Niulize chochote kuhusu biashara ya duka la rejareja

Unauza bidhaa gani mkuu nimetamani kujuaa
Nauza mahitaji ya nyumbani,na bidhaa ninazouza sana ni sukari,ngano,mafuta ya kula,sabuni,Mchele,sembe,ni bihaa mhimu sana ambazo ukifungua duka tu lazima uuze mathlani sukari kg 50 nauza Kwa kuipima na naimaliza within a day,Pia nawarahisishia wateja wangu hata wa kipato Cha chini nawahudumia,mf.nauza mpaka sukari ya 300,500, vivyo hivyo katika mafuta,jambo hili limeniongezea wateja sana na kuongeza mauzo
 
Mwanzoni ulivyoanza ulikuwa unauzaje?
 
Na Mimi napenda kufungua duka Ila changamoto Ni wamama hapa mtaani.

Nashindwa kabisa kuwanyima bidhaa wakija kukopa.
Hili linanikumba mimi pia mtu anakuja kwa huruma ila kulipa ni shida inabidi abadili duka kukwepa deni , kukopea ni kufukuza wateja.
 
Hili linanikumba mimi pia mtu anakuja kwa huruma ila kulipa ni shida inabidi abadili duka kukwepa deni , kukopea ni kufukuza wateja.
Yani ukimkopaa kesho unamuonaa yule anapitaa anaenda duka la jiranii[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mi ninaduka,ni ukweli duka la rejareja linalipa sana Tena sana Cha msingi ni location na usimamizi mzuri,mie 2018 nilianza duka Kwa 1.8mil.kwa Sasa 2023 Hali SI mbaya mauzo per week yanarange 10-15mil,
Daah unamtaji wa kiasi gani kwa mauzo hayo ya karibia milion 2 kwa siku?
 
Sijawahi kufikiria kufungua duka maana naona kama vle faida ni ndogo sana. Nimepatapata madini kwenye uzi huu
 
Hiyo sukari ya 300&500 unaipima vip?!
 
Hiyo sukari ya 300&500 unaipima vip?!
Sukari ya sh 500 ni g 150 na Kuna zilizopekiwa tayari Kwa ujazo wa g 150 na unaweza kupima wewe mwenyewe Kwa ujazo huo ingawa siku hizi sukari ya ujazo huo tunauza sh 600. Ila hiyo sukari ya sh 300 hata mimi nahitaji uzoefu .
 
Safi
 
Kufungua duka na kumuajiri mtu auze, hapa hua mnapigiana vp hesabu? I mean kujua faida, vitu vilivyoisha na vinavyohitajika kuongezwa dukani. ..

Unaepuka vp huyu uliyemwajiri asikupige?
Swali zuri.
 
Umenena vyema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…