Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Yapo nyumbani kwangu yananisumbua huwa nayakata hapa naandika reply nipo sehem yalipo bado machanga ngoja yatoe mbegu niyafanyie
Aisee pole sana,kutokujua.Kwa taarifa yako hapo ulipo ikitokea umejikata kwa bahati mbaya na kitu chenye ncha kali mahali popote katika mwili wako,chukua hayo majani mabichi yafinyange vizuri kiganjani mpaka yatoe maji.Hayo maji yake dondoshea kwenye hilo jeraha jipya.Jeraha litakauka kabisa.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ini ini ini

Wanywaji wengi wa pombe hasa hizi kali tuna matatizo ya ini bila kujijua

Story yangu, mwaka juzi nilienda nchi fulan kufanya kazi na ile kazi nilazima upekuliwe ili wajue afya yako,

Ini likaonekana lina matatizo ya mwanzo ila sikua na dalili yoyote. Nilivyopewa dawa ndo kama nikawa nimestua kitu ivi nikaanza kuhisi ini likicheza bila maumivu(nilikua napata maumivu ya woga tu)

Dawa ni kuacha pombe na ini ni miongoni mwa viungo vya binadamu vinavyojitibu vyenyewe.

Ukiwa unakunywa pombe jua kuna kitu unakitafuta na usipokua makini utakipata tu
 
Umeongea point kubwa sana mkuu, sasa mbali na Ini kuna Figo Figo, pombe huchangia kufail kwa figo na Ini pia.
 
Masikio kuwasha na kutoa usaha?
1. Chukua tembe moja ya kitunguu saumu uiponde kisha uchanganye na mafuta safi ya nazi kiasi cha kijiko kimoja cha chakula. Acha mchanganyiko huu ukae pamoja kwa dakika 30 kisha uchuje na kuhifadhi hayo mafuta kwenye kichupa kidogo. Toneza matone matatu ya hayo mafuta kwenye masikio kila siku kabla ya kwenda kulala mpaka mwasho uishe kabisa,

2.Pasha ua la boga joto na baada ya hapo kamulia hilo sikio lenye matatizo.



Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mimi tatizo langu ni ngozi!

Kama unavyofahamu saloon zetu hizi, na mimi mara kadhaa nimekuwa mtu wa safari!

Mwaka 2020, niliotwa vijipele vinavyotoa maji maji (mapunye) sijui nilivipatia wapi, lakini wengi wamehusianisha na saloon ambapo kumekuwa na matumizi ya mashine pasipo kuzifanyia usafi zaidi.

Nimejitahidi kuyatibu mapunye hayo kwa dawa tofauti tofauti, hadi kwa wataalamu wabobezi wa ngozi Hospital, lakini halo bado tete, natimiza mwaka wa tatu sasa bila mafanikio.

Naomba msaada wako!
 
Ngozi mwili mzima,au eneo gani la mwili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…