra Sound huwa zinadanganya sometimes!?.
back to topic kasema yupo hospital two weeks now.

Ndiyo usiitegemee kwa asilimia 100. Mimi jamaa yangu alipiga akaambiwa ajiandae kwa mapacha na haikuwa hivyo. Na wanaozioperate pia wengi hawajasoma ipasavyo. Nyingi zinaletwa ambazo ni used zimeshachakaa na sio za kisasa, kutokana na ufisadi wetu wa kawaida.
 
Naomba niulize kua akidungwa ile sindano ya kuleta uchungu ina madhara yoyote kwa Mke wangu ambae anasubiria uchungu tu?
 
Sidhan km kuna sindano za uchungu,kuna drip za uchungu..bt ucjal as lng as yupo hosptl under doctrs care utapata mtoto wko tu.usisahau kumuomba Mungu.
 
mke wa brother alijifungua wiki ya arobaini so ucwe na wac mambo kama ayo utokea
 
Nawashukuru sana kwa michango Yenu,tusaidiane kwenye Maombi Tafadhal
 
usiogope mfano mimi tarehe ya makadirio ilikuwa tarehe 14 january na nikajifungua tarehe 31january ikiwa ni week ya 41 kikubwa muombe MUNGU yeye ndio kila kitu.
 
Leo ni wiki ya 42 na siku 1,We are still waiting Guys,Maombi yenu yahitajika bado
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…