Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Naomba kujua dawa ya fungus Sugu sehemu nyetii. Dawa zimetumika mda mrefu lakini zinapotea na kurudi
Hii ni simple sana na unapona maisha yako yote.Ni vigumu hata nikieleza hapa hutanielewa.Labda kama utahitaji nikuandalie.Hautatumia tena hizo antifungal za kupaka na kumeza.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Sababu mojawapo ya maambukizi ya bacteria wabaya ukeni ni
Vitanzi,

Sabuni za kikemikali,

magonjwa ya ngono,

wasababishao maambukizi katika via vya uzazi wa mwanamke,,

Kwa suluhisho juu ya PID call 255-719196408 upate tiba
IMG_20230127_110318_457.jpg
 
tunajaribu kuutafta mti huu bila mafanikio yoyote, kama ungeweza kutupa more information kuhusu wapi pakuupata au kama kuna wanao uza zilizo kaushwa na kusagwa tafadhali, nitashukuru sana.
Zilikqushwa na kuandaliwa kwa matumizi zipo za kutosha pia
 
Mungu ni mwema Watanzania wenzangu maana ishara ya baraka kutoka kwake (Mvua) tunaendelea kuishuhudia, mfano hapa nilipo mimi ni tangu asubuhi mpaka sasa inaendelea kunyesha!

Watu wengi sana wanasumbuliwa na magonjwa ya uvimbe katika sehemu mbalimbali za miili yao, inaweza kuwa tumboni, kwenye utumbo, figo, mirija ya uzazi na sehemu nyingine za mwili. Asilimia kubwa hufanyiwa upasuaji ili kuondoa vimbe hizo na wengine kulingana na unyeti wa sehemu zilipo wanaendelea kuishi kwa matumaini ya kutumia vidonge vya kutuliza maumivu huku siku zikisogea,na asilimia ndogo hupata suluhisho kupitia tiba mbadala na kupona kabisa bila kufanyiwa upasuaji wowote.

Mti huu wa Nsuha (rejea katika picha) unafanya kazi hii ya kuondoa uvimbe mwilini kwa ufanisi mkubwa sana kama utazingatia uandaaji na matumizi yake, kila sehemu yake ni dawa lakini kwa mimi hapa nazungumzia mizizi yake. Mizizi yake huvunwa na kukaushwa (siyo juani) vyema ili isipoteze ubora na baadaye husagwa vizuri kwa ajili ya matumizi.

Mtu mwenye uvimbe wa aina yoyote anaweza kuitumia kwa muda wa mwezi mmoja tu akapata nafuu na kupona kabisa tatizo. Asubuhi na jioni kijiko kimoja cha chai katika maji moto ama uji. ACHA KUPUUZA NA KUDHARAU VITU.

Kuna miti mingi sana yenye uwezo wa kuondoa kabisa vimbe sugu katika mwili wa binadamu, na inaweza hata kuchanganywa miwili ama mitatu kwa ufanisi na ikatoa matokea makuu sana kwa ajili ya kujifunza tutajifunza mmoja baada ya mwingine. Usiogope kujaribu mitishamba ni hazina kubwa sana.

Mungu akubariki!

Ezekiel 47:12.

View attachment 2086499
Huu mti twiga wanakula majani yake huko maporini.
 
Huo mti unaitwa Totilis sema kuna spices kama 180 hvi sasa sijajua kama ni zote zina tibu . Ni kweli n chakula pendwa cha twiga kama mdau hapo juu alivyosema
1b0d334bc2f4139634e57f3b036d0f6d.jpg
 
Jambo ndugu watanzania wenzangu!
Kuna watu wameteseka muda mrefu sana na wanaendelea kuteseka na magonjwa mbalimbali mpaka leo bila suluhisho na imefikia wakati sasa wanaweza kukata tamaa juu ya maradhi hayo.

Ninaomba tushirikishane hapa hadharani ili tushauriane na kuelekezana nini cha kufanya kulingana na changamoto ya kila mmoja wetu.

Binafsi nina uzoefu wa tiba za mimea na mitishamba katika kutatua changamoto ya maradhi mbalimbali ambayo wakati mwingine yameshindwa kutibika kwa dawa za asili ya kizungu. kwa hiyo ninaweza kukupa A B C ukavuna ili utumie na ninaamini unaweza kupata muujiza wako na ukarudisha tumaini jipya la afya yako.Nina zaidi ya mimea tiba 500 mpaka sasa katika hifadhi yangu binafsi na ninaendelea kujifunza zaidi.Hii inaweza pia kupanua wigo wa watu wengine katika kufanya tafiti zao juu ya mimea na magonjwa.Hata kama kuna mwenye uelewa zaidi au mtaalam tuelekezane hapa aina ya mmea tiba na formula yake katika matumizi ya tiba.

Tafadhali sana mambo ya ramli sitahangaika nayo.Sema ugonjwa unaokusumbua nitakushauri aina ya mimea tiba unayopaswa kutumia kwa utaratibu maalumu ili upone.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Taja ugonjwa uliokusumbua na namna ulivyopona... Yani dawa iliyokuponyesha.

Mimi nilisumbuka na vidonda vya tumbo kiasi kwamba ilifika mahali ikawa haja kubwa inatoka na damu, nikaishiwa hadi damu ila nikaja kusoma hapa jamiiforum kwamba mashona nguo ni dawa ya vidonda vya tumbo.
Nikatumia kama ilivyoelezwa kwamba ni asubuhi kwa siku 3, sasa nilituma siku mbili tu nikapona na mpaka leo nipo fiti hadi pombe kali nagonga, maharage, pilipili na mazagazaga ya aina zote.

Kuna watu wanasumbuka na kuingia gharama hata za mamilioni kumbe nje kwake kuna dawa ya muda mfupi tu ambayo unakuta ni majani yamejiotea tu

Hayo mashona nguo nilitumia siku 2 nikaacha kutokana na hofu sababu mwelezaji aliweka tahadhari kwamba ukitumia muda mrefu yanasababisha kuwasha kwa figo

images (9).jpeg
 
Hayo mashona nguo mti wake si una miba mina?
 
Back
Top Bottom