Jambo ndugu watanzania wenzangu!
Kuna watu wameteseka muda mrefu sana na wanaendelea kuteseka na magonjwa mbalimbali mpaka leo bila suluhisho na imefikia wakati sasa wanaweza kukata tamaa juu ya maradhi hayo.
Ninaomba tushirikishane hapa hadharani ili tushauriane na kuelekezana nini cha kufanya kulingana na changamoto ya kila mmoja wetu.
Binafsi nina uzoefu wa tiba za mimea na mitishamba katika kutatua changamoto ya maradhi mbalimbali ambayo wakati mwingine yameshindwa kutibika kwa dawa za asili ya kizungu. kwa hiyo ninaweza kukupa A B C ukavuna ili utumie na ninaamini unaweza kupata muujiza wako na ukarudisha tumaini jipya la afya yako.Nina zaidi ya mimea tiba 500 mpaka sasa katika hifadhi yangu binafsi na ninaendelea kujifunza zaidi.Hii inaweza pia kupanua wigo wa watu wengine katika kufanya tafiti zao juu ya mimea na magonjwa.Hata kama kuna mwenye uelewa zaidi au mtaalam tuelekezane hapa aina ya mmea tiba na formula yake katika matumizi ya tiba.
Tafadhali sana mambo ya ramli sitahangaika nayo.Sema ugonjwa unaokusumbua nitakushauri aina ya mimea tiba unayopaswa kutumia kwa utaratibu maalumu ili upone.
Tafadhali mods usiunganishe uzi huu!
Karibuni sana.
Sent from my TECNO BA2 using
JamiiForums mobile app